Mbona hayo yote unayosema kuwa Ndugai ni weak nishayaandika hapo juu, umenifuatilia vizuri au ndiyo kwanza unaanza kusoma post hii?
Mimi nasema hivi, ukikubali kujiuzulu, katika mazingira kama haya aliyojiuzulu Ndugai, ni kama vile umeenda mahakamani ukakubali guilty plea, kwamba wewe una makosa, kwa namna moja au nyingine. Ukipigwa kifungo baada ya kukiri una makosa, huna nafasi ya kujitetea kuwa umelazimishwa kukiri makosa. Kama huna makosa dindisha tu, usikubali makosa yasiyo yako.
Preet Bharara alielewa hili, ndiyo maana alimgomea Trump kujiuzulu baada ya figisu za Trump. Akamwambia Trump kama unataka nifukuze kazi, watu wote wajue umenifukuza kazi. Watu wana haki ya kujua ukweli na kuepushwa na speculations.
Trump akamfukuza kazi. Bharara katufanyia haki watu, tumejua wazi Trump kamfukuza kazi, hiyo haina chengachenga watu waanze kufanya speculations.
Ndugai hajatufanyia haki, hata kama kalazimishwa kujiuzulu, habari hizo haziko wazi, ni speculations tu.
Hata yeye Ndugai hajawahi kusema kwamba kalazimishwa kujiuzulu.
For all I know, hii habari inaweza kuwa kampeni za kisiasa za kumdhoofisha Samia, watu wanapigania urais 2025. Wewe hujiulizi, Ndugai kashajiuzulu, kwa nini hii habari inaibuliwa sasa?
I mean I am not a Samia fan, but let's look both ways. Hii habari ina significance gani wakati huu kama si siasa za urais 2025 baada ya Samia kuonekana ana consolidate power kwenye mkutano wa CCM?
Kama huna makosa, usikubali guilty plea. Kama huna makosa na umesimamia kitu cha haki, hujiuzulu, unapingana na rais kwa kusimamia unachoona sawa. Hata rais akikuonea, watu wote waone. Siyo unajiuzulu halafu unalalamika chinichini kuwa umelazimishwa kujiuzulu, kwa namna ambayo haina rekodi na imejaa speculations.
Haya si maneno "idealistic" tu, haya ni mambo ambayo nimeyaona nyumbani kwetu.
Mimi kuna mzee wangu mmoja alikuwa ni mteule wa rais. Akapingana na rais. Akasema sera hizi ni mbovu. Kwenye hotuba live.
Akasema kashafunga virago kama kazi kufukuzwa na afukuzwe.
Watu wakamfuata rais Mkapa, wakamwambia huyu bwana kakukosea heshima, mtimue kazi.
Rais Mkapa akasema muachieni huyu bwana, amefanya sanaa ya hali ya juu (kwa kuwa alisema ana confidence kuwa rais Mkapa anapenda watu wanaomuambia ukweli, Mkapa akaona akimfukuza kazi atakuwa kaharibu hiyo sifa yake).
So, matokeo yake huyo Mzee kafanya kazi mpaka kastaafu, wala hajasumbuliwa, tena kabla ya hiyo hotuba alikuwa anasumbuliwa, baada ya hiyo hotuba hakusumbuliwa kabisaa.
Unaona kabisa huyu mtu anasimamia principle, kampa mazima Mkapa, rais aliyeogopwa na wengi. Tena kampa mazima wakati akiwa ni presidential appointee, sio kama Ndugai kiongozi wa muhimili huru..
Tatizo Watanzania tumeshajikubalia kwamba watu hawawezi kusimamia principle.
Kina Ndugai wanatuchezea michezo ya kuigiza.