Jinsi ndoa ya Mabeste Ilivyovunjika

We jamaa umeniwahi me mwenyewe nilitaka niweke Uzi unahusiana na ndoa ya mabeste na mkewe Lisa Leo Leo.
 
Hahaha ngoja wachaga waje '' Hili tatizo la U-marioo naona linazidi kushika kasi nchini vijana wakiume Tunapoteza ile sifa yetu stahiki inayotufanya tuitwe wanaume ... Hii ni mbaya sana aise
Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna kipindi East Africa tv walishawahi kwenda mpaka nyumbani kwake mabeste na mkewe. huyu mkewe alikuwa anaumwa kalala tu ata kuongea hawezi..

Mabeste alipambana kinoma na harambee za wadau kama East Africa TV na wengine, wakafanikiwa akapona.. hakulalamika siku zote hizo??

Swali kwanini aseme yote hayo baada ya kuachana??

Mwanamke hata umfanyie mangapi, mkiachana ataeleza mapungufu yako na vijikosa vidogo vidogo na kuvikuza...
 
Huyu Mwanamke ni Mpumbavu kufikia hatua ya kuanza kurekodi mpaka marumbano ya ndani ya ndoa ina maana kua alishapanga kumuacha jamaa.. Na kajipanga kumdhalilisha pia.
 
Naam nikweli ...Mimi nilikuwahga karibu sana na Mona gangster Ma-beste alikuwaga anakuja pale classic sound na shetta pamoja na marehemu Pancho .... So najua kiasi baadhi ya story zao zinazo husu maisha yao ... So unachokisema ni kweli Huyo binti alijitoa sana kwa ma-beste .... Ma-beste ni msanii mwenye kipaji sana '' Lakini tatizo Hana kiu ya kutafuta mafanikio
Ni changamoto, nafikiri tuna kitu kikubwa cha kujifunza.

Ila huyo mwanamke alikuwa anampenda jamaa, maana hata kukaa walikaa kwa huyo dada.

Na ukoo mzima wa Mabeste ulikuwa haumtaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi vijana wengi kusimamia familia hatuwezi sababu ya anasa na kujipenda kulikopitiliza kunakoleta ubinafsi ndiyo maana mjini unaweza kuta mbaba in his 50's amevaa rafu na sendo chini muda wote yupo busy ila ukienda home mke wake anafaidi anasukuma range na watoto wanasoma na mahitaji wanapata kwa wakati.... Ila kijana bado hajanunua kipochi cha gucci sijui raba kali mara ashinde saloon kuweka kijogoo. .its sad

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam nikweli ...Mwanamke akikosa Kazi maisha Yake yote Mwanaume atamvumilia .....ila mwanaume akikosa Kazi mwezi 1 tu basi kuna hatari kubwa kwa ndoa Yake kuvunjika

Sent using Jamii Forums mobile app
Me mama yangu kamvumilia mzee wangu alikosa kazi Mwaka 1 mzima huduma zote mama ndo alikuwa ana hudumia kuanzia kulipa ada shule, kula, nauli za Baba kwenda kutafuta kazi sehemu tofauti tofauti pamoja na kumlisha Baba n.k.Mzee baba sio wanawake wote wapo hivyo.
 

Mkuu ina maana huyu dada alimkuta Mabeste hana shughuli au? Kama alimkuta na shughuli now mambo yamekwama anamkosea sana. Naona namna mambo yakiyumba sana mwanaume akikosa kipato kuliko wanawake. Huwezi kusikia mwanaume akisema nimemuacha sababu nilikuwa namlea.

Wadada wa siku hizi pamoja na kuelimika wamekuwa tegemezi zaidi kuliko mama zetu wa zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kasikilizeni interview hiyo, acheni kufanya judgement kabla hamjasikiliza kesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…