Jinsi ‘mikono’ ya Serikali ilivyotishia uhuru Bunge sintofahamu ya kujiuzulu Ndugai

Kwa hiyo unakubali Ndugai hakusema habari za deni kwa kuwa ni idealistic defender of fiscal responsibility?
Kiranga we ni mtanzania mwenzetu kweli au una uraia wa nje,Tanzania Rais ni mungu mtu akitaka ufe keo utakufa tu.
Tanzania huwezi kujiuzulu mwenyewe kwa cheo chenye ulaji na utukufu kama uspika,
Ndugai ni weak sana hana sifa ya kuwa speaker.samuel sitta ndio alikuwa na uwezo wa kudinda mbele ya mtu yeyote
 
Mbona hayo yote unayosema kuwa Ndugai ni weak nishayaandika hapo juu, umenifuatilia vizuri au ndiyo kwanza unaanza kusoma post hii?

Mimi nasema hivi, ukikubali kujiuzulu, katika mazingira kama haya aliyojiuzulu Ndugai, ni kama vile umeenda mahakamani ukakubali guilty plea, kwamba wewe una makosa, kwa namna moja au nyingine. Ukipigwa kifungo baada ya kukiri una makosa, huna nafasi ya kujitetea kuwa umelazimishwa kukiri makosa. Kama huna makosa dindisha tu, usikubali makosa yasiyo yako.

Preet Bharara alielewa hili, ndiyo maana alimgomea Trump kujiuzulu baada ya figisu za Trump. Akamwambia Trump kama unataka nifukuze kazi, watu wote wajue umenifukuza kazi. Watu wana haki ya kujua ukweli na kuepushwa na speculations.

Trump akamfukuza kazi. Bharara katufanyia haki watu, tumejua wazi Trump kamfukuza kazi, hiyo haina chengachenga watu waanze kufanya speculations.

Ndugai hajatufanyia haki, hata kama kalazimishwa kujiuzulu, habari hizo haziko wazi, ni speculations tu.
Hata yeye Ndugai hajawahi kusema kwamba kalazimishwa kujiuzulu.

For all I know, hii habari inaweza kuwa kampeni za kisiasa za kumdhoofisha Samia, watu wanapigania urais 2025. Wewe hujiulizi, Ndugai kashajiuzulu, kwa nini hii habari inaibuliwa sasa?

I mean I am not a Samia fan, but let's look both ways. Hii habari ina significance gani wakati huu kama si siasa za urais 2025 baada ya Samia kuonekana ana consolidate power kwenye mkutano wa CCM?

Kama huna makosa, usikubali guilty plea. Kama huna makosa na umesimamia kitu cha haki, hujiuzulu, unapingana na rais kwa kusimamia unachoona sawa. Hata rais akikuonea, watu wote waone. Siyo unajiuzulu halafu unalalamika chinichini kuwa umelazimishwa kujiuzulu, kwa namna ambayo haina rekodi na imejaa speculations.

Haya si maneno "idealistic" tu, haya ni mambo ambayo nimeyaona nyumbani kwetu.

Mimi kuna mzee wangu mmoja alikuwa ni mteule wa rais. Akapingana na rais. Akasema sera hizi ni mbovu. Kwenye hotuba live.

Akasema kashafunga virago kama kazi kufukuzwa na afukuzwe.

Watu wakamfuata rais Mkapa, wakamwambia huyu bwana kakukosea heshima, mtimue kazi.

Rais Mkapa akasema muachieni huyu bwana, amefanya sanaa ya hali ya juu (kwa kuwa alisema ana confidence kuwa rais Mkapa anapenda watu wanaomuambia ukweli, Mkapa akaona akimfukuza kazi atakuwa kaharibu hiyo sifa yake).

So, matokeo yake huyo Mzee kafanya kazi mpaka kastaafu, wala hajasumbuliwa, tena kabla ya hiyo hotuba alikuwa anasumbuliwa, baada ya hiyo hotuba hakusumbuliwa kabisaa.

