Kwani wewe umeelewa nini?Ndo umekaa ukawaza hicho tu
Tabia za wachawi wa mombasani wazijua weye ama unadhani Mombasa ni maarufu kwa ubasha tuh?
Think outside the box, don't go for the obvious.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani wewe umeelewa nini?Ndo umekaa ukawaza hicho tu
Hasidi hana sababu mkuu, unajua mchawi kitu kidogo anakifanya kionekane kikubwa
Walikuwa wanawake mkuuHaukukuta ute ute kwenye makalio
Pole sana Cc ephen_Shalom wapendwa,
Leo nimekumbuka kisa hiki, kilichonitokea mwenyewe nikiwa katika harakati Mkoa wa Njombe. Narudia tena hii sio stori ya kufikirika imenitokea mwenyewe.
Uchawi hauna faida yoyote ni ujinga uliokomaa, ni utumwa. Walio wachawi wanamani kutoka ila there is no way out there. Ninamiliki maduka ya dawa za binadamu yaliyopo maeneo ya vijijini huko, kazi yangu hua ni kuzunguka na kutafuta watu wa kuuza tu na kufunga mahesabu mwisho wa mwezi.
Siku Moja kuna dada wa ADDO aliyekuwa akiuza moja kati ya maduka alipata dharura na kwakua nilikuwa na nafasi nilimruhusu aende nami nikaenda kumpokea kuuza dawa Ili clients wasikose huduma mpaka atakaporejea. Sasa hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
Hiyo siku nimeamka vizuri kabisa nikashinda vema jioni imefika nikafunga hesabu na kulikua na pesa kwenye draw nilizibeba na kwenda nazo nyumbani kwa sababu za kiusalama, nikaacha kiasi kadhaa pia kwenye draw. Baada ya kufikia nyumbani nikaweka pesa vizuri nikawasha data niperuzi kidogo Kisha nikalala.
Naamka asubuhi nimelala nje[emoji23][emoji23][emoji23] kwenye shimo Moja lilikua jirani na nyumba. Kitu kilichonishangaza nililala na boksa nikaamka nje nikiwa na nguo zangu nilizovaa jana[emoji32]
Kitendo cha kutaka kurudi ndani nakuta mlango umefungwa kwa ndani, nikawa najiuliza nilitokea wapi? Nikajaribu kupush mlango ukafunguka kuingia ndani nakuta panya sita kitandani wametulia wananiangalia tu[emoji23][emoji23][emoji23] nikarusha kiatu wakapanda darini na kupotea ghafla kukawa kimya.
Impact za tukio lile, pesa nilizorudi nazo jana hakukua na hata kumi iliyokuepo[emoji51] (zilipotea)
Sikuweza kukaa tena kule, nikafunga duka mpaka yule dada aliporudi kusongesa gurudumu. Kwa Sasa nikienda huwa silali kabisa hata iwe late kiasi gani nitarudi mjini.
Kama hujapita Njombe hujaona uchawi bado.