Jinsi Mungu alivyombariki mtu mweusi. Namna Biblia inavyomuongelea mtu mweusi

Jinsi Mungu alivyombariki mtu mweusi. Namna Biblia inavyomuongelea mtu mweusi

05CUBA

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2025
Posts
1,106
Reaction score
1,650
Uzi huu natamani hata usomwe na mtu mmoja tu ntafurahi,
Ilimradi mtu huyo mmoja spare ufahamu juu ya ukweli juu ya Baraka alizokirimiwa mtu MWEUSI na namna mtu mweus alivyo ongelewa kwa uzuri ktk biblia .

Kuanzia sa nne naanza kupost taratibu, Sasa uuonapo Uzi huu comment kitu chochote ili kuusubcribe namimi nikianza kuflow ntaku mention au kureact kwa comment yako.

Tunaenda kifungu Hadi kifungu wazee ... Nnashida na mtu mmoja tu aondokane na wazo kuwa watu weus walilaaniwa.
 
Unauliza majibu mkuu kama watu wana kila kitu wao ndio wanaenda kuomba msaada tena si laana hiyo..
 
Mungu ajalaani race yeyeto hizo ni propaganda tu za wabaguzi.
Kama tumelaaniwa mbona tumepewa kila kitu.
Tungekuwa na laana tungeshushiwa mitume, mitume walishushwa kwenye jamii zenye maasi mfano mashariki ya kati.
Tungekuwa na laana tusingepewa raslimali tele.
Tungekuwa na majanga makubwa ya asili nk.
Hakuna sehemu yeyeto kwenye maandiko eti mwafrika alilaaniwa
 
Je MUNGU aliwahi umba watu weusi na WAZUNGU separately ?

No hajawahi umba watu separately aliumba mtu mmoja Ila kutokana na tofauti za kitabia na myenendo iloambatana na mazingira nayo watu baada ya kuzaliana waliishi ndiyo yaliwatofautisha.

SWALI : mtu wa kwanza alikuwa wa rangi gani ?

Jibu: hakuna ushahidi wa moja kwaoja Bali Kuna nadharia zinazoeleza rangi ya mtu wa kwanza ilikuaje,

Binafsi naiamini nadharia inayosema kuwa mtu wa kwanza alikuwa wa dhambarau na si mweupe Wala mweusi.

SWALI : biblia inasemaje juu ya uwepo wa watu kwa rangi tofauti ?

Jibu: hakuna sehem watu wanatamkwa kwa rangi zao mpaka pale ilipofika muda na nyakati watoto wa NUHU wanapoanza kuelezewa haswa kwa majina yao katika mwanzo 1:9 na in specific pale mwanzo 1:10 majina Kama HAMU (baba wa watu weusi) na majina Kama Kush, putu,Misri(MIZRAIM) na kaanani yalipoibuka na kuonekana Yana rejelea Weus wa rangi wa watu husika.

Lakini pia kutajwa kwa maeneo Kama Ethiopia, kushi, na Misri kwote kukirejelea MIZRAIM yaan ardhi ya watu weusi kumeanza Mara baada ya kizazi Cha HAMU kutapakaa ambaye anatajwa kuwa ndiye baba wa watu weusi Huku Kaka zake Yefesi na Shamu wakiwa ni baba wa WAZUNGU na waarabu.

SWALI: ni lini MWAFRIKA ALILAANIWA ?

Jibu: hapajawahi tokea MWAFRIKA au mtu mweusi na ama rangi yake ililaaniwa na MUNGU au na Mtumish yoyote wa mungu.

SWALI: unaliongeleeje swala la mwanzo 9:25 ambapo kaanani analaaniwa na kusemekana anakimbia na kwenda kuish mbali ambako ndiko husemekana Kama Africa ??

Jibu: alolaaniwa ni kaanani mjukuu wa NUHU .. mmoja Kati ya watoto watatu wa HAMU ambao kwa rangi wote walikuwa weusi.

Katika mwanzo 9:1 MUNGU aliwabariko NUHU na WANAWE wote watatu Yefesi, SHEMU na HAMU ambaye ndiye Baba wa watu weusi.

Badae katika mwanzo o:22 HAMU alifany kosa na katika kutoa adhabu baba yake akamlaani mwanawe wa kwanza wa HAMU ambae Alikuwa ni mjukuu wa NUHU.

Swali kabla hujamalizia kujibu: kwanini hakumlaani mtenda kosa akaenda kumlaani mjukuu wake ?

