Jinsi nilivyofilisika na kupoteza Tsh Milioni 25 kupitia kamari ya Aviator

Serikali na wadau wote lawama hizi zinawahusu Moja kwa moja.

Kuna siku nilikua 8.5M NBC iliisha kuazia saa 9 usiku mpaka saa moja asubuhi.

Naamini kungekua na deposit limit kwenye haya makampuni ya kubet au makampuni ya simu nisinge poteza hii pesa.

Kampuni linaona na deposit milioni ya kwanza mpaka milioni ya nane kwanini wasiweke limit kwamba bwana kudepost mwisho 500k ndani ya masaa 24?

All in all addiction ya aviator ni mbaya sana,kama sio wewe ndugu yako wa karibu yupo addicted na huu uchawi ni vile tu hujajua.

Bado naishi🙏
 
Bro UMESABABISHA NIMECHEKA USIKU HUU WA MANANE IJAPOKUWA HAICHEKESHI

ANYWAY URAIBU MBAYA SANA TUOMBE MUNGU TU TUSIINGIE HUKO
 
Fuatilia mafunzo ya Complete deliverance part 1 - 3 Mtandao wa YouTube, mfundishaji ni Apostle Joshua Selman

Uwe huru milele katika jina la Yesu!
 
Dah pole sana mkuu
 
Wewe upo kama mimi kabisa, acha tuu, sema kuna watu naona wanabahati nayo sana betting ya mpiga, najiulizaga sana matukio yao sijui ni kweli.
 
Kinachoponza ni ile kutaka kurudisha ulichopoteza, kuna kipindi nilijaribu kucheza Derive options, japo ilinipa hela ndan ya siku chache ila niliapa sitorudia, maana unaweza kujikuta unakufa kwa pressure!
 
Wewe ni motivation speaker umekuja kupiga promo tu watu waichukie aviator

Aliyepigwa m.25 hawezi kuwa na maelezo marefu kiasi hicho.

Wazee wa aviator weka likes za kutosha hapa
 
Pole sana mkuu. Kama kweli hiki kisa ni cha kweli, basi kiwe fundisho kwa yeyote anayefikiria kucheza kamari.
 
Betting ni mbaya
 
Bora hata ingekua mpira hivi mtu mwenye akili timamu unachezaje KINDEGE??????
 
Mimi nimeshaandika sana kuhusu hili jambo humu ndani,limemaliza vijana hata Mimi limeniumiza sana.

Mnaosema ni ujinga wetu hamjui maana ya addiction na kiufupi mna low IQ sana.
Tuendelee kupaza sauti ndugu. Wengi hawajui addiction ni nini
 
Wewe ni motivation speaker umekuja kupiga promo tu watu waichukie aviator

Aliyepigwa m.25 hawezi kuwa na maelezo marefu kiasi hicho.

Wazee wa aviator weka likes za kutosha hapa
Sawa nawajua watu wa makampuni ya kamari mpo kutetea kampuni zenu. Ila nilichoandika ni ukweli, na nipo kuwapigania watu wengine wasiendelee KUPOTEZA pesa zao.
Kama napiga promo ya watu kuchukia aviator, unadhani nafaidika nini na hiyo promo?

Na wewe unayetaka watu waipende aviator unafaidika na Nini?

Kama una kampuni ya kamari sawa, endelea kutetea lakini ukweli ndio huo.
 
Pole sana . Bora wengine mnaojitokeza wengi walihisi Mimi nadanganya.
Tupaze sauti zetu, SERIKALI ifungie HUU MCHEZO wa aviator.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…