Jinsi Mpesa ilivyofanikiwa Afrika ikashindwa kwenye soko la Ulaya - Funzo wa madevelopers

Kwa investor sio kwa user.
Mfano kuweka huduma ys Mpesa kijiji x ni cheap kuliko ATM machine. Bado ATM inahitaji ulinzi, umeme, services no, wakati mpesa unaondoka na simu yako.
Jambo kubwa ni kutunza tech zao tu hakuna lingine.
Infrastructure zao wanatumia gharama kubwa wakati Mpesa unaatumia mitambo ileile iliokuwepo zamani na huna haja ya internet
Ukifanya critical analysis ni kulinda kampuni zao tu, hayo mengine ni kujifariji tu.
 
Investor anaangalia demand ya watu. Hufuati matakwa yako bali matakwa ya walaji. Kwa mfano, initial plan ya mpesa ilikuwa ni kwa ajili ya taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo ziweze kuwa na access ya kuwatumia mikopo watu wasiokuwa na akaunti benki na kwa bei nafuu. Ila watu wakaibadili matunizi ikawa njia ya kutumiana pesa. Ndipo sasa safaricom wakaisitisha huduma na kuamua kuiunda upya ili kuendana na matakwa ya watu. So innovation inafuata mahitaji ya watu sio matakwa ya mwekezaji.
 
Mpesa ni mfuko umekaa kimasikini maskini sana..huwezi kukuta Ulaya na Marekani wao mambo ya financial inclusion wako mbali sana...huku africa ni watu wangapi wako kwenye mfumo wa banki? Wangapi wanalipa kodi? ....wenzetu wameendelea sana mpesa ni sign ya umasikini.
Wao kila kitu kuhusu manunuzi ,mikopo,kodi etc its simple coz ya mfumo wao wa kifedha...
 
Nakwambia hio mifumo unayoitetea ingekuwa rafiki kiuchumi ingesambaa vijiji vyote ila kwa gharama zake za uendeshaji imeishia kwenye mabenki kwenda nje ya bank imeshindikana.
Mpesa imesambaa kutokana na unafuu wake hakuna lingine.
Nimekupa mfano wa max malipo ambao ni mfumo copy ya ulaya ulifeli kutokana na gharama zake.
Wazungu wapo tayari kulinda tech zao hata kama ni za gharama.
Nilikupa mfano wa 5G ya china na Ulaya, ya ulaya ina gharama lakini wazungu wameikumbatia tu kwa sababu ni ugunduzi wao.
Wazungu bado wapo ktk fikra za karne ys 19 "Whiteman supremacy" bado wanawaza kuwa superior hata walipozidiwa. Endelea kutetea mambo yao mie naishia hapa.
Kajifunze kwenye makala zinazojadili kwa nini Detroit city ilikufa.
Au kwa nini British empire ilikufa.
Binafsi sishangai wazungu kuikataa tech ilioanzia Afrija.
Hata mazao yetu huyakataa na kununua kwa bei ya chini, wewe endelea kuamini unavyoamini lakini wazungu wana secret agenda nyingi sana dhidi ya watu wengine ila kwa macho ya juu watu kama nyie huwaami.
Sijii kwa nini sisi watu weusi hatutaki kujifunza kutokana ba matukio na matendo ya wazi ya hao watu.
 
Mkuu hivi tumeelewana kweli? Mpesa tu imefail hapo south kwasababu zaidi ys 50% ya wasouth wana bank account. Japo vodafone iliimpliment mpesa south kwa kushirikiana na benki ya pili kwa ukubwa south bado ilifail ikabidi huduma waifunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…