Hii ili ilinitokea mwanza, nilikua mwanafunzi kipindi hicho form 2, nilikutana na jamaa mmoja maeneo ya sahara.. jamaa alikua mchafu anaonekana mshamba na lafudhi yake ni ya kisukuma.
Nilikua na mishe zangu natembea mtu akanigusa samahn naomba kukuliza, akaniambia mimi nimetoka sengerema niliokota bahasha hii akanionesha, akasema kuna gari lilipata ajali huko kijijini kwao kwahyo wana kijiji waliokota vitu vingi tofauti tofauti kwenye ile ajali. Sasa akaniambia walitangaziwa kwamba yoyote aliyeokota kitu chchote ktk ile ajali apeleke jijini mwanza kwenye ofis fulan utapewa zawadi ya milion 3, jina hizo ofis nimelisahau maana ni zaman kidgo.
Me nikamjibu hizo ofis sifahamu zilipo labda uliza watu wengine, akaniambia yeye ni mgeni pale mwanza anaomba nimsaidie tu tuulize wote tupeleke hiyo bahasha atanipa laki 2.. sasa tukawa tunatembea tunaongea lengo langu ni kuachana nae niendlee na mambo yangu., siunajua barabaran mjini watu wengi mnapishana tu yule jamaa akamuliza mtu tunaepishana nae samahan kaka tunaomba kuuliza.
Akamuelezea vile vile kama mimi nikiwa nasikiliza pale , yule jamaa aksema hebu fungua hiyo bahasha kwanza tuone usije ukawa tapeli unataka kutapeli, jamaa akaifungua kulikua na vimawe vinang'aa yule jamaa aliyeulizwa akaniambia dogo hizi ni dhahabu alafu anaonekana hajui kama ni dhahabu kwahyo tumdhulumu ila tuliongelea pembeni bila yule mchafu mchafu mwenye mali kusikia.
Sasa yule jamaa akamwambia yule mwenye mali ww hizi ni dhahabu usipeleke ukapewe milion 3, achana nao twende mwanza hotel tukauze utapata pesa nyingi sana utatupa na sisi kidogo.. jamaa akakubali sasa tukaa sehem tupange mipango vizur ndo twende mwanza hotel, kumbuka nilikua mwanafunz wa form 2 sikua najielewa vzur hata dhahabu siijui pia ila ni mtoto wa mjini na mjanja.
Me na yule mshkaji mwingine tukaongea pembeni tumtapeli yule boya zile dhahabu[emoji1787]!! Yule jamaa akamwambia boya sasa yule boya kwamba itabidi mmoja aende mwanza hotel na jiwe kama sample sisi wengine tubaki tumsubiri, sasa yule jamaa tuliepanga nae tutapeli zile dhahabu tulikua tumeshapanga mipango pembeni ya kumdhurumu yule boya, kwahyo akasema wanipe mimi zile mali niende mwanza hotel alafu yeye atabaki na yule boya ana mzuga zuga alafu atamkimbia atanikuta namsubiri pale nje.
Mimi nikaona sawa wanipe zile mali, sasa tatzo likawa mwenye mali hatuamini kutuachia zile mali, Jamaa akatoa sim yake galaxy na sh 80,000 akaniambia na ww toa hiyo sim yko tumpe huyu akae nazo ili atuamini utangulie nkukute mbele, akanisisitiza nisimgeuke nimsubirli pale getin.
Nikatia kanokia kangu nikampa nikashika zile mali, yule boya alika kavaa koti la suti ile bahasha kaiweka kwenye mfuko wa ndani wa koti, sasa baada ya kuangalia mara ya kwanza tulisema ficha sasa sjui alikua na zile bahasha 2 hata sielew mpk leo.
Nikapewa bahasha nitangulie ila yule alinihusia sana nisimzunguke et nimsubiri pale mwanza hotel, nilivoanza kuondoka nikafika mbele mawazo yangu yakabadilika nikasema spending mwanza hotel naenda nyumbn basi nilikua speed balaa[emoji23] kufika karibu na nyumbn nikasema hebu nianglie nikakuta sio zile dhahabu ni mawe mengine ya chupa aisee nilitaka kuchanganyikiwa kisimu changu dah.
Nikarudi kule sikuwapata ila bahati nzuri nilikua najuana na wahuni na vibaka kule mtaan kwetu walikua wananikubali sana, nikamfata brother mmoja akacheka akasema twende tukaenda kule Sahara kule juu tukawakuta ila walikua wameshaiuza ile sim akaniambia mdogo wangu samehe tu, tutakutftia nyingine