Jinsi Mzalendo Magufuli alivyofanana Sana kimtazamo na Idd Amin Dada

Umechambua kiuhalisia na kiutaalam. Mimi kwa 100%, naamini kabisa, Rais Magufuli alikuwa anarandana kwa kila kitu na Idd Amin Dada wa Uganda, kuanzia kutopenda kufuata sheria, kutopenda kukosolewa, kuwachukia wenye utajiri, kuwachukia wazungu bila sababu, ulaghai wa kuwaaminisha anawapigania wanyonge, n.k.

Ukisikia mtu kila mara anataja watu wanyonge, kila mara anamtaja Mungu lakini matendo kinyume chake, anapenda kusifiwa, mwogope sana, kwa 100% mtu huyo atakuwa na siasa za hila, ana maovu mengi ambayo anataka ayafiche kwa kivuli cha wanyonge.
 
Wacha maneno ya kijifurahisha, hivi Waafrika mlilogwa na nani? MTU anayeua RAIA wake anapendwaje! Acha unafiki.
Stallin aliuwa warusi zaidi ya milioni 9, mazishi yake ndiyo yanayoongoza kwa kuhudhuriwa na watu wengi Duniani - hao walioitwa wanyonge.

Dikteta anachofanya, ni kama alivyokuwa anafanya marehemu Magufuli hapa kwetu, kuua uhuru wa vyombo vya habari, kuua uhuru wa maoni, baada ya hapo kinachofuata ni kusikia habari za kumsifia yeye tu. Wenye akili ndogo, baadaye huchotwa akili zao na hizo sifa za hila. Ndiyo maana hata hapa kwetu, ni vigumu sana kumwona mtu mwenye akili tamu kabisa, mwenye akili huru, na mkweli wa nafsi yake, akausikia utawala wa Magufuli. Wengi wanaosifia ni ama wenye elimu ndogo, wenye akili kidogo ja watu wanafiki.
 
Hauoni kuna tatizo mahali?

Kwasababu Idi Amin alikua na misimamo na mitazamo hiyo huku akiwa ameishia shule ya msingi sasa Magufuli ana PhD na yeye anashare mitazamo na misimamo hii hii?

Misimamo ya Idi ikafikia hatua akatupa walemavu Ziwani ili waliwe na mamba.

Akaua wapinzani.

Akaua wageni.

Akaua uchumi.

Akajitangaza Rais wa Maisha wa Uganda.

Au nakosea?
 
We unapenda kukosolewa?
 
"You can not run faster than a bullet" by Alhaji Dr General Iddi Amin.
"Kuna watu eti wanavamia vituo vya Polisi, na nyinyi polisi mna silaha, kwa nini msiwalaze chini? Pale Chato kuna wakati naambiwa watu walivamia kituo cha polisi, kama ningeenda pale, hata nikamwona ndugu yangu amelazwa chini, ningempandisha cheo mkuu wa kituo" - Magufuli.
 
Kwa hiyo kama wanafanana, si ni wakati sasa kama Taifa, kulichukua jambo hili kama moja ya LEGACY ya Hayati!! Yaani Hayati nae alikuwa ni Dikteta kama alivyokuwa Idd Amini Dada!

Au nitakua sijaelewa lengo hasa la hii mada?
 
Kwamba Idi Amin alikuwa mcha Mungu?
Inaelekea hujui true nature ya utawala wa Amin!
 
Dah.... Bwana William....waache walipakodi wenyewe wakwambie JPM alikuwa mtu wa namba gani...Mbona mnasumbuka Sana? Ili iweje? Inatusaidia nini Sisi wananchi wa kawaida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtasema yote lakini JPM kaacha legacy, viongozi wote wajao wa Tanzania watapimwa kwa mizani ya je angekuwa Magufuli angefanyaje, na watanzania walio wengi hawatakuja kumsahau JPM na uongozi wake shupavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…