Jinsi nilivyotapeliwa na wakushi ambao hutumia uchawi/mazingombwe ya kumtemesha mtu nywele na kucha

Jinsi nilivyotapeliwa na wakushi ambao hutumia uchawi/mazingombwe ya kumtemesha mtu nywele na kucha

Hv hizi pesa hawa jamaa huwa wananufaika nazo sana kama kujenga nyumba za kisasa kumilik usafir au huwa wanaishia kutumia kwa matumiz ya kula tu
Umewahi kusikia mchawi tapeli tajiri kupindukia?
 
Hao watu nilitoka nao Buguruni hadi Segerea.kufika pale stend akili ikazinduka.walisema eti nimelishwa uchawi nikatema makucha na nywele.eti nikachukue sim na TV niwape ili wanizindue.nilienda kwa mangi anipe hela nityarudisha maana home palikua pamefungwa.nikamsimulia akacheka sana.kugeuka nyuma sioni mtu washasepa.ndo kupona kwangu
 
Huna nyota ya Bahati!! hao nimesha kutana nao sana!! taaangu nikiwa seco. na karo zangu hawakuniweza!.....namie nilikuwa nawafanyia usanii mmoja alitaka nidhurumu simu palee magomeni Morocco!

baada ya mazungumzo marefuuu alisema hebu tuone simu yako nimuite Padre nikampa simu imefungwa na rubber Band siyo za dunia hii!! ikabidi acheke wala sikuwa na wais wasi nenda kapigie hata huko nje!

akazuga kidogo akanambia padre hapokei simu!.....soda misosi yake nikanywa na kula bureee!! kifupi mie ndo nilifaidi! mwingine kaja ofisini ke wa kiarabu mzuriii! kabisaaa

anakasema ataka kwenda Tanga, kuchukua biashara so nimkopeshe Laki moja tu! nikasema sawa mbona hiyo kidogo tu! ila nisubiri hapo naenda Bank kukuchukulia! akasubiri weeee! mpaka leo! anasubiri!

halafu hawanaga kumbukumbu nzuri siku nyangine usiku nakula zangu chips! kwa kioski kaja huyo huyo! kwa mambo yale yale!..nikwambaia nilikwambia siku ile unisubiri nirlipo rudi sija kukuta kumbe hukupata??

dada wa watu kakata moto palepaleee akawa wa baridiiiii!!...........

Haha Jaman haki nmecheka hapo mwishoni
 
Hii ili ilinitokea mwanza, nilikua mwanafunzi kipindi hicho form 2, nilikutana na jamaa mmoja maeneo ya sahara.. jamaa alikua mchafu anaonekana mshamba na lafudhi yake ni ya kisukuma.

Nilikua na mishe zangu natembea mtu akanigusa samahn naomba kukuliza, akaniambia mimi nimetoka sengerema niliokota bahasha hii akanionesha, akasema kuna gari lilipata ajali huko kijijini kwao kwahyo wana kijiji waliokota vitu vingi tofauti tofauti kwenye ile ajali. Sasa akaniambia walitangaziwa kwamba yoyote aliyeokota kitu chchote ktk ile ajali apeleke jijini mwanza kwenye ofis fulan utapewa zawadi ya milion 3, jina hizo ofis nimelisahau maana ni zaman kidgo.

Me nikamjibu hizo ofis sifahamu zilipo labda uliza watu wengine, akaniambia yeye ni mgeni pale mwanza anaomba nimsaidie tu tuulize wote tupeleke hiyo bahasha atanipa laki 2.. sasa tukawa tunatembea tunaongea lengo langu ni kuachana nae niendlee na mambo yangu., siunajua barabaran mjini watu wengi mnapishana tu yule jamaa akamuliza mtu tunaepishana nae samahan kaka tunaomba kuuliza.

Akamuelezea vile vile kama mimi nikiwa nasikiliza pale , yule jamaa aksema hebu fungua hiyo bahasha kwanza tuone usije ukawa tapeli unataka kutapeli, jamaa akaifungua kulikua na vimawe vinang'aa yule jamaa aliyeulizwa akaniambia dogo hizi ni dhahabu alafu anaonekana hajui kama ni dhahabu kwahyo tumdhulumu ila tuliongelea pembeni bila yule mchafu mchafu mwenye mali kusikia.

