Jinsi nilivyofilisika na kupoteza Tsh Milioni 25 kupitia kamari ya Aviator

Mfilisi

Member
Joined
May 31, 2026
Posts
40
Reaction score
98
Siku zote jambo usilolijua ni usiku wa Giza, sikuwahi amini Wala sikuwahi kuelewa kitu kinaitwa URAIBU , ila sasa nimejua kwa vitendo Nini maana ya URAIBU

Nilikua nikisikia neno KAMARI , lakini sikujua kama Kuna siku nitakua MRAIBU WA kamari. Nimeshuhudia kwenye maisha yangu kwa vitendo , maana ya URAIBU WA kamari.

Ni Bora URAIBU WA pombe na sigara pengine unatibika na mtu anaweza acha bila hata kufilisika, kuliko URAIBU WA kamari. URAIBU WA kamari ni ZAIDI ya unavyochukuliwa na watu wengi, URAIBU WA kamari unafilisi na pengine hata kuua.

Sio tu nimeshuhudia URAIBU WA kamari bali nimeambulia mateso ya kamari ,kufilisika na KILA aina ya maumivu ambayo sikuyatarajia kama yatakuja kunipata

Kamari ni kamari ila kamari ya AVIATOR ni janga kubwa sana kwa sasa. Ni janga ambalo limeivamia Tanzania , japo Afrika Mashariki kwa nchi kama Kenya , taarifa zinaonesha kuna waraibu wengi wakubwa ZAIDI wa kamari ya Aviator, ila kwa sasa nafikiri Tanzania imekuja juu kwa Afrika Mashariki.

Japo Sina takwimu Rasmi, hii ni kutokana na visa ambavyo vimeanza kujitokeza, na taarifa mbalimbali za magazeti na vyombo vingine vya habari, zinavyoelezea janga la kamari nchini Tanzania

Mimi kijana ambaye nimezaliwa SUMBAWANGA - Rukwa , TANZANIA, Katika familia ya hali ya maisha ya kawaida , maisha ya kuamka kwenda shambani, kulisha mifugo, kwenda shule na kurudi kuendelea na shughuli zingine za nyumbani.

Kwa kifupi ni maisha ambayo wazazi walikua ni wakulima na wafugaji wadogo. Hawakua na UWEZO mkubwa sana kimaisha, bali UWEZO tu wa kumudu chakula na mahitaji muhimu madogo madogo ya nyumbani

Nimesoma shule za SERIKALI kuanzia, shule ya msingi iliyopo SUMBAWANGA ,shule ya sekondari iliyopo SUMBAWANGA pia, na kidato Cha Tano na sita, shule iliyopo TABORA. Nimehitimu CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SIKOINE (SUA) , kilichopo MOROGORO mwaka 2014.

Bahati isiyo nzuri sikubahatika kupata kazi ya fani niliyosomea, nikaomba kazi ya ualimu nikapata kufundisha shule binafsi kwa masomo ya sayansi, CHEMISTRY na BIOLOGY.

Nilianza kazi shule hiyo X, iliyopo Morogoro tangu mwaka 2015 hadi 2018. KATIKA kipindi chote hicho namshukuru Mwenyezi Mungu maisha yalibadilika kiasi fulani, mpaka nikafikia hatua ya kuoa mwaka 2016.

Sikua na mshahara mkubwa sana ila nilikua na nidhamu ya pesa , nilikua nalipwa Tsh 408,000 /= kwa mwezi.

Pesa hiyo nilifanikiwa kununua kiwanja ,shamba , pamoja kutoa mahitaji ya nyumbani na mahitaji mengine madogo madogo ya muhimu.

Pia Kupitia pesa hiyo niliweza pia, kuwahudumia wazazi kwa kiasi fulani, kusaidia ndugu na jamaa kwa kiasi hicho hicho kidogo nilichojaaliwa. Kwa kipindi kile kwangu nilikiona ni kiasi kikubwa Cha pesa, kwa sababu nilikua na nidhamu ya pesa.