Kibubu: okay naona hukuelewa kitu nimesema mwanzo 9:1 MUNGU aliwabariki watoto wote wa NUHU hivyo haikuwa wezekana NUHU kumlaani baba wa watu weusi hivyo alimlaani moja ya watoto wa Baba wa watu weusi (kaanani)

Issue ya kaanani kutoroka kwenda kuish mbali ukiendelea baada ya mstari wa 9:25 utajifunza kuwa alikimbilia nchi ya Jangwa ya Mashariki ya Kati yaani Israel....

Ukisoma btn lines alipo laaniwa ALILAANIWA kuwa atakua mtumwa kwa wenzake na ndiyo ilivyo.

Watu wa kabila la kaanani waliopo middle east wamefamyika watumwa kwa wa Israel kwa Karne zote.

Mfano Ile nyika iliyosafishwa na kaanani na WANAWE wakiweka miji yao katika Israel, jordani na mpaka mji wa kaanani wenyewe unakuta ndiyo ardhi alokuja kupewa NUHU Kama nchi ya ahadi.

Hivyo kanaani baada ya kulaaniwa alikimbia kwa na kwenda nchi ya jangwa... Baba na kaka yake walipo mfata wakimtaka arudi MIZRAIM (ardhi ya watu weusi) yeye alikataa na kubakia huko nchi ya jangwa.

Baada ya mda mref utaona kizazi Cha kanaani kwa asilimia kubwa kilikuja kuuwawa katika moto wa Sonoma na Gomola. Kilijichetua Sana na maisha ya anasa Mara baada ya kutaabuka kwa mda mref .

Itaendelea hapo Chini Tena. ..

Ikiwa Kuna swali unauliza. Nipo hapa na bible ntakujibu.

min -me
the redeemer
Odense
matunduizi
Isanga family
 
SWALI : watu wanasema dini ya kikristo hajawahi kuwepo kwa mtu mweusi Sasa je .. kuonyesha uhusika wake katika maisha ya dini hii kiujumla Kuna namna yoyote katika biblia mtu mweusi ameongelewa zaidi ?

Jibu: ndiyo katika biblia mtu mweusi na mahali anakotokea amezungumzwa Mara zaidi ya 1417 hii inaonyesha uhusika wake katika dini na shughuri zingine muhim ktk maendeleo ya ulimwengu kiujumla.

Mara 740 mtu mweusi amerejelewa ama kuongelewa katika agano la kale bila kurejelea anakotokea.
Mfano : Jeremiah ndiye kawaongelea Sana Hawa Jama mara 61
Isaya Mara 40
Ezekia Mara 47
Daniel Mara 4.

SWALI: Kuna mtish yoyote katika agano la kale ambaye ni mtumishi wa mungu ?? Au wanatajwa tu Kama kutajwa ?

Jibu : wapo wengi Sana ambao ni watumishi Ila katika wale ambao ni maarufu yupo bwana Simioni ambaye katika biblia anarejelewa Kama Simioni mtitu/Nigeria (mweusi) soma ktk kitabu Cha mtitu matendo ya mitume. Lakini pia hata Musa mwenyewe alikua kaoa pisi ya kiafrika Soma Hesabu 12:0

Je Kuna mtu yoyote mweusi katika biblia anaonyesha kubarikiwa Sana ?

Jibu: nenda palepale mwanzo 1: 9 sogea Hadi 10.

Unakutana na NIMRODI ambaye ndiye mtu alikuwa na ukwasi balaa. Na ndiye mtu wa kwanza ktk biblia kutamkwa Kama mtu mkuu Sana (mighty man)

Ndiye mjenzi wa kwanza wa miji mikubwa kabla ya yote duniani. Na ndiye alienda na kuitawala Babeli Kama mfalme wa kwanza kabisa ..

Miji aliyoijenga kwa kutumia teknolojia ya Rami na tofari kabla ya wajenzi wengi e ni kama : Ereku, Ninawi, ekadi, rehobosiri, Kara, resemi na mingi ene mingi ikiwepo Babeli kabla hajaamua kuondoka kwa hiyari yake bila kuuawa Wala kupinduliwa.
 
