🤣🤣🤣ubabe ubabe tuUnaamka asubuhi unakuta barua yako ya kujiuzulu inasambaa mitandao, unashangaa "mbona mimi sijaandika hiyo!!". Alafu watu wanakiri wameshaipokea na michakato ya chama imeanza.
Unataka kutoka nje labda uongee na vyombo vya habari unakuta umewakwa chini ya ulinzi nyumbani kwako, ni umafia yaani.
Wanasema ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga, maza asisheshangaa nayeye yakimkuta ya 'kujiuzulu' akiwa amewekwa mtu kati na 'wazalendo'.
Sawa.Kuwa spika ni lazima uwe sponsored na Chama cha siasa ata kama wewe si Mbunge
Sema wanaccm usitutaje sisi watanzania. Maovu ya Ndugai yanajulikana ndio maana hakuna aliyemuonea huruma wala kumtetea.Mkuu, Watanzania ni WANAFIKI sana! Kwa wakati ule, kelele zilikuwa kila kona za kumtuhumu! Wabunge wengi wakageuka kuwa ni CHAWA wa MWENYE NGUVU kuliko SPIKA.
Ni afadhari alivyojiuzulu "mwenywe",kwani alikuwa anaelekea KUAIBISHWA!
Kama unaingia kazi za uwakilishi wa watu kwa kuangalia maslahi ya familia, uko katika kazi isiyohusika na lengo lako.Halafu nani alee familia yake...!!???
Kiranga we ni mtu makini sana hoja zako zinakufanya uonekane kama mtu wa kawaida hapa JF.Kama angekuwa na hoja nzito zenye mashiko kwa wananchi, angepata chama cha kum sponsor au hata kuanzisha faction ndani ya CCM kumpa support.
Katiba ya Tanzania haimruhusu rais kumuondoa Spika. Unless avunje bunge na kuitisha uchaguzi mpya kwa namna ambayo hata yeye rais anaenda kuchaguliwa tena.
Sasa katika hili katiba yetu imempa nguvu vipi rais kumlazimisha Spika ajiuzulu?
Mkuu Kiranga nahisi unakosea kusema hayo.Ndugai alikuwa mkuu wa muhimili, analazimishwa vipi kujiuzulu bila ya kura ya bunge kutokuwa na imani na Spika?
Angekataa kujiuzulu tuone kama wangemvua uanachama.
Na hata wangemvua uanachama, hilo lingemuondolea ubunge tu, kuwa Spika wa bunge sio lazima uwe mbunge.
Marehemu Dr. Aleck Che Mponda aligombea Uspika bila ya kuwa mbunge.
Ndugai kwa njia moja au nyingine alikubali kujiuzulu yeye mwenyewe.
Kuna mtu anaitwa Preet Bharara, huyu alijuwa US State Attorney for the Southern District of New York, a presidential appointment. Rais Trump alikuwa hampendi, akawa anamfanyia figisu ajiuzulu. Jamaa likasema sijiuzulu ng'o, nataka nione unanifukuza kazi, dunia nzima ijue nimefukuzwa kazi na Trump, sijajiuzulu.
Trump akamfukuza kazi, dunia nzima iksjua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.
Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?
Hapa ninachoona kimetokea ni hiki, ni uozo juu ya uozo juu ya uozo, hakuna kitu kilichotokea kwa principle.Mkuu, Watanzania ni WANAFIKI sana! Kwa wakati ule, kelele zilikuwa kila kona za kumtuhumu! Wabunge wengi wakageuka kuwa ni CHAWA wa MWENYE NGUVU kuliko SPIKA.
Ni afadhari alivyojiuzulu "mwenywe",kwani alikuwa anaelekea KUAIBISHWA!
You could be very right.Labda kasahau "If you live in a glasshouse, don't throw stones".Ndugai alikuwa fisadi na kapiga hela za kutosha sana Bungeni. Who knows? Perhaps alikuwa blackmailed. Uresign na kusepa silently or else..
OK, kwa hiyo ushatoka kwenye katiba umeenda kwenye habari ya kwamba rais wa Jamhuri ni mwenyekiti wa CCM pia?Rais wa Tanzania ni mwenyekiti wa CCM pia.
Na ni vigumu kuitofautisha CCM na dola.
Sawa. Tunakubaliana Ndugai ni fisadi.Kwa ufujaji wa pesa za umma aliofanya hui ujasiri unaotaka aoneshe angeutoa wapi? Ulitaka Mwenzio akanyee debe?
Sawa.Kwa cheo cha urais hapa kwetu, urais uko juu ya katiba. Kwenye makaratasi ndio inaonyesha rais hawezi kumuondoa spika. Lakini kiuhalisia rais anaweza kumuondoa yoyote kwenye cheo chake, kwa njia halali na zisizo halali. Haya tunayaona kwa macho yetu. Rejea sakata la CAG Profesa Assad.
Mimi hapa naona tatizo ni kwamba Ndugai ni mnafiki tu.Mkuu Kiranga nahisi unakosea kusema hayo.
Unajua Katibabya Tanzania imetengeneza umungu kwa mtu anayekalia kiti cha urais.
Ndugai hakuwa na namna maana tayari wabunge walishapangwa kuanzisha hoja ya kutokuwa na imani naye.
Wapo waliomtuhumu kutaka kuwatweza utu wao yaani wanawake.
Maandalizi ya kura kutokuwa na imani naye ilishakamata kasi
Sawa.
Lakini kama mtu anasimamia principles zake za msingi, kwa nini aogope rais kumuondoa kwenye cheo?
OK, kwa hiyo ushatoka kwenye katiba umeenda kwenye habari ya kwamba rais wa Jamhuri ni mwenyekiti wa CCM pia?
Hili jambo halipo katika katiba, na tushakuwa na rais wa Jamhuri Mwinyi na Mwenyekiti wa CCM Nyerere.
So, katiba si issue au ni issue hapa?
Naam. Nakubaliana na wewe.Ndugai hajawahi kusimamia principles ndio maana ilikuwa rahisi kung'oka.
Kwa hiyo unakubali Ndugai hakusema habari za deni kwa kuwa ni idealistic defender of fiscal responsibility?Katiba ni issue kwa sababu lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa ili uwe mbunge au spika. Haiwezekani kuwa na kina Kyrsten Sinema, Joe Manchin, Angus King au Bernie Sanders katika bunge la Tanzania. Kama Ndugai asingejiuzulu mwenyewe wala hata isingefikia kura hatua ya wabunge wote kupiga kura ya kuamua abaki au aondolewe.
Kiranga unalitazama suala la Ndugai ki "idealistic" zaidi. Hii bado ni Tanzania ile ile ya Nyerere ya chama kushika hatamu.