Nilijikita sana kufanya ibada ,kwani mimi ni muislamu, ikiwemo swala Tano na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu dini, na pia kutumia muda Mwingine kukaa na familia yangu.

Mwaka 2019 mwanzoni ,nilipata shule kazi shule ngingine Y binafsi pia iliyopo mkoani IRINGA.

Kwa kweli namshukuru Mungu, shule hii nilibahatika kulipwa mshahara mara ya mbili na kiasi ya mshahara niliokua nikilipwa na shule X ya MOROGORO.

Mimi na mke wangu tulifurahi sana, kwani miezi michache tulilinunua kiwanja kingine lakini sio IRINGA ni Mkoa mwingine tu sehemu ilipo familia yangu mpaka sasa.

2019 Hadi 2021 mimi na mke wangu tulifanikiwa kujenga nyumba katika hicho kiwanja kipya, ingawa nyumba ilikua bado kumalizika hasa finishing kwa ndani ,pamoja na umeme. Lakini kwa maisha yetu sisi watu wa hali ya chini, ilikua unaweza kuhamia tu kwenye nyumba hiyo. Japo sikufanya hivyo.

Mpaka hapo tulikua tayari tuna nyumba MKOA Y, kiwanja na shamba MOROGORO. Pia tulikua na mpango mwingine wa kununua gari ya kutembelea na kukuza biashara ndogo ndogo tulizokua nazo wakati huo.

Kiufupi akaunti yangu kwa kipindi hicho ilikua haikosi akiba ya Tsh. milioni 2 Hadi 5. Ambapo kwa mwezi nilikua naweza weka akiba ya laki Tano (500,000) au zaidi. Uzuri mwingine sikua na madeni, wala jambo ambalo lingeshughulisha akili au kutumia pesa nyingi.

Mke wangu pia alikua amejiariwa, ajira za mwaka 2017, hivyo pia alikua na mshahara wake.

Kupitia mshahara wake aliweza kuchangia kuongezea kwenye akiba.

Wote wawili kwa mwezi tulikua tunaweza weka akiba ya Tsh 800 ,000/=. Yaani Mimi naweka Tsh 500,000 na mke wangu anaweka Tsh 300,000.

Kwa kuwa tulikua na mpango mwingine wa kununua gari na kukuza biashara, hasa gari ni jambo ambalo binafsi nilikua Nina hamu nalo sana.

Kiukweli ilikua inawezekana, kwani malengo yalikua ni kuweka akiba ya Tsh 800,000 kwa mwezi, kwa miaka miwili, yaani miezi 24. Ambapo 24 X 800,000 = 19,200,000/=

Tulifanikiwa kwa asilimia 60% japo, mwaka 2021 mwishoni, wife alienda chuo kikuu kujiendeleza kimasomo.

Ni mwaka 2022 ambapo, mambo yalianza kubadilika, kwani taasisi ninayofanyia kazi ILIANZA kuyumba kulipa mishahara kwa wakati, pia na mke wangu alikua ameanza KUSOMA , hivyo tukawa na jukumu lingine la kulipa ada chuoni, pamoja na kumlipia mtoto ada.

Kazini tukaanza kusubiri hadi miezi mitatu ndio tunalipwa mishahara. Wafanyakazi wengi wakaanza kukopa kukopa hovyo mtaani, kwenye microfinance na mikopo ya nyonya damu.

Wengine wakaanza kubet ,wengine kuingia kwenye kalinda, Q net na michezo mingine ya mtandaoni na wengi waliishia kutapeliwa na kupoteza pesa.

Ilimradi KILA Mmoja alianza kuangalia njia mbadala ya kutafuta pesa.

Binafsi sikuwahi kujiingiza kwenye michezo ya Kalynda, Q net Wala kamari kwa wakati huo. Kwani nilihofia kufanya hivyo ni kucheza kamari na ni haramu na ni dhambi kwa Imani yangu ya kiislamu.