Sasa yule jamaa akamwambia yule mwenye mali ww hizi ni dhahabu usipeleke ukapewe milion 3, achana nao twende mwanza hotel tukauze utapata pesa nyingi sana utatupa na sisi kidogo.. jamaa akakubali sasa tukaa sehem tupange mipango vizur ndo twende mwanza hotel, kumbuka nilikua mwanafunz wa form 2 sikua najielewa vzur hata dhahabu siijui pia ila ni mtoto wa mjini na mjanja.

Me na yule mshkaji mwingine tukaongea pembeni tumtapeli yule boya zile dhahabu[emoji1787]!! Yule jamaa akamwambia boya sasa yule boya kwamba itabidi mmoja aende mwanza hotel na jiwe kama sample sisi wengine tubaki tumsubiri, sasa yule jamaa tuliepanga nae tutapeli zile dhahabu tulikua tumeshapanga mipango pembeni ya kumdhurumu yule boya, kwahyo akasema wanipe mimi zile mali niende mwanza hotel alafu yeye atabaki na yule boya ana mzuga zuga alafu atamkimbia atanikuta namsubiri pale nje.

Mimi nikaona sawa wanipe zile mali, sasa tatzo likawa mwenye mali hatuamini kutuachia zile mali, Jamaa akatoa sim yake galaxy na sh 80,000 akaniambia na ww toa hiyo sim yko tumpe huyu akae nazo ili atuamini utangulie nkukute mbele, akanisisitiza nisimgeuke nimsubirli pale getin.

Nikatia kanokia kangu nikampa nikashika zile mali, yule boya alika kavaa koti la suti ile bahasha kaiweka kwenye mfuko wa ndani wa koti, sasa baada ya kuangalia mara ya kwanza tulisema ficha sasa sjui alikua na zile bahasha 2 hata sielew mpk leo.

Nikapewa bahasha nitangulie ila yule alinihusia sana nisimzunguke et nimsubiri pale mwanza hotel, nilivoanza kuondoka nikafika mbele mawazo yangu yakabadilika nikasema spending mwanza hotel naenda nyumbn basi nilikua speed balaa[emoji23] kufika karibu na nyumbn nikasema hebu nianglie nikakuta sio zile dhahabu ni mawe mengine ya chupa aisee nilitaka kuchanganyikiwa kisimu changu dah.

Nikarudi kule sikuwapata ila bahati nzuri nilikua najuana na wahuni na vibaka kule mtaan kwetu walikua wananikubali sana, nikamfata brother mmoja akacheka akasema twende tukaenda kule Sahara kule juu tukawakuta ila walikua wameshaiuza ile sim akaniambia mdogo wangu samehe tu, tutakutftia nyingine
 
Yamenikuta hayo uku kwetu morogoro mitaa ya chuo cha kiislam wameondoka na simu yangu ya tecno y3
 
Nilikutana nao manzese ananiuliza ofisi gani sijui ya kuuzia madini yake

Huwa nna jicho langu moja namwangalia nalo stranger ataamua abaki au aondoke
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huna nyota ya Bahati!! hao nimesha kutana nao sana!! taaangu nikiwa seco. na karo zangu hawakuniweza!.....namie nilikuwa nawafanyia usanii mmoja alitaka nidhurumu simu palee magomeni Morocco!

baada ya mazungumzo marefuuu alisema hebu tuone simu yako nimuite Padre nikampa simu imefungwa na rubber Band siyo za dunia hii!! ikabidi acheke wala sikuwa na wais wasi nenda kapigie hata huko nje!

akazuga kidogo akanambia padre hapokei simu!.....soda misosi yake nikanywa na kula bureee!! kifupi mie ndo nilifaidi! mwingine kaja ofisini ke wa kiarabu mzuriii! kabisaaa

anakasema ataka kwenda Tanga, kuchukua biashara so nimkopeshe Laki moja tu! nikasema sawa mbona hiyo kidogo tu! ila nisubiri hapo naenda Bank kukuchukulia! akasubiri weeee! mpaka leo! anasubiri!

halafu hawanaga kumbukumbu nzuri siku nyangine usiku nakula zangu chips! kwa kioski kaja huyo huyo! kwa mambo yale yale!..nikwambaia nilikwambia siku ile unisubiri nirlipo rudi sija kukuta kumbe hukupata??

dada wa watu kakata moto palepaleee akawa wa baridiiiii!!...........
hao huwa pia wanaangalia na watu wa kuwatapeli, dawa wanazo ila inategemea na reception atakayoipata na hao jamaa 90% sura zao ukiziona tu unajua ni teja
 
Tapeli akiongea maneno 7 nshamjua
lkn pia wanaangaliaga hasa ukishangaa shangaa!! au km umevaaa Laizoni, usoni umepaukaaa kidogo hata upake mafuta....sura ya mjini na ya pori tofautiiii... wanajua enheeee! huyu wakuja!
 
