Mabeste kaanza kufunguka baada ya mkewe kufunguka Sana Kama mkewe asingefanya ile interview sizani Kama mabeste angefunguka.
Hahaha kazi kweli aiseLivivuu!basi ataolewa[emoji3][emoji3][emoji3]alijua kapata mzungu wa kumchuna
Hajui kua ukishikwa shikamana usibweteke!
Sent using Jamii Forums mobile app
Aise ...Mapenzi bwana kweli kizungumkuti ...Awali mapenzi Yalivyo kuwa moto moto Hayo yote Hawakuwa wakiyaongeaIla Ni kweli ukae Tu uhudumiwe hujishughulishi na chochote upo tuuu unasubiri mkeo apambane hata pipi huuzi au huonyeshi jitihada zozote za kutafuta mweeeehhhh
Sio Lisa hata Mimi siwezi kuvumilia
Ntavumilia mwanaume hata akiwa anauza nyanya au mzibua vyooo mradi anapata kihalali hapo mabeste alikua amekaa anasubiri apate shoo so akili yake inamuambia kwa hadhi yake hawezi uza pipi yeye Ni staa[emoji41][emoji41][emoji41]mpuuzi huyo kaka!!!
Mwanamke hata siku 1 hawezi ona wala kukubali wanawe walale njaa atapambana mpk kieleweke
Wanaume hakuna kazi ya hadhi yako, kazi Ni kazi mradi mkono uende kinywani!
Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha yanaenda resi afadhali katoa gundu!
Binti yangu ikitokea anataka kuolewa ntampa miezi miezi 6 ya kujifikiria kama ntakua hai
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawake ni wepesi sana kusahau..Yaani hata hawa wake zetu huku nyumbani,unakuta unahidumia kila kitu kila siku lakini itokee siku hujafanya atasahau hiduma za miaka yote iliyopita..
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe una uhakika gani mabeste alikuwa atafuti hela?
Okay, mara nyingi tunaposhindwa hoja tunakuja na allegations za namna hii.
Siwezi kumtetea mwanaume aliyeolewa na mwanamke for more than 4 years.
Mkuu unaonekana huwajui vizuri wanawake.. Au labda ni mtu mwepesi sana wewe!
By the way, Lisa ndiye amesema amemuoa/amemlea jamaa kwa miaka 4 au umejazia jazia nyama? Sio kwamba amedai alihudumia familia kwa miezi 3?
Ni zaidi ya miaka 4 kamlea.
Ukisikiliza hiyo interview utamuheshimu zaidi.
Ndio kasema hivyo? Na hiyo miezi 3 imekaaje? Univumilie, interview nitaisikiliza nikishawishika na maelezo uliyoyaleta maana tayari umeshaamua kwa wakili wa Lisa.
Kupitia replies zako tu, anaonekana ni mdada mjinga mjinga tofauti na nilivyokuwa namchukulia..
Mwanamke anaweza kukuzushia lolote mkigombana..Mwana ukiisikia hiyo interview, straight utachukua upande wa Lisa.
Sijasikia hiyo issue ya miezi mitatu, sijui mwandishi kaitoa wapi.
Lisa kasema, Mabeste alihamia kwake Lisa, na kwa kipindi chote cha mahusiano yao, kama Mabeste kachangia basi ni 20%. Kilichomuuma Lisa mpaka kuibuka ni baada ya Mabeste kuanza kuzungumza kwenye media. So ikabidi na yeye aongee ili kuweka records clear.
BTW kulikuwa na tuhuma kwamba kwao Mabeste ndo walikuwa wanamchezea Lisa, hiyo anasema hata Mabeste amewahi kuwatuhumu ndugu zake.