Hivyo niliwashangaa sana watu walivyokua wakilalamika kutapeliwa pesa zao, kiujumla niliwaona ni wazembe na wenye tamaa ya pesa, ndio maana wanapoteza pesa.

Usilolijua ni usiku wa Giza, sikutegemea kama ipo siku Mimi ndio nitakua mraibu wa kamari wa kutupwa, sikutegemea wale niliokua nawaona wazembe, wao ndio watakuja kunishangaa Mimi na kunishauri kuacha kamari, yaani kama ni UGONJWA basi Mimi niliugua kuwazidi, kama ni URAIBU basi Mimi nilikua mraibu mara 1000 Yao.

Ilikua tayari Mwaka 2023 ndio mwaka sitousahau, ndio mwaka maisha yangu yalipoanza kuharibika.

Ndio mwaka niliposikia na kujifunza neno AVIATOR. Kwani tayari Kuna wafanyakazi walikua wameanza kucheza huo MCHEZO. Ukilinganisha mishahara ilikua imeanza kucheleweshwa tangu 2022. Japo tatizo la mishahara lilianza 2020 ila lilitatuliwa kdg Hadi 2021. Na 2022 likapamba moto ZAIDI.

Septemba 2023 ni mwezi ambao sitousahau , ni mwezi ambao nilifundishwa hiyo aviator. Kumbuka hapo awali nimesema nilikua sijawahi kubet Wala KUSHIRIKI MCHEZO wowote wa kamari, na nilikua nimejikita sana kwenye ibada.

Septemba 2023 nadhani ndio mwezi shetani alikuja na ukoo wake wote kuhakikisha najifunza na kucheza AVIATOR.

Siku moja nipo kazini, Kuna mfanyakazi MMOJA akamwambia mfanyakazi mwenzetu mwingine
"Aisee hivi umemuelekeza huyu ( yaani Mimi) kuhusu Aviator?"

Yule dada akajibu aah hapana. Mi kipindi hicho sielewi chochote na Wala sikua mtu wa kubet Wala sikuwahi kujiunga kwenye michezo yeyote inayohusu pesa au kamari.

Nilikua nikisikia watu wametapeliwa kwenye Kalinda, Q net, Desi n.k nawaona kama wajinga hivi. Sikuwahi kuruhusu akili yangu Kupenda pesa za haraka, na uzuri nilikua mtu wa ibada sana yaani swala Tano. Kwa hivyo ile Aya ya kukataza kamari katika surat Maida ,Aya ya 90 ilikua sana kichwani kwangu na nilikua nina hofu sana na makatazo ya Mwenyezi Mungu.

Basi yule jamaa alipomuuliza yule dada, kama amenifundisha? siku Ile sikujali sana, nikaona wananipotezea muda nikaachana nao.

siku iliyofuata akili ikanijia hebu ulizia hiyo aviator ni nini? Hapa sasa shetani alikua Jirani na ukoo mzima kuhakikisha najifunza AVIATOR.

Basi kwa shauku nikauliza, hiyo AVIATOR ndio Nini? Ili swali ndilo kosa langu kubwa kuwahi kutokea.

Akaja yule dada kunionesha, nikaona anaweka pesa halafu anaacha izunguke mf. Ukiweka 1,000 ikizunguka mara 2 UNAPATA 2,000/=

Nikasema kumbe ndio rahisi hivi, basi wakanielekeza pale pale namna ya kujisajili

Nikafungua akaunti sportpesa .
Baada ya kufungua akaunti sportpesa kwa msaada wa watumishi wenzangu walionitangulia kucheza Aviator, nikaweka Tsh 70,000/= nikaanza kama BURUDANI, ikanipa Tsh 150,000 sikutoa.