Kuonyesha uhusika wa mtu mweusi katika ujenzi wa historia ya ukristonama historia ya biblia vifuatavyo ni vifungu vinavyo mtamka mtu mweusi na ama Afrika katika bible


KUSHI

  • Mwanzo 2:13 – Mto Gihoni unapita nchi ya Kushi.
  • Mwanzo 10:6-8 – Kushi ni mtoto wa Hamu na baba wa Nimrodi.
  • 1 Mambo ya Nyakati 1:8-10 – Kurudia ukoo wa Kushi kama katika Mwanzo.
  • 2 Wafalme 19:9 – Tirhaka mfalme wa Kushi alipigana na Ashuru.
  • 2 Mambo ya Nyakati 14:9-12 – Zera Mkushi alipigana na Asa.
  • Ayubu 28:19 – Topazi ya Kushi haiwezi kulinganishwa na hekima.
  • Zaburi 68:31 – Kushi atamnyooshea Mungu mikono yake.
  • Isaya 11:11 – Bwana atawakusanya watu wake kutoka Kushi.
  • Isaya 18:1 – Nchi ya Kushi imeelezwa kuwa ya mbali na mito.
  • Isaya 20:3-5 – Kushi itawekwa uchi na kuchukuliwa mateka.
  • Isaya 37:9 – Tirhaka, mfalme wa Kushi, anatishia Ashuru.
  • Yeremia 13:23 – Mkushi hawezi kubadili ngozi yake.
  • Yeremia 38:7 – Ebed-Meleki Mkushi anamwokoa Yeremia.
  • Ezekieli 30:4-5 – Kushi itaangamia pamoja na Misri.
  • Ezekieli 38:5 – Kushi yatajwa miongoni mwa mataifa yatakayoshambulia Israeli.
  • Nahumu 3:9 – Kushi ilikuwa nguvu ya Ninawi.
  • Sefania 3:10 – Watu wa Kushi watamletea Mungu sadaka.

MISRI

  • Mwanzo 12:10 – Abramu alikwenda Misri kwa sababu ya njaa.
  • Mwanzo 41:1-57 – Yosefu aliinuliwa kuwa mtawala wa Misri.
  • Kutoka 1:1-22 – Waisraeli waliteswa na Farao wa Misri.
  • Kutoka 14:30 – Waisraeli waliokolewa kutoka mikononi mwa Wamisri.
  • Mambo ya Walawi 18:3 – Waisraeli waonywa kutoiga matendo ya Wamisri.
  • Kumbukumbu 5:6 – Mungu aliwatoa Israeli kutoka Misri.
  • 1 Wafalme 3:1 – Sulemani alioa binti Farao wa Misri.
  • 2 Wafalme 17:4 – Israeli walitaka msaada kutoka kwa mfalme wa Misri.
  • Isaya 19:1 – Bwana anaingia Misri, miungu yao inatetemeka.
  • Yeremia 46:2 – Farao Necho wa Misri alishindwa katika vita.
  • Ezekieli 29:2 – Misri inalaumiwa kwa kiburi chake.
  • Danieli 11:42 – Misri itawekwa chini ya mfalme wa kaskazini.

SEBA

  • Mwanzo 10:7 – Seba ni mwana wa Kush.
  • 1 Mambo ya Nyakati 1:9 – Kurudia ukoo wa Seba.
  • Isaya 43:3 – Seba alitolewa kwa ajili ya Israeli.
  • Isaya 45:14 – Watu wa Seba watamwabudu Mungu wa Israeli.
  • Zaburi 72:10 – Wafalme wa Seba wataleta zawadi kwa mfalme.

PUTI

  • Mwanzo 10:6 – Puti ni mwana wa Hamu.
  • 1 Mambo ya Nyakati 1:8 – Kurudia ukoo wa Puti.
  • Yeremia 46:9 – Mashujaa wa Puti wameshindwa.
  • Ezekieli 27:10 – Puti walikuwa askari wa Tiro.
  • Ezekieli 30:5 – Puti wataangamia pamoja na Misri.
  • Ezekieli 38:5 – Puti wataungana katika vita dhidi ya Israeli.
  • Nahumu 3:9 – Puti ilikuwa nguvu ya Ninawi.

EBED-MELEKI

  • Yeremia 38:7-13 – Ebed-Meleki Mkushi anamwokoa Yeremia shimoni.
  • Yeremia 39:16-18 – Mungu anamwokoa Ebed-Meleki kwa sababu ya imani yake.

MKE WA KUSHI WA MUSA

- Hesabu 12:1 – Haruni na Miryam walimlaumu Musa kwa kumuoa mwanamke Mkushi.
 
Back
Top Bottom