Unaona kabisa huyu mtu anasimamia principle, kampa mazima Mkapa, rais aliyeogopwa na wengi. Tena kampa mazima wakati akiwa ni presidential appointee, sio kama Ndugai kiongozi wa muhimili huru..

Tatizo Watanzania tumeshajikubalia kwamba watu hawawezi kusimamia principle.

Kina Ndugai wanatuchezea michezo ya kuigiza.
 
Lakini ujue ndugai alifanya makosa,kiongozi mkubwa kama ndugai kumkosoa rais au utendaji wa serikali ni makosa makubwa sana huku afrika,haina tofauti ba uhaini,kama ni rwanda ndugai angekuwa matehemu,so ndugai was guilty
 
Ulitaka wamkolimbe!?
 
Yaezekana alitengenezewa mazingira threat ya kwake au wanafamilia serikali hawashindwi kufanya umafia akaona isiwe taabu
Kuna taarifa za chinichini kwamba viongozi karibia wote huwa wanafuatiliwa kwenye mambo yao binafsi wanapokuwa kwenye hali ya kawaida hasa ya sirini.
System yaweza kuwa na picha zako uko faragha na mchepuko ukiwa ziarani popote na pengine unapiga Tigo au aibu nyingine.
Sasa wakitaka ufanye jambo na unapinga basi wanakuonyesha jee zitolewe?
Jibu unalo!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Trump akamfukuza kazi, dunia nzima iksjua Preet Bharara amefukuzwa kazi na Donald Trump.

Kwa nini Ndugai hakusimamia anachoamini na kukataa kujiuzulu mpaka afukuzwe tuone kafukuzwa clearly bila chengachenga?

Mkuu hivi kweli unalinganisha matukio ya kisiasa ya US na ya hapa kuzimu Tanzania?

Ndugai angejaribu kudinda kuachia kiti muda huu angekuwa kapumzishwa kwa amani.
 
Kiranga usemayo ni kweli, lakini shida ni kuwa pamoja na msimamo wake ulikuwa sahihi na angeusimamia vyema lazima angepata support ya wananchi kwani ni ukweli bado yeye binafsi ni mchafu sana.
Ripoti ile ya CAG kuhusu ubadhilifu wa pesa za matibabu mabilioni kadhaa India bila backup ya chama na serikali hii ji suala la kuwa jela directly.
Jee alikuwa tayari kwa hilo? Ndugai hakujipanga na wakatumia udhaifu wake kumsulubu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
We unadhani Crown peke yake ndio inashika moto?...Ata V8 zinaungua pia... Tanzania sio kama uijuavyo...
 
Ndi
Ndio maana alikosa jeuri na serikali ilifanya vile ikijua hana pakutokea ana machafu mengi
 
Lakini waswahili Wanasemaga “ siri ya mtungi aijuaye ni kata “ kata ndio anayejua ndani ya mtungi huwa kuna kitu gani. !!
 
R. I. P Samuel Sitta Mzee wa viwango na spidi !!
 
Naomba uzi huu ufungwe kwa comment hii tu
 
Kwa nn sasa hii hoja? Ndio mjue kampeni zimeanza tayri. Na hajawai sema haya ww unahisi hisi tu
 
Lakini waswahili Wanasemaga “ siri ya mtungi aijuaye ni kata “ kata ndio anayejua ndani ya mtungi huwa kuna kitu gani. !!
Mkuu, kwa maneno hayo anything goes.

Unaweza hata kudai kwamba wewe ni baba wa baba yako, kwa sababu "siri ya mtungi aijuaye ni kata". Watu wa nje tunamjua yule baba yako, kumbe wewe ndiye baba yake huyo tunayemjua baba yako.

Au siyo?

That is neither here nor there and therefore utter meaningless.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…