Hapo ilikua Septemba 2023. Basi jioni ake nikaenda kumuonesha mke wangu, kwamba Kuna MCHEZO wa ajabu ukicheza unakupa pesa nyingi sana, nikaanza kucheza mbele yake, Ile pesa nakumbuka ikapanda Tena kutoka 150,000 mpaka 370,000

Hapo sasa nikaona sasa huu MCHEZO unapesa, nikasahau GHAFLA kwamba ni kamari na ni haramu

Akili ikabadilika kutoka kucheza kama burudani, nikaanza kucheza kama kazi, na kufanya mtaji ile Tsh 370,000,

Kumbuka sikuitoa Ile pesa, basi ikaliwa yote.

Kwa kua akili ilishaniamisha Kuna hela , nikaanza kuweka hela kubwa kubwa mara Tsh 100,000,
Wakati Mwingine Tsh 200,000

Ikawa wakati Mwingine napata, na wakati Mwingine naliwa pesa yote. Ikafika hatua kiasi ambacho naliwa kikaanza kuwa kikubwa kuliko kiasi ninachokula

Nikaanza kufunguka akaunti hovyo hovyo, kila kampuni ya betting , mara wasafibet, betway, betika, betpawa, mbet , lionbet, n.k

Ilimradi nikiona kampuni na Tangazo la betting, nafungua naweka pesa nacheza aviator, ikiliwa nahamia kampuni nyingine.

Nikazunguka kampuni zote mpaka nikarudi Tena sportpesa.
Mpaka hapo nikawa nimeishapoteza pesa nyingi ila akili na MAWAZO yangu ,yananiaminisha na kuniambia hizo pesa utaradisha tu.

kufikia DISEMBA 2023 nikapiga hesabu tayari nikawa nina hasara ya Tsh Milioni 3.7.
Hapo sasa nikaanza kuwa na msongo wa MAWAZO , nikaandika makala ya kusimulia kiasi nilichopoteza na kujisemea sitocheza Tena HUU MCHEZO.

Lakini ilikua sio kweli, NAFSI ilitaka kuacha, ila shetani alikua bado ananihitaji niendelee KUPOTEZA pesa.

Mwaka 2024, mwezi Januari, nikiwa kazini, nilipewa jukumu la kukusanya pesa Fulani.
Basi baadhi ya wazazi wakawa wanatuma pesa KUPITIA Mpesa yangu.

Pesa zingine wanaleta mkononi, yaani pesa Taslim. Nakumbuka nilitumiwa Tsh 800,000 KUPITIA Mpesa.

Tsh 800,000 zote nilicheza Aviator ndani ya muda mfupi, nikawa nimepoteza na kuongeza deni lingine. Tena deni la ofisi kazini. Nikajieleza UONGO nikazilipa taratibu.

Hali yangu kiuchumi na kiafya ikaanza kuwa mbaya, wakati huo mshahara tayari unachelewa kutoka, pia madeni yakazidi kuongeza na kuwa mengi.

Sasa nikaanza kukopa pesa hovyo mtaani , Tena kwa riba, nakopa Tsh 300,000 Tena kwa riba ya 30% nachezea yote aviator. Nakopa Tsh 700,000 nacheza karibu 600,000 kwenye aviator.

Nikaanza kuazima pesa za ndugu hovyo hovyo, Leo naazima kwa huyu, kesho kwa huyu, ikawa sasa kila pesa ninayopata napeleka kwenye aviator.

Kufikia mwishoni mwa 2024 nikapiga hesabu ya hasara, sasa ikawa imeongezeka kutoka Tsh Milioni 3.7 hadi Tsh Milioni 18.

Hapo sasa tayari nikawa nimechanganyikiwa, nikadhohofika kiafya kwa sababu nilikua siwezi kula vizuri, afya ya kiakili kwa sababu ya msongo wa mawzo, kimwili nikawa nimepungua sana, na hata kijamii nikawa siaminiki tena. Na pia nikawa sina hela Tena ya kwenda gym.

