Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?
Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama.
Na hata wangemvua uanachama, hilo lingemuondolea ubunge tu, kuwa Spika wa bunge sio lazima uwe mbunge.
Marehemu Dr. Aleck Che Mponda aligombea Uspika bila ya kuwa mbunge.
Ndugai kwa njia moja au nyingine alikubali kujiuzulu yeye mwenyewe.
Kuna mtu anaitwa Preet Bharara, huyu alikuwa US State Attorney for the Southern District of New York, a presidential appointment. Rais Trump alikuwa hampendi, akawa anamfanyia figisu ajiuzulu. Jamaa likasema sijiuzulu ng'o, nataka nione unanifukuza kazi, dunia nzima ijue nimefukuzwa kazi na Trump, sijajiuzulu.
Trump akamfukuza kazi, dunia nzima ikajua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.
Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?