Jinsi ‘mikono’ ya Serikali ilivyotishia uhuru Bunge sintofahamu ya kujiuzulu Ndugai

Sawasawa..
 
Ndio hivyo
 
Ndungai alikubali kujirahisisha mwenyewe kwa kukubali kutumiwa na yule dhalim kama houseboy wake na kuligeuza bunge kama kitengo cha Ikulu, asingekubali ujinga ule wa dalim asingechezewa hivi. Ndungai alivuna alichopanda
 
Kama Ndugai angethubutu kukosoa kama vile wakati wa Magufuli kisha tukaona kajiuzulu basi pengine asingeonekana kuwa ni dhaifu au kusema machafu yake ndio yaliyofanya aogope na kujiuzulu, tungemuona ni shujaa kwa kumkosoa Jiwe na sasa lawama zingekuwa zote kwa Magufuli tu kwamba anaminya uhuru wa kutoa maoni.

Kwangu mimi kitendo cha Ndugai ni kitendo cha ujasiri hasa kwa mazingira yetu bila kujali huko nyuma alikuwa vp au ana machafu gani, alikuwa anao uwezo wa kunyamaza na kuendelea kula mema ya nchi ingekuwa ni manufaa kwake.
 
Katiba ya Tanzania haimruhusu rais kumuondoa Spika. Unless avunje bunge na kuitisha uchaguzi mpya kwa namna ambayo hata yeye rais anaenda kuchaguliwa tena.

Sasa katika hili katiba yetu imempa nguvu vipi rais kumlazimisha Spika ajiuzulu?

Rais ni mwenyekiti Pia wa CCM, hivyo hata kama Hana Mamlaka ya kumuondoa Spika kwa cheo chake cha Urais, anaweza kumfukuza uanachama na kumnyang'anya kadi. Hapo Automatically hawezi kuwa Spika tena, Kwa sababu aligombea uspika akiwa Chini ya udhamini wa chama.
 
ina maana Ndugai alikuwa hajui alipo Tundu Lisu hadi akamvua ubunge?
Huyu si ndo yule aliyesema atake asitake tutamlazimisha kuongeza muda? mbona hajakataa asife?
 
ccm kwenye kushika utawala wa nchi ni wajanja sana. Watagawanyika lakini kwenye jambo lao watabaki salama dhidi ya adui wao ambaye ni mwananchi.
Tatizo wananchi wanawaamini sana maadui zao.
Upinzani nao umekosa focus!
 
Nilikusudia kwamba sababu iliyomfanya asigome kujiuzulu ni kwa sababu yeye ni kama kata anajua vizuri yaliyomo kwenye mtungi si mazuri kwa afya yake kama akishupaza shingo !!
 
We unabwabwaja tu huna unalojua.
 
Ndugai alikuwa fisadi na kapiga hela za kutosha sana Bungeni. Who knows? Perhaps alikuwa blackmailed. Uresign na kusepa silently or else..
ndicho alichofanyiwa, kaletewa faili meza la maufisadi yake yote, akaambiwa achaguee jela maisha au ajiuzulu smoothly, aka-opt kujiuzulu
 
Na huo ndio ukweli mchungu !!
 
Tatizo la Tanzania ni watu wenyewe. Hata uwape katiba mpya bado kuifata mtihani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…