Nikawa sasa hata hela ya kula ni changamoto, hela ya Kodi ya nyumba changamoto, hela ya kumlipia ada mtoto changamoto. Nikaapa mara ya pili kwamba nimeacha kamari.

Nikauza simu mara ya kwanza nikakaa miezi miwili bila kucheza aviator, nikanunua nyingine BAADA ya miezi miwili.

Siku nimenunua tu simu nyingine, nikasema nijaribu tena kucheza aviator, nikajikuta nimecheza tena, nikaliwa pesa zingine karibu Tsh 400,000

Nikauza tena ile simu, nikajikuta sasa madeni ni mengi sana na Hali ni ya maisha ni ngumu sana. Mshahara hautoki kwa wakati , mke wangu haniamini Tena.

Mwishoni mwa mwaka 2024 nikanunua tena simu. Kuna siku wenzangu walinipa nishike Tsh 300,000 ya Rambirambi kwa ajili
ya kwenda kumuona mwenzetu alifiwa na baba yake.

Ile pesa nilicheza kamari ya Aviator nikaliwa yote. Walipofika ili twemde kumuona mwenzetu, nilikuwa tayari sina ile hela, ikabidi niende kukopa microfinance ,uzuri nikapata mkopo WA Tsh 320,000 Tena kwa riba. Nikawapa Tsh 300,000 nikabaki na Tsh 20,000

Madeni yakazidi kuongezeka, nikaenda Tena sehemu nikakopa Tsh 300,000, nikacheza aviator Tsh 200,000 ili nirudishe Ile hasara ya Tsh 300,000 ya rambirambi ikaliwa yote. Ikabaki Tsh 100,000 tu

Kuna siku tulilipwa mishahara ya miezi miwili, nilikua Nina Simbaking, kwenye akaunti ilikua imebaki Tsh 1,100,000.

Basi nikawa nachukua zile pesa kupitia mobile banking / simbanking nacheza aviator, kidogo kidogo inaliwa, mpaka ikaliwA milioni Moja yote. Ikabaki Tsh 100,000 tu

Mwaka 2025 mwanzoni nikapiga hesabu ya hasara tayari, ikawa ni Tsh Milioni 21. Nikawa nimezidi kuchanganyikiwa ZAIDI na kudhohofika kiafya, kimwili, kiakili. Hata nikawa sijipendi Tena. Navaa hovyo hovyo, sipendezi kama zamani.

Nikaomba ndugu wanichangie ,niliwadanganya mambo mengi kwamba nina madeni mengi Kuna hela niliibiwa, wakanichangia karibu Tsh 400,000,

Kiukweli nilienda Tena kucheza tena Tsh 250,000 ikaliwa yote, nikaambuliwa Tsh 150,000

Ikafika hatua nikamuita Shekh anisomee Dua , ila sikumwambia nacheza kamari, nilimwambia mambo yangu tu hayaendi

akasoma lakini bado sikuacha
Kazini kwangu, Mkuu wangu akaniita na kunihoji, akasema naomba tuongee kama kaka na dada, maana yeye ni wa kike.

Hapo ilikua tayari ni 2025 Juni, akaniuliza Mr. Mbona umepungua sana, ikabidi nimueleze mkasa mzima sikumficha , akasema nitamuita Mchungaji, Kama utaridhia akuombee, japo najua wewe ni Imani tofauti. Yaani Mimi ni muislamu ,yeye ni mkristo. Nikamwambia sawa tu.

Akaja yule Mchungaji akaniombea.
Baada ya hapo ,Mkuu wangu akaniuliza ulitaka nikusaidie vipi, nikamwambia kwa sasa Nina madeni mengi sana, ila Nina madeni ya haraka sana ,ambayo kama nitapata Tsh 1,200,000/=utakua umenisaidia sana.
Kisha nitakua nalipa taratibu. Akapambana akaja kunipa Tsh 600,000 ,akasema ndio aliyopata

Basi Ile laki sita , siku Ile Ile nikacheza aviator nikawa nimeliwa Tsh 200,000. Tsh 400,000 tu ndio nililipa madeni,

Kulikua Kuna pesa nyingine, nazikusanya na kutunza za kazini za mfuko wa wafanyakazi.
Tayari na zenyewe nikawa nimepoteza Tsh 1,383,000 kwenye kamari ya aviator.

