Jinsi nilivyotapeliwa na mtu niliyedhani ni mhitaji kumbe ni tapeli

Aisee kwa hiyo jamaa ameamua kutembea na mkono wenye usaha ili apige pesa tu, akicheza huo usaha utamuozesha mkono mwishowe utakatwa.
nahisi siyo kidonda kuna yule jamaa walimkamata ubungo miaka ya nyuma
kumbe kuna kitu ameweka mguu unaonekana kama umeoza hivi
 
[emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16]

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ila binadamu bana[emoji848]

Yaan msaada unaweza kugeuka kuwa jela watu hawajali kabisa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Dah! Inasikitisha coz thats the oldest trick na mm ilitaka kunitokeaga enz hizo, kama hujui bac ni hivi:-

Huyo dogo mwenye begi na huyo mzee liyeulizwa baada yako wote ni kitu kimoja, hapo target ilikuwa ni ww dada na walikukamata vzuri sana, pole sana jmn.
 
Hawa wanaosingizia hivi wapo wengi nimeshakutana nao sehemu tofauti, tofauti..

Kuna siku nilikuwa nakula seheme , jamaa akanijia na gia kama hiyo,

Yule mwenye cafe akamtimua kwa hasira, jama naye aliyekuwa anaomba.. akaanza kuropoka matusi kwa hasira, hapo ndio nili thibitisha hana utu wala shida yoyote!
 
mi huwa nawaza wale wanaopita na forms zao maofisini kuomba ada au msaada wa matibabu. huwa natoa kidogo kwao sijui ni kweli au nao matapeli
Baadhi mwanzoni wanakuwa na shida kweli ,
Lakini kadri siku zinavyenda huingiwa na tamaa...

So unakuta ile form ina miaka hata mitano au yakufoji.. anabadili wilaya na vitongoji kila siku vya kuomba
 
Pole, jitahidi kuwa unawasaidia wahitaji halisi ili uepuke kutapeliwa na matapeli uchwara!
 
Kuna siku nilikua town nikakatiza mitaa flan nikakuta wadada wawili wamekaa mmoja kabeba mtoto wakaniita nikasogea wakaniambia wanaenda kwao wilaya nyingine wamepungukiwa nauli pia mtoto wao alikua kalala hajala kwa hio wanaomba msaada wa nauli iwafikishe
Me nikawapa pesa kias nikaondoka baada ya siku tatu nikakutana na wale wale sehemu nyingine wakanipiga mzinga vile vile , nikawaambia leo sina pesa wakaondoka kwa aibu baada ya kuumbuka
 
Mwaka 2015, nakaa hostel(MUHAS) Kuna dada alikuwa amebeba mtoto mgongoni hajamvalisha chochote anagonga kila room kuomba msaada wa nguo au chochote kwa madai kua nyumba yao imepata shoti ya umeme na imeungua yote na vilivyomo,mdogo wake yupo amana hospital ameungua so ndio anapita kuomba msaada tukampatia, 2018 nipo makazi mengine(hostel) namuona dada yule yule na mtoto amebeba vile vile anapita anachungulia vyumban na kuwasimamisha watu,akaja room yangu akagonga mlango yeye ameshanisahau nikamuambia ukweli yule dada kuwa aondoke mahali pale kabla sijampeleka kwa mlinzi na nilimuonea tu huruma mtoto aliembeba yule dada alioniomba msamaha akaondoka.
 
Huyo jamaa ana asili ya kipemba?
 
Mi huwa natoaga tu msaada ata kuchunguza huwa sichunguz km ni wa kweli au lah. Ila sadaka ina baraka na mafanikio mbele yako. Hao inawezekana ni Wana shida kweli lkn njia zao wanazotumia ni mbaya na zisizo stahili. Kwa uluchokitoa ww ata usilalamike ww jihesabie tu kwamba unapokea baraka kutokn na moyo mzuri uliouonyesha kwa huyo muhitaji. Usijutie kwa uluchokitoa bali mshukuru Mungu kwa moyo huo mwema aliokugea.
 
Hey daah booonge la tapeli mwana
 
Wabongo wamepinda,, kumbe ni mgonjwa kweli lakini haendi kutibiwa ili aendelee kuufanya ugonjwa kitega uchumi.
 
Sasa huko kwa watoto ndio balaa. Mi kuna mtu namjua yupo hai kamchukua mwanae kamppeleka kwa watoto yatima akalelewe. ye anadunda Tu
 
Sipati picha na Mimi ungekuja kuniomba nauli nisingekuamini. by the way ni kweli I don't fuckn trust no body in this world especially wanaoombaomba
 
Wanaita Devils breath, (scopolamine) hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…