Jinsi ndoa ya Mabeste Ilivyovunjika

Jinsi ndoa ya Mabeste Ilivyovunjika

Robidinyo

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
4,043
Reaction score
8,686
Mwanzilishi wa harakati za Piga Kambi Utalii wa Ndani, Lisa Karl Fickernscher ambaye alikuwa ni mke wa msanii wa Hip Pop hapa nchini Mabeste amefunguka kiundani kuhusu maisha yake na aliyekuwa mume wake.

Maisha ya wawili hao yalikuwa maarufu zaidi kupitia mtandao wa instagram ambapo watu wengi zaidi pasi kujua nyuma ya pazia ya maisha yao walikuwa wakifurahia familia yao na kutamani kuwa kama wao.

Ambapo Lisa kupitia Youtube chaneli ya simulizi na sauti amefunguka mazito ukweli kuhusu maisha ya mahusiano yao nje ya kile ambacho mashabiki wengi walikuwa wanakiona kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Ndoa si siri tena, juzi tumeyasikia ya Stamina kupitia sanaa yake leo Lisa amefunguka kinagaubaga sababu ambazo zimepelekea kuvunja ndoa yake na Mabeste na yapita mwaka sasa tangu wawili hao kufarakana.

Akihojiwa Lisa amehadithia sababu kuu mbili za kuachana na Mabeste ambapo ametaja kuwa Mabeste alikuwa mwanaume mwenye mkono mwepesi wa kumpiga hata mbele ya watoto wake , lakini pia ameeleza kuwa Mabeste hakuwa mwanaume wa kujitoa na mtafutaji kwaajili ya familia yake.

Pili amesema kwa asilimia 80 Mabeste alikuwa hasimamii majukumu yake kama baba wa familia na mume kwake.
”Hakuwahi kusimamia majukumu yake, sikuwahi kula hela ya muziki wake,… Kuna tofauti kubwa sana kati ya mkulima anayeenda shambani analima lakini hapati mavuno kuliko yule ambaye hafanyi kitu anashonda tu nyumbani…

Mabeste alikuwa mzito sana infika stage mnagombana nageuka kama mzazi kwake namlea kama navyolea watoto” amesema Lisa
Lisa ameongezea ”Alikuwa hataki kufanya chochote, kunipenda sio kusema unanipenda kunipenda ni matendo, sikuajiliwa, mwenzangu alirelax hakuwa na wivu mwanamke nimehudumia familia miezi miwili mitatu, alikuwa hata hajiulizi natoa wapi hakuwa na wivu”.

Aidha Mabeste na Lisa wameachana yapita mwaka sasa wakiwa na watoto wawili, Kendrick na Catelyn Mabeste.
Pia tumeona kumekuwa na mfumuko wa matukio ya aina hiyo ya ndoa za watu maarufu kufarakana jambo ambalo si jema sana kwani linatishia pakubwa sana wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa.

Tumeona Stamina na mke ndoa yao ikiwa na doa na Stamina kupitia sanaa yake ameamua kuweka wazi kisa mkasa.
Ndoa ni fumbo zito sana, ni Mungu tuu azijalie ndoa amani, upendo na ushirikiano kwani kila ndoa ina changamoto yake ni namna tu mnavyoweza kutatua changamoto hizo ili kusogeza familia.

Share this:

Chanzo Dar24
 
Labda nikuambie kitu kimoja tuu mtoa maada, mwanamke akihudumia familia mwezi mmoja tuu basi mtaa mzima watajua
Hapo kwenye maada anasema alihudumia familia miezi 2 , sasa kipindi cha maisha yao yote nani alikua analipa bills?
Ndoa zinachangamoto hiyo iko wazi lakini wanawake wengi wako hivyo...
Hata kipindi nakua mzee wangu anaweza kutuma hela kwa bi Mkubwa ili akupatie, basi akikupatia anaanza kusema mi nawasomesha kwa pesa yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila si ndo uyu demu ambae alikua anaumwaga kpnd flani hv MABESTE alikua nae bega kwa bega lamn ? Au yule alikua kamikaze maana nawafananishaga sana hawa jamaa wawili

yess BiShoo haswaaA
Ndiye demu huyo huyo ..mabeste alipambana mpaka akafanyiwa harambee na wa-bongo ili demu wake akatibiwe " na hatimae akapona

Hapa wanaume Tunajifunza kwamba pesa ndio kila kitu " hata ujitoe kwa mwanamke kiasi gani 'Kama hauna pesa Thamani yako itabaki kuwa rehani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam nikweli ...Mwanamke akikosa Kazi maisha Yake yote Mwanaume atamvumilia .....ila mwanaume akikosa Kazi mwezi 1 tu basi kuna hatari kubwa kwa ndoa Yake kuvunjika
Labda nikuambie kitu kimoja tuu mtoa maada, mwanamke akihudumia familia mwezi mmoja tuu basi mtaa mzima watajua
Hapo kwenye maada anasema alihudumia familia miezi 2 , sasa kipindi cha maisha yao yote nani alikua analipa bills?
Ndoa zinachangamoto hiyo iko wazi lakini wanawake wengi wako hivyo...
Hata kipindi nakua mzee wangu anaweza kutuma hela kwa bi Mkubwa ili akupatie, basi akikupatia anaanza kusema mi nawasomesha kwa pesa yangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amesema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya mkulima anaye kwenda shambani kisha akakosa mazao na Mtu ambaye amekaa tu amebweteka Bila ya kutafuta .... Daahh matusi makubwa sana haya

Kama huo ndio ukweli ma-beste anapaswa kujifunza
Ukisikiliza hiyo interview utamuheshimu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabeste alikuwa Marioo.

Kazi hafanyi, muziki hafanyi. Yuko Busy na media tu na neno 'Nakupeoda, Nakupenda'

Does the word Nakupenda pay bills ?

Hivi Mabeste huwa ni mchagga ?

Miaka ya karibuni vijana wa kichagga wamekuwa ma-marioo wa kutosha.

Wengine wanaolewa Ulaya wengine Bongo !

Daaah
 
Mwanzilishi wa harakati za Piga Kambi Utalii wa Ndani, Lisa Karl Fickernscher ambaye alikuwa ni mke wa msanii wa Hip Pop hapa nchini Mabeste amefunguka kiundani kuhusu maisha yake na aliyekuwa mume wake.

Maisha ya wawili hao yalikuwa maarufu zaidi kupitia mtandao wa instagram ambapo watu wengi zaidi pasi kujua nyuma ya pazia ya maisha yao walikuwa wakifurahia familia yao na kutamani kuwa kama wao.

Ambapo Lisa kupitia Youtube chaneli ya simulizi na sauti amefunguka mazito ukweli kuhusu maisha ya mahusiano yao nje ya kile ambacho mashabiki wengi walikuwa wanakiona kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Ndoa si siri tena, juzi tumeyasikia ya Stamina kupitia sanaa yake leo Lisa amefunguka kinagaubaga sababu ambazo zimepelekea kuvunja ndoa yake na Mabeste na yapita mwaka sasa tangu wawili hao kufarakana.

Akihojiwa Lisa amehadithia sababu kuu mbili za kuachana na Mabeste ambapo ametaja kuwa Mabeste alikuwa mwanaume mwenye mkono mwepesi wa kumpiga hata mbele ya watoto wake , lakini pia ameeleza kuwa Mabeste hakuwa mwanaume wa kujitoa na mtafutaji kwaajili ya familia yake.

Pili amesema kwa asilimia 80 Mabeste alikuwa hasimamii majukumu yake kama baba wa familia na mume kwake.
”Hakuwahi kusimamia majukumu yake, sikuwahi kula hela ya muziki wake,… Kuna tofauti kubwa sana kati ya mkulima anayeenda shambani analima lakini hapati mavuno kuliko yule ambaye hafanyi kitu anashonda tu nyumbani…

Mabeste alikuwa mzito sana infika stage mnagombana nageuka kama mzazi kwake namlea kama navyolea watoto” amesema Lisa
Lisa ameongezea ”Alikuwa hataki kufanya chochote, kunipenda sio kusema unanipenda kunipenda ni matendo, sikuajiliwa, mwenzangu alirelax hakuwa na wivu mwanamke nimehudumia familia miezi miwili mitatu, alikuwa hata hajiulizi natoa wapi hakuwa na wivu”.

Aidha Mabeste na Lisa wameachana yapita mwaka sasa wakiwa na watoto wawili, Kendrick na Catelyn Mabeste.
Pia tumeona kumekuwa na mfumuko wa matukio ya aina hiyo ya ndoa za watu maarufu kufarakana jambo ambalo si jema sana kwani linatishia pakubwa sana wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa.

Tumeona Stamina na mke ndoa yao ikiwa na doa na Stamina kupitia sanaa yake ameamua kuweka wazi kisa mkasa.
Ndoa ni fumbo zito sana, ni Mungu tuu azijalie ndoa amani, upendo na ushirikiano kwani kila ndoa ina changamoto yake ni namna tu mnavyoweza kutatua changamoto hizo ili kusogeza familia.

Share this:

Chanzo Dar24
 
Amesema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya mkulima anaye kwenda shambani kisha akakosa mazao na Mtu ambaye amekaa tu amebweteka Bila ya kutafuta .... Daahh matusi makubwa sana haya

Kama huo ndio ukweli ma-beste anapaswa kujifunza

Sent using Jamii Forums mobile app

Kitu kilichomuumiza ni Mabeste kuanza kuongea kwamba sababu ya wao kuachana ni pesa. Kaongea kwenye media.

Mama wa watu imebidi atoke hewani akaelezea jinsi alivyomlea jamaa toka mwanzo mpaka wanaachana, hadi mahari alijilipia.

Ugonjwa aliokuwa anaumwa inasemekana kwamba chanzo ni familia ya Mabeste, maana mara zote Mabeste alikuwa akiwatuhumu nyumbani kwao na haelewani na wazazi wake kabla hata hajakutana na Lisa.

Idea ya kukusanya michango kwa ajili ya matibabu ni ya Lisa, na hata kuendesha accounts za Mabeste yeye ndiye alikuwa anafanya hivyo, ile concert yeye ndiye aliyeplan na kuanza kufatilia kila kitu.

Ukiweza kupata muda wa kumsikia utaelewa, na bahati mbaya kwa Mabeste, Lisa alifikia sehemu akaanza kurekodi kila walichokuwa wanazozana au kujadili.
 
Back
Top Bottom