Pia Kuna pesa ya ada ya mtoto tulichanga na mke wangu Tsh 700,000 nayo nikacheza na KUPOTEZA kwenye kamari ya Aviator.

Pia Kuna Tsh 1,500,000 rafiki yangu alinikopesha , nikaanza biashara ya kuuza mchele, lakini Ile pesa ilipotea yote kwenye kamari ya Aviator na biashara ikafa.

Zipo pesa nilikua nakopa kwa mke wangu nazo nacheza kamari ya Aviator. Zingine sikumbuki, zipo pesa ndogo Tsh 10,000 Tsh 20,000 Tsh 30,000 n.k hizo ni nyingi sana

Ushindi mkubwa niliowahi kupata ni Tsh 1,200,000 tu , nayo niliweka Tsh 300,000
Kwa hiyo FAIDA ilikua Tsh 900,000
Lakini pesa yote niliirudisha kwa kucheza tena aviator.

Sasa hali yangu ikazidi kuwa mbaya ZAIDI,
Mpaka mwishoni mwa mwaka 2025 nikawa Nina hasara Tsh 22 Milioni

Kufikia mwaka HUU wa 2026 , nikawa nimeuza 90% ya vitu vya ndani na kucheza kamari ya aviator. Nikawa nimepoteza ZAIDI ya Tsh 3,000,000 kutoka kwenye vitu nilivyouza.

Niliuza Tv , Simu, kabati, kitanda, meza ,meza ya Tv, mtungi wa gesi, Kompyuta na Radio.

Mpaka hapo nikawa sasa nina hasara Ya Tsh Milioni 25. Yapo matukio mengi sana ya JINSI nilivyopoteza pesa , mengine nimeyasahau na mengine sijayaeleza tu.

Yapo MADHARA mengi sana niliyapata ya kifamilia, kijamii, kiafya, kiakili na kiuchumi.

Kwa sasa , namshukuru Mungu akili imenirudi, niliweka wazi tatizo langu kwa ndugu, jamaa na marafiki nikapata ushauri mzuri sana na dua zao

Pia nimekubali kwamba hakuna faida katika kamari, na tatu nimeweka mpango wa kulipa madeni yangu taratibu na kidogo kidogo , wanaonidai nimeongea nao na kuwaeleza JINSI nitakavyolipa kidogo kidogo madeni yangu.

Pia nimeweka mpango wa kuweka akiba kidogo kidogo ,na nimeanza KUFIKIRIA kujiajiri na sio kucheza Aviator

Nimesimulia hii stori yangu ya kweli kabisa , iliyonikuta Mimi mwenyewe. Tafadhali ndugu zangu
Kama hujawahi kucheza kamari yeyote Ile na ZAIDI hii ya Aviator USITHUBUTU

Na kama umecheza umepoteza pesa nyingi, kubali tu kuwa umepoteza usilazamishe kurudisha utapoteza ZAIDI. Kumbuka pesa inatafutwa na kurudi, ila ukifa haurudi Tena.
 
Pole sana
Kamari ni janga la taifa
 
Pole kwa yote mkuu na pia nikupongeze sana kwa kushirikisha watu wako wa karibu, huu uraibu unaua watu wengi kimya kimya.. Lakin hatua ya kushirikisha ilikuwa uponyaji mkubwa sana kwako. Mungu akufanikishe kwa safari mpya ya maisha. uhai ndo kila kitu. mali zinarudi lakini uhai tumepewa mara moja
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako na dua yako
 
Back
Top Bottom