Jinsi nilivyoanza kuwa mtu wa mazoezi ya mwili/ push ups mpaka kuwa na sexy body

Jinsi nilivyoanza kuwa mtu wa mazoezi ya mwili/ push ups mpaka kuwa na sexy body

Mimi huyo,japo najitahidi kupiga push up 100 kwa siku lakini na zenyewe nategea leo napiga kesho sipigi.
Screenshot_2024-12-06-17-21-15-621_com.facebook.katana-edit.jpg
 
Kwenye 80 had 120 hapo za kunyanyuq mwili umedanganya labda kama ni kwa siku sio kwa mkupuo wa mara moja
Hizo unaunga unga mkuu push mia kwa mara moja siyo mchezo though wapo wanaokupigia 50 kwa mkupuo.

Mimi nagonga 30 nashuka na 20 15 mara mbili namalizia na makumi mawili kisha taulo begani kwenda kujimwagia.
 
Nakumbuka nilianza kwa kuning'nia juu ya paa la nyumba kisha kupush mwili wangu ups&down, then push ups 80 hadi 120 kila siku.

Nikawa nachelewa kuamka sababu mazoezi sikuyazoea hivyo nilikuwa nasikia uchovu sana na mgongo pamoja na mbavu ziliniuma sana.

Ilipo timia miezi 3 tangu kuanza mazoezi nikaanza kuona kifua changu pamoja na shoulders vikitanuka sana-hamu ya kula ikawa ikiongezeka kwa kasi, ngozi ikaanza kunawili.

Baada ya kupata matokeo chanya nilipata hamasa ya kuendelea na mazoezi, nimekuwa na kifua ambacho kila mdada anavutiwa nacho.

Aisee ukiona mtu amekata mwili muheshimu sana mazoezi yanahitaji consistency na moyo sana yaani ni kama unavyo struggle kutafuta utajiri, noma sana.
Safi sana
 
Kwa wiki piga mazoezi siku 3 tu inatosha kubadilika kabisa.
Najitahidi mkuu,kusema ukweli mazoezi yangu mimi ni kukimbia lakini nina miezi minne nimepumzika misuli ya miguu inaninyima fursa hiyo.

Kupiga push up mzee uwe na moyo siyo jambo la masihara.
 
Back
Top Bottom