Mimi nilikutana na mzee maeneo ya kanisani magomeni na yeye akainiomba nauli..wakati narudi namwona kajibanza sehemu anahesabu hela nyingiπ€£Kuna siku moja alinisimamisha mzee mmoja, akaniambia mwanangu nimetoka hospitali naomba nauli nipande bajaji kwa hali yangu siwezi kutembea nikampa. Wakati anaondoka nikajilaumu kwanini nimempa hela ya bajaji wakati obvious hela ya kula atakuwa hana naye ni mgonjwa.
Namfata chap kumuongezea fedha ya chakula, kwa mbali namuona bajaji anazipita bila kupanda mpaka akazimaliza. Mbele akamsimamisha mtu mwingine anamuomba, niliumia.
Mkuu kama una amani nafsini uwe unatoa tu!nafsi ndio mwalimu mzuri wa kila jambo!!!we fanya kile nafsi ina kwambia tu!!kuna kibabu huwa kila ijumaa anapita ofisini kwangu kuomba nampa jero au buku!!
siku hiyo sikumuona kama kawaida yake ya kupita mchana siku ya ijumaa!
badala yake akapitia jioni na akanikuta ofisini!!
nikamwambia leo sina kitu mzee umechelewa nimewapa wenzio...
akaanza kulalamika leo hali mbali toka asubuhi hadi jioni hajapata vile amezoea kupata!!
nikamuuliza kiutani kwani mzee umepata sh ngapi leo??!!
elfu 48 mwanangu yaani leo ni nuksi tupu!hadi leo omba omba pita hivi usinisogelee.
mwingine huwa anatembea kwenye mahospitali na hotpot na chupa ya chai..
anasema mtoto wake kalazwa amekataa kula hvyo anaomba ela kdgo ajaribu kumnunulia mtori au supu
Umenikumbusha miezi miwili iliyopita nikiwa pale studio nasubiri daladala niende kariakoo akaja kaka mmoja mdogo mdgo umri kati ya miaka 17-19. Akaniambia dada samahani mimi naulizia machinga complex ipo wapi, mimi nikasahau ilipo nikamwambia mh hata sikumbuki ipo wapil akasema yeye ametoka singida huku amekumbatia begi lake kama wa bush haswa aliepewa story dar kuna matapeli, akaniambia ni wachimbaji wadogo wa madinj hivyo wamepata na yeye ameambia aje huku auze maana wananunua kwa bei nzuri huko machinga complex,
Ikabidi nianze kumshauri.kwanza nikamwambia mimi machinga complex sipakumbuki ipo wapi ila ukiwa unamuuliza mtu usipende kumueleza shida yako yote sababu hujui yupi atakua mwema kwako na yupi mbaya. Basi ikabidi nimpigie mume wangu kumuuliza hivi machanga complex ipo wapi, huku napiga kuna baba yupo pembeni yangu mtu mzima yule kijana akaanza kumuuliza tena yule baba machinga xomplex ni wapi na akaanza kumuelezea habari ya yeye kuja kuuza haya madini, ikabidi nimvute yule kaka nimkumbushe awe makini asubiri mme wangu apokee sim anielekeze ni wapi na asirudie tena kuwaambia watu kila kitu kuhusu yeye. Bas yule baba akaamuelekeza machinga ni wapi, huku bado nasubiri daladala yule kaka akaanza kuniambia dada nisaidie nisije nkatapeliwa na bla bla nyingi, kilichokuja nitokea hata sielewi nilijikuta science sina simu wala pesa , ikabidi niombe msaada wa nauli nirudi nyumban.
Mpak leo naomba Mungu amuongoze yule kaka, unajitoa kumsaidia mtu kwa moyo kumbe ni tapeli.
Niliapa sitosaidia tena wapita njia lkn bado najiuliza kila mtu akila hiki kiapo tutaishi vipi maana na mimi nilisaidiwa nauli ya kurudi kwangu.
Kubwa ni kuwa makini matapeli ni wengi sana na sijui wengine wanatumia dawa gani maana niliumwa almost wiki nzima na nikawa napoteza kumbukumbu
Nilikuja kuammbiwa wapo wengi wa design hiiHuyu nilikutana nae Manzese kwenye Zebra pale machale yakanicheza nikamkata jicho nikapanda bajaji nikaondoka zangu
Ila hadithi ni Kama hii hii
ππππππππWala usiumie
Katika kila tendo atendalo binadamu kwa mwenzake Mungu huwa anaangalia moyo wake,ni nini haswa kusudi la mtu kutenda jambo fulani kwa mwenzake na kama kusudi lako lilikua jema basi hakika hujapoteza!
Utavuna tu huo wema siku moja na wema huo utaenda adi kwa watoto wako, watafadhiliwa na wasiowajua!
Jamani..7000 nayo ni hela? Mxiew7000 kila siku?Sawa Kidukulilo..
Aiseee.Mimi nilikutana na Mtu kipindi kile cha mfungo wa Ramadhani akanisimamisha akaniambia hajala tangu jana ivi basi yeye anatumia ARV akasema nimpe ata elfu moja akapate chai anywe zile dawa. Nikampa buku tano kwa vile alinionesha kile kichupa cha Dawa nimekaaa kama masaa ma3 hivi namuona yule jamaa amelewa yupo chakali yupo na wenzie niliumia sana.
Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app