Jinsi nilivyotapeliwa na mtu niliyedhani ni mhitaji kumbe ni tapeli

Hupaswi kuwachukia bali unapaswa kuwaombea......kimsingi ni kwamba wamekwama na ni wahitaji lakini wanatumia njia zisizofaa kijapatia kipato......
 
pole sana na Mungu atakulipa na ndo maana umejua!
 
Huku kishapu kuna mzee anasafiri kila baada ya miezi 6 kuenda mombasa na Nairobi kule kazi yake ni omba omba kama ya hao wa gogo, ila pale ndo tajuri ana maduka na nyumba hapa senta ana wake wawili na mashamba mengi.....omba omba imekua kazi nzuri ukipata sehemu nzuri na kilema au kasoro nzuri kwenye mwili wako, utapiga pesa paka basi.
 
Hayo ndo mawazo ya wajinga
 
Dah poleni sana.

Niliwahi kumhifadhi Dogo mmoja hata sikuwa namjua alikuja kunililia shida kuwa katoka huko kwao hana pa kula wala pa kuishi,Dogo akaniambia ana ujuzi Wa kunyoa,nikamtafutia job kwa mama mmoja alikuwa mke Wa mkurugenzi Wa manispaa alikuwa na salon yake hapa town.

Akakbidhiwa saloni apige job,Dogo alipiga kazi kama mwezi hivi,Dah sitakaa nisahau mama aliponipigia simu kunijulisha kuwa salauni imekombwa kula kitu,Dogo sijui pa kumpata,
mbaya zaidi alipita pia na baiskeli ya Kijana Wa duka LA Jirani na hiyo salon.

Pona yangu ilibidi nimweleze ukweli,Dah mama akanielewa akanipa somo LA kutomwamini mtu usiyemfahamu,ila toka Siku hiyo nimekuwa makini though bado natapeliwaga ila so kwa kiwango hicho tena.
 
Umenikumbusha miezi miwili iliyopita nikiwa pale studio nasubiri daladala niende kariakoo akaja kaka mmoja mdogo mdgo umri kati ya miaka 17-19. Akaniambia dada samahani mimi naulizia machinga complex ipo wapi, mimi nikasahau ilipo nikamwambia mh hata sikumbuki ipo wapil akasema yeye ametoka singida huku amekumbatia begi lake kama wa bush haswa aliepewa story dar kuna matapeli, akaniambia ni wachimbaji wadogo wa madinj hivyo wamepata na yeye ameambia aje huku auze maana wananunua kwa bei nzuri huko machinga complex,
Ikabidi nianze kumshauri.kwanza nikamwambia mimi machinga complex sipakumbuki ipo wapi ila ukiwa unamuuliza mtu usipende kumueleza shida yako yote sababu hujui yupi atakua mwema kwako na yupi mbaya. Basi ikabidi nimpigie mume wangu kumuuliza hivi machanga complex ipo wapi, huku napiga kuna baba yupo pembeni yangu mtu mzima yule kijana akaanza kumuuliza tena yule baba machinga xomplex ni wapi na akaanza kumuelezea habari ya yeye kuja kuuza haya madini, ikabidi nimvute yule kaka nimkumbushe awe makini asubiri mme wangu apokee sim anielekeze ni wapi na asirudie tena kuwaambia watu kila kitu kuhusu yeye. Bas yule baba akaamuelekeza machinga ni wapi, huku bado nasubiri daladala yule kaka akaanza kuniambia dada nisaidie nisije nkatapeliwa na bla bla nyingi, kilichokuja nitokea hata sielewi nilijikuta science sina simu wala pesa , ikabidi niombe msaada wa nauli nirudi nyumban.
Mpak leo naomba Mungu amuongoze yule kaka, unajitoa kumsaidia mtu kwa moyo kumbe ni tapeli.
Niliapa sitosaidia tena wapita njia lkn bado najiuliza kila mtu akila hiki kiapo tutaishi vipi maana na mimi nilisaidiwa nauli ya kurudi kwangu.
Kubwa ni kuwa makini matapeli ni wengi sana na sijui wengine wanatumia dawa gani maana niliumwa almost wiki nzima na nikawa napoteza kumbukumbu
 
7000 kila siku?Sawa Kidukulilo..
 
Mimi nilikutana na Mtu kipindi kile cha mfungo wa Ramadhani akanisimamisha akaniambia hajala tangu jana ivi basi yeye anatumia ARV akasema nimpe ata elfu moja akapate chai anywe zile dawa. Nikampa buku tano kwa vile alinionesha kile kichupa cha Dawa nimekaaa kama masaa ma3 hivi namuona yule jamaa amelewa yupo chakali yupo na wenzie niliumia sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hawa ndo husababisha wahitaji wa Kweli washindwe kusaidiwa, ..... usichoke kutenda mema Mungu atakulipa “
 
Wala usisikitike, ulitenda wajibu wako kama mtu muungwana! Mungu atakulipa! Maisha na yaendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…