Jinsi nilivyofilisika na kupoteza Tsh Milioni 25 kupitia kamari ya Aviator

Ahsante
Pia hongera kwa kujilinda na kamari, wengine tumejutia BAADA ya kupoteza
 
Pole sanamkuu mi naomba nikupongeze kwa hatua kubwa ya kuweza kiacha hii michezo ni rahisi sana kuingia ila kutoka ndio huwa mtihani mkubwa sababu wengi huamini atazirudisha
 
Bora umemwambia ndugu. Anadhani Mimi nadanganya...
 
Pole ndugu , karibu tunaweza onana ukiwa tayari takupa mawasiliano ,nipo Iringa. Nakuombea na wewe uache
 
Mimi ni shuhuda
Kama three days zilzopita nmepoteza more than 5m kwenye aviator.....nkaapa stocheza tena ila muda syo mrefu nmetoka kuliwa 2m.....npo tuu nalewa npoteze haya mawazo.....
Pole sana mkuu Dawa ha
Mimi ni shuhuda
Kama three days zilzopita nmepoteza more than 5m kwenye aviator.....nkaapa stocheza tena ila muda syo mrefu nmetoka kuliwa 2m.....npo tuu nalewa npoteze haya mawazo.....
Pole sana mkuu Dawa hapi ni kukubali kwamba umeshapoteza na haziwezi kurudi tena samehe kabisa na isahau usitake kupambana zirudi kadri utakavyojaribu kucheza ili urudishe ndivyo unavyozidi kuliwa na mwishowe kuwa mraibu kabisa
 
Ahsante sana, pia na wewe pole na huyo mtoto wa dada Yako. Kwa hatua aliyofikia anahitaji Tiba ya kisaikolojia na Tiba ya UGONJWA WA akili.
 
kuna mwenzako analala nje kwenye makochi ya bar saa 11 kasoro asubui anaonekana na watu wakienda kanisani kaketi juu ya gogo akichezea simu
 
Kuhusu kiwango ulichopoteza umedanganya. Siyo kweli huna hesabu za kupiga hapo kuonesha umepoteza hata Mil 10.
 
Bora betting kuliko aviator
Japo all in all kamari zote ni msala.
Pole sana mkuu na hongera kwa maamuzi
 
Kuna kitu kinaitwa sunk cost fallacy, lile wazo la kurudisha ulichopoteza ndo kinatugharimu wengi.

Aviator huwa nacheza buku tu mia mia kujifurahisha.
 
Kuhusu kiwango ulichopoteza umedanganya. Siyo kweli huna hesabu za kupiga hapo kuonesha umepoteza hata Mil 10.
Soma VIZURI hiyo makala, sijaandika pesa zote Tsh Milioni 25 kwa hesabu unayotaka wewe ,

Hapo nimekupa tu baadhi ya matukio makubwa niliyopoteza pesa nyingi kwa wakati MMOJA.
Zipo pesa nilikua napoteza kwa siku Tsh 50,000 n.k hizo hata sijaandika

Ndio maana nimesema zingine mpaka nimesahau

Hiyo Tsh Milioni 25 nimejumlisha kupitia transaction history ya sportpesa tu..

Bado betting companies zingine hata sijazungumza. Na ukumbukue nilikua natunza records kila mwaka tangu 2023 Hadi 2026
 
Inavyoonesha uraibu wa kindege unawakumba matajiri na masikini.
Ukiwa unaangalia live watu wanavyoweka pesa unakuta mtu anaweka mpaka 300,000 na mnaliwa wote kwa sekunde shwaaaa kabla hakijapaa unakuta 1.02.
 
Kweli ni changamoto
 
Pole sana! Kamari zote kuanzia vindege/aviator, betting n.k ni janga sana !

Serikali inapewa kodi na haya makampuni wao wanakausha ! Hakuna pesa rahisi !
Serikali haihusiki na wewe kucheza kamari, unayehusika ni wewe mchezaji. Kupata huigawii serikali, ukikosa ndo unasema eti serikali IPO. Anayekutuma kucheza siyo serikali ni uamuzi wako kama vile kuhonga malaya tuu.
 
Hivi huwa mnafikiria nini mpaka kusema hivi ? Mnajua maana ya addiction nyie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…