Pole sana mkuu hawa jamaa siyo watu wazurii
Kuna uzi niliandika kama huu kuna mkasa ulimkuta jamaangu unaweza pita uucheki niliandika
KUTAPELIWA SIYO USHAMBA
 
Ni ukweli matapeli wapo na wanatapeli, mwaka 2018 December sita sahau maisha yangu yote, hawa wa kuda walinitapeli kila nilicho kuwa nacho, ngoja niwapeni mkasa wangu[emoji116][emoji24]

Ilikua ni Asubuhi ya saa 5 nikaondoka nyumbani Tegeta-Madale kuelekea Kariakoo kununua suruali na n.k sikumbuki vingine nilivyo nunua ila kila kitu nilivyo nunua vilikua na thamani ya 70k simu pia nilitapeliwa pesa taslimu kana 17k kwa jumla nilitapeliwa vitu vyenye thamani ya Tzs 300k...

Mbinu walizotumia kunikamata ni zile zile alizo sema mtoa uzi tofauti ni moja tu mimi baada ya mzee wa makamo mwenye umri kati ya 46-53 kukutana na e uso kwa uso ilikua ni mitaa ya Msimbazi na Livingstone akajifanya ana niulizia mtaa wa Mafia kuna hotel moja ana enda huko kuna mama mmoja huwa anampekea kuku wakienyeji ana hotel

Nikamjibu mimi mtaa wa Mafia siufahamu, ghalfa atokea kijana mmoja mwenye umri kati ya 27-32 yule mzee akajaribu kumuuliza huo mtaa yule kijana akasema ana pafahamu wakati mimi bado nime zubaa yule kijana akasema tumsindikize wote ni hapo tu maana yeye ana haraka ya kwenda wapi sikumbuki...

Njiani yule akaleta pigo za vistori vya kikuda mara ooh..! Tukimfikisha yule mama ata weza kutuzawadia chochote tayari nikaingiwa na tamaa yule tapeli mwenzie kijana wa 27 umri nae ana sapoti tuende tukupeleke tu kufika huko mbele zikaanza stori za yeye ni mganga yaani ni full kama ulivyo simulia mtoa mada hapo juu ndio hivyo nilipigwa kana mbwa koko

Nilicho jifunza katika heka heka hizi ni ili utapeliwe ni lazima uingizwe kwenye hii mitego

1.una wekwa kwenye mtego wa tamaa
2. Usamaria wema/huruma (hii kitu ili nigharimu sana)
3. Kuaminishwa imani za kishirikina
4.nyingine mtaongezea na ninyi
 
Nikiwa darasa la sita arusha nikakutana nao mitaa ya sabena. Ananiuliza hospitali ya macho nikamjibu sipajui akatokea anaepajua et tumpeleke atatupa hela tugawane. Me kuskia hela nshapiga hesabu za matumiz safari ikaanza. Tukashuka posta meru tukakatiza arusha meru sec hao uwanja wa nmc sahiv ndo samunge tukavuka kimfereji njian wananipigisha story kwamba niwachezesha jackpot bingo mara anafanya utabiri wa hapa na pale me nasema huyu mchezesha jackpot mbona kavaa viatu vimeisha upande. Na ilikuwa jpl nkuwa naenda kanisan st teresa ile tumefika karibu nakumaliza uwanja wa arusha sec kuna jomba mmoja alikuwa anachunga ng'ombe afu anavuta bangi alikuja speed kali huku anatukana wale jamaa matus mazito kuwa mnampeleka wap dogo mnataka mkamuibie wale jamaa walifungua turbo sijawahi kuona. Nilibaki nimeduwaa magoti yamelegea mfukon nkuwa na jero sijui yasadaka nkamshukuru tu yule jomba akanambia ukaniombe nanilimuombea kweli kwanzia hapo Nkawa nkikutanaga nao naanza kuchekaa mpaka tukazoeana nao maana walikuwa na hapo hapo town
 
Back
Top Bottom