Jinsi nilivyotapeliwa na wakushi ambao hutumia uchawi/mazingombwe ya kumtemesha mtu nywele na kucha

Jinsi nilivyotapeliwa na wakushi ambao hutumia uchawi/mazingombwe ya kumtemesha mtu nywele na kucha

Pole sana mimi nimeshawai kuwachukulia simu zao zaidi ya mara3 uku wananiona na chakufanya awana..nina visa kama vitatu vya uwo utapeli nitavileta apa jukwaani nikitulia.
 
Waliniibia begi langu jipya la laptop na Tsh700 nilitembea nao kuanzia Temeke stereo mpaka Uhasibu mbwa wale kipindi hiko Niko Form One.
 
Nasikiaga tu ukiingia kwenye 18 zao hata ulikuwa na senti mpesa utaenda kuchomoa.
 
miaka ya 2004 iv nikakutana nao pale stand ya mwenge Zamani NBC bank nikatoka nao hapo mpk Magomeni Butiama hotel ndo nimetoka kununua Nokia 3310... hawakunipata nilikutana na binamu yangu ile kumsalimia tu kuwacheki hao washatimua sikuwaona ikawa pona yangu.
 
Nikiwa darasa la sita arusha nikakutana nao mitaa ya sabena. Ananiuliza hospitali ya macho nikamjibu sipajui akatokea anaepajua et tumpeleke atatupa hela tugawane. Me kuskia hela nshapiga hesabu za matumiz safari ikaanza. Tukashuka posta meru tukakatiza arusha meru sec hao uwanja wa nmc sahiv ndo samunge tukavuka kimfereji njian wananipigisha story kwamba niwachezesha jackpot bingo mara anafanya utabiri wa hapa na pale me nasema huyu mchezesha jackpot mbona kavaa viatu vimeisha upande. Na ilikuwa jpl nkuwa naenda kanisan st teresa ile tumefika karibu nakumaliza uwanja wa arusha sec kuna jomba mmoja alikuwa anachunga ng'ombe afu anavuta bangi alikuja speed kali huku anatukana wale jamaa matus mazito kuwa mnampeleka wap dogo mnataka mkamuibie wale jamaa walifungua turbo sijawahi kuona. Nilibaki nimeduwaa magoti yamelegea mfukon nkuwa na jero sijui yasadaka nkamshukuru tu yule jomba akanambia ukaniombe nanilimuombea kweli kwanzia hapo Nkawa nkikutanaga nao naanza kuchekaa mpaka tukazoeana nao maana walikuwa na hapo hapo town
Nilikutana nao mitaa ya Arusha Meru,
Style zao ndio hizo hizo wanaulizia sehem kama wadau walivyoandika...
Ujingaujinga wao nimsindikize sijui wapi mara katokea mwingine...
Nilicheka nikawapuuza nikasepa.
 
lkn pia wanaangaliaga hasa ukishangaa shangaa!! au km umevaaa Laizoni, usoni umepaukaaa kidogo hata upake mafuta....sura ya mjini na ya pori tofautiiii... wanajua enheeee! huyu wakuja!
Wewee acha majivuno, wanapigwa sana Daslam wazawa typical, downtown. Script ikiwa nzuri na inaangukia shida na tamaa zako tayari.
Haujawahi kupigwa hata katika mapenzi, mtu akaiba feelings. Sasa ndio kama hivyo. I love you...unaitikia i love you too.
 
Wewee acha majivuno, wanapigwa sana Daslam wazawa typical, downtown. Script ikiwa nzuri na inaangukia shida na tamaa zako tayari.
Haujawahi kupigwa hata katika mapenzi, mtu akaiba feelings. Sasa ndio kama hivyo. I love you...unaitikia i love you too.
Weweee!! ukweli ndo ujivuni???.......yaani nyie wanakijiji ndo zenu, tunawajua tu kwa miandiko yenu! mnatuona wana Diaspora/ Dai salama tunariiiingaaa, tunajisiiikiiiaaaa,

sababu tu eti tuna kaa Maghorofani, ni wazuri wa maumbo ajli ya joto, warefu watanashati, tunakula nyama choma/mbuzi. roast za kumwaga/viti myoto, ndizi mnunurisho kila siku, Basi mnakuwa na vinyongooo!

Mpiga Debe wa Bongo/Dalali, sijui dereva wa bodaboda mbongo, ukimuona anavo pendeza utadhania ofisaaa! anakula vizuri na kulala pazuri! sasaaa ulinganishe na mpiga debe wa ntwara maweee!

eti sisi wadaisalama ni wajivuni! nyie wa kijiji mna shida sana, na bado mtakoma tu!...huko Mikoani hatuji ng'ooo!... sikia sie Down town hapigwi kijinga ivo!

sababu anajua kila kona ya jiji, zaidi atawatumia vibaka hao hao! kukujua ulipo, watakuliza utakosa mtetezi, kibaka utajificha wapi?? saaana utajipalia Mkaaa! usifanye yako kwa uhuru, mnaopigwa ni nyie wa kuja!

Wanajua nikipigwa kwenye Mapenzi najua pa kuwa kamatia tena kirahisi sana na wale!! wale! kwani hujawahi ona mdada au mkaka anaazima nguo kwa watu ajisetiri! au mwingine anaomaba Nauri??

Basi ndo km hao wakibugi wanaingiaga cha kike! kwa watoto wa mjini!...hatuendi polisi bali tunamalizana kimjini mjini!......muacheni turinge sisi wabongo level nyangine kabisa hatuna vikwapa!
 

Weweee!! ukweli ndo ujivuni???.......yaani nyie wanakijiji ndo zenu, tunawajua tu kwa miandiko yenu! mnatuona wana Diaspora/ Dai salama tunariiiingaaa, tunajisiiikiiiaaaa,

sababu tu eti tuna kaa Maghorofani, ni wazuri wa maumbo ajli ya joto, warefu watanashati, tunakula nyama choma/mbuzi. roast za kumwaga/viti myoto, ndizi mnunurisho kila siku, Basi mnakuwa na vinyongooo!

Mpiga Debe wa Bongo/Dalali, sijui dereva wa bodaboda mbongo, ukimuona anavo pendeza utadhania ofisaaa! anakula vizuri na kulala pazuri! sasaaa ulinganishe na mpiga debe wa ntwara maweee!

eti sisi wadaisalama ni wajivuni! nyie wa kijiji mna shida sana, na bado mtakoma tu!...huko Mikoani hatuji ng'ooo!... sikia sie Down town hapigwi kijinga ivo!

sababu anajua kila kona ya jiji, zaidi atawatumia vibaka hao hao! kukujua ulipo, watakuliza utakosa mtetezi, kibaka utajificha wapi?? saaana utajipalia Mkaaa! usifanye yako kwa uhuru, mnaopigwa ni nyie wa kuja!

Wanajua nikipigwa kwenye Mapenzi najua pa kuwa kamatia tena kirahisi sana na wale!! wale! kwani hujawahi ona mdada au mkaka anaazima nguo kwa watu ajisetiri! au mwingine anaomaba Nauri??

Basi ndo km hao wakibugi wanaingiaga cha kike! kwa watoto wa mjini!...hatuendi polisi bali tunamalizana kimjini mjini!......muacheni turinge sisi wabongo level nyangine kabisa hatuna vikwapa!
Majivuno again!! 😆😆. I don' wanna hurt you diaspora😆. Vipi huyo katika picha ni wewe?🤗
 
Mtu akinishawishi jambo lolote likielekea kama miujiza miujiza, kuamini amini, kutabiri tabiri. Amenikosa.

Simpi hata sekunde ya kuendeleza sanaa yake. Na wengi hupotelea mbali.

Enzi hizo watu wawili walinijia mmoja akajifanya mtabiri. Eti hata kifimbo cha Mwl. Nyerere katengeneza yeye. Baadaye anataka nimpe kiganja aweke moshi wa sigara. Niligoma.

Tapeli mwenzake akafungua kiganja, mtabiri akageuza majivu kuwa noti, enzi hizo ya shilingi kumi.
Huyu wa pili akajifanya kushangaa sana. Mimi nilikauka kama sikuona kitu.
Wakaondoka baada ya kuona sijali kitu.

Watu wengi pia hutapeliwa sababu ya kupenda njia za mkato.

Unaweza punguza uwezekano wa kutapeliwa kwa kuacha kuendekeza baadhi ya mambo ya mkatomkato.
 
Majivuno again!! 😆😆. I don' wanna hurt you diaspora😆. Vipi huyo katika picha ni wewe?🤗
Ndo maana mnakufa mapema wanakijiji!!! sie ndo tulivo! nyie mwaona majivuno shekhe! majivuno again and again! mnaendelea kuumia mijidonda ya tumbo! mnakufa kwa mengi! sasa tunanuua Meli ya wana daisalama!

halafu tunapendana sana! tukijua weye no mbongo kindaki ndaki! unakula bure!
 
Ndo maana mnakufa mapema wanakijiji!!! sie ndo tulivo! nyie mwaona majivuno shekhe! majivuno again and again! mnaendelea kuumia mijidonda ya tumbo! mnakufa kwa mengi! sasa tunanuua Meli ya wana daisalama!

halafu tunapendana sana! tukijua weye no mbongo kindaki ndaki! unakula bure!
Hahaha😆😆🤗.
I let you win, sababu unashindana na ukweli. Nilisema kila mtu anaweza kutapeliwa, hata Dar downtown...nikasema ulichoandika ni majivuno. Kosa au tatizo liko wapi?
Jibu kwa busara, au na mimi nitaandika kama wewe😆😆
 
Hahaha😆😆🤗.
I let you win, sababu unashindana na ukweli. Nilisema kila mtu anaweza kutapeliwa, hata Dar downtown...nikasema ulichoandika ni majivuno. Kosa au tatizo liko wapi?
Jibu kwa busara, au na mimi nitaandika kama wewe😆😆
Lool! dis is completely nonsense!.....I cannot be 'u, as de villager as you're! never! come what may!.. If en' If' -u let me win, it's just b'se u've nothin' to argue about ma gorgeous drift!

What's wrong for me! to brag concernin' ma Bongo land guy?? dats how we are!! en' no body shall take it way from me/us!.. here we stand to be Wana Daisalama, tunakula na kusaza, hatuogopi kitu, sisi ndo sisi!!

Ukija kishamba! Shamba! tuna ku magufurisfy! hata humu humu jaribu uone! kwani weye hujui wenzako km weye kuwa Dodoma wana enda na kurudi???

hata km tunajidai na tunajua kuwa tuna jidai! so what? tujikatae?? ukiona vepi kunywa sumu tu!...huko hatuji ng'oo! mtasubiri sana! sikia sasa likizo tunakwenda zetu Ulayaaa, South. USA, Australia na Japan tu!

Na kwa taarifa yako tuna viwanja huko! viwanda ndo usiseme! dogo...endelea kulima Majaruba, ukiongea saana hatuta nunua ivo vimazao vyenu! uone utamuuzia nani! na mipaka tunafunga zaidi!

Bongo sisi ndo tunawagawia hela huko halafu unaleta dharau hapa eti tunajidai?? enhee! wkt tunawawezesha wewe tutakupiga laana mpaka utembee kinyume nyume!

Yaani wala hata sijakosea Mkuu! sisi wana Daisalama ndo sisi! ndo sisi haswaaa! hata weye uko humu ajili ya kijana wetu aliye somea Bongo Land ukibisha! kataa! hakuna mtandao wa kijamii unaorindima km huu wa wana bongo!

teete teteheheheheh!! tuko juuuuuu! Bab tulia umeze utatufanyia nini!!! bando lenyewe la mawazo hilo mpka wafungue duka la kijiji! sijui saa ngapi, hapa utajibu mwezi kesho... baada ya kuvuna vitunguu!

rafiki yako kaja na Mwembwe nyingii mara atufungie mtandao wetu weeeee! unajua tulicho mfanya??....jifunzie hapo!
 
Hiyo style ya kutapeli sio dawa unapiga maneno mazuri ya uongo yanayoendana na ukweli mwisho unafanyiwa jambo la kutisha mfano tafuna hii karatasi tema mkononi ile kutema kiganjani nywele kumbe bila kujua walizichanganya ndani karatasi baada ya hili tukio wanakwambia unaona ulilishwa nywele za maiti sasa unatakiwa tukutibu kabla ya kukutibu unatakiwa uende njia panda utaokota pete kwa hiyo mkabidhi mwenzako vitu vyako ulivyo navyo ile kwenda tu na wao wanaondoka nimefupisha kwa haraka ukielezea neno kwa neno yanaweza fika maneno elfu saba.
 
Double check yourself. Unaandika ndoto zako na ushamba wako😆😆😆.
Okay moja sijawahi kulima tangu nizaliwe, but i respect farmers...
Sijawahi kulima tangu nizaliwe, sijawahi kuwa ktk chama cha baba yako. What's ya point?
Ujanja hauna wewe😆😆. Na jeans yako ya afutatu dp😆😆😆
 
Dah kuna mishe moja nilikuwa napiga mitaa ya Samora, sasa mchana nikatoka break, nikakaa ile garden iliyokarabatiwa na Makonda🚬.
Kuna washkaji bana wakawa wanapiga stori jinsi wanavyotegesha mingo karibia na jengo la Freemason, wanawapiga wataka slope na kuwapa risiti za kutengeneza zenye logo za freemason😆🤔
 
Aisee mimi nakumbuka mwaka 2005 nikiwa natoka shule Sengerema secondary school (sesesco) naenda nyumbani likizo, ilikuwa ni december.
Sasa wakati nimevuka tu pale kamanga ferry nikakutana na jamaa mmoja hivi wa heshima tu, age yake ilikuwa kati ya 40-45. Akaniuliza dogo unaenda wapi? nikamjibu naenda Nyakato national ila sijui stand ya daladala za kwenda huko ipo wapi. Akasema usijali na mimi (yeye) naelekea huko. Bs nikafurah kuona nimepata mtu wa kunifikisha stand.
Sasa wakati tupo njian tunatembea taratibu kuelekea stand jamaa akaniuliza kama nina chenji ya tsh 10,000, nikamwambia sina ila nina tsh 7000.
Akasema nipe hiyo hiyo tukifika hapo mbele nitachange nikurudishie hela yako. Aisee sijui akili huwa tunapeleka wapi, kufika mbele kidogo akaniambia nisubili hapa niende nikachange hii pesa ili nikupe hela yako akaniachia kimfuko chake hivi alichokuwa nacho.
Nilisubir zaid ya lisaa kabla sijajua kwamba nishapigwa[emoji23][emoji23][emoji23]bila jamaa kutokea. Kuangalia kwenye ule mfuko nