Jinsi nilivyotapeliwa na mtu niliyedhani ni mhitaji kumbe ni tapeli

at leas at least I hear something positive maana kusaidiaga matapeli siwez
 
Pole sana, watu hawa ndio husababisha hadi wale wenye shida kweli washindwe kusaidiwa, maana mtu akikuleza shida yake unaona kama ni utapeli mtupu..
 
Kukwambia ana madini hyo ni chambo ya kukuvuta😀matapeli wana mbinu nyingi sna, shukuru mungu wamekuacha salama kuna dada mmoja alikutana na hao matapeli anasema aliongozana nao kutoka posta hadi kimara nyumban kwake na akawakaribisha ndani walikomba kila kitu kilichokuwa rahisi kuhamishika. Baada ya kupata fahamu amekuta nyumba nyeupe kuuliza majirani wanasema walikuwa wanajua anahama nyumba mana wale matapeli walisema ni ndugu yao wamekuja kumuhamisha kwenda nyumba nyingine na kwa vile aliingia nao ndani hawakuwa na hofu nao...baada ya dada kupoteza faham ndani jamaa walileta Fuso wakaanza kuhamisha vitu. Dada anasema hajui alifikaje nyumbani kwake mda ule mana yeye alitoka ofisin alikuwa anaenda lunch ndio akakutana na hao watu. Tuwe makini jamani
 
Hivi hao huwa wanatumia dawa kukulaghai au ni lugha tu?
 
Sipati picha na Mimi ungekuja kuniomba nauli nisingekuamini. by the way ni kweli I don't fuckn trust no body in this world especially wanaoombaomba
Ni kweki ingekua ngumu kunisaudia kwa namna nilivyo vaa alafu nlikua naomba mia tu ya kuongezea nauli maana kweny pochi ilibaki 300 na 60000 imechukuliwa pamoja na simu
 
Du mtihani kwa kweli. Yan aliniumiza kwa kua very kind to him, imagine nampigia hadi mme wangu aniambie machinga ni wapi sema hakupokea simu,
 
Hivi hao huwa wanatumia dawa kukulaghai au ni lugha tu?
I think dawa ina husika sababu baada ya siku ile nilikua nikiumwa kichwa sana na kupoteza kumbukumbu ktk baadhi ya nyakati ndani ya wiki
 
Unasaidiaje mtu usiyemjua pesa? Binafsi hii kitu sifanyi tangu 2009 hadi leo hii. Na hili jambo niliambiwa na jamaa mmoja ni mchungaji ilikuwa ni semina akasema hili jambo.

Tangu kipindi kile hadi leo pesa ni kitu nisichokitoa kama sadaka popote. Nikikutana na mtu hivyo kama ni hela ya kula naenda mnunulia mwenyewe na njiani sitaki stori naye.

Unaweza kutoa hiyo pesa ukanunua matatizo makubwa zaidi, wanadamu si wema kabisa.
 

Hahaaa! Endelea na moyo huo huo nawe utalipwa na Maulana!
 
Wanashida ya kutokufanya kazi
 
Pole Sana, mama angu pia aliwahi kutapeliwa kwa njia hiyo
 
Niliwahi kukaa na dogo mmoja hivi hakua na mwelekeo, maisha yake yalikua magumu Sana lakini yangu uhakika wa kula ulikuwepo, siku moja nimeenda kwenye mihangaiko nilipoludi sikuamini kabeba nguo zangu zote, na uwezo wa kununua hata nguo ckuanao, Mungu mkubwa hazikuisha wiki mbili niliingiza mil. 9 cash
 
Kuna jamaa alinisimamisha njiani akalalama sana kwamba yeye ni mwalimu anatoka mkoa A kwenda B, siku hiyo amelala guest hata hela ya chumba hana na ana familia akadai nimsaidie hela ya chumba tu kuhusu kuondoka atajua mwenyewe, hapo tulipokutana alikuwa na kandambili za guest zimekatwa kwa mbele akasema amedanganya anakwenda benki kuwachukulia hela lakini kiukweli hana hela yoyote benki hivyo anafedheheka nimsaidie aepuke fedheha inayomkabili

Mimi kama mwanaume ikanigusa kwamba mwanaume mwenzangu anafedheheka wacha nimsaidie, haikuwa kubwa sana ilikuwa kama elfu 12 tu nikamwambia twende benki tulipofika karibu na benki akabaki njiani akasema ntamkuta nikamtolea hela nikampa akachukua na namba yangu

Baadae nikaja kugundua alikuwa tapeli ndio maana aliogopa kuongozana na mimi mpaka benki alijua nimemshtukia ntamkamatisha kwa askari wa benki

Hela haikuniuma ila nilichukia kudanganywa/kutapeliwa.
Nikawaza hawa matapeli ndio wanafanya tusisaidiane, kila mmoja unamuona tapeli kumbe wengine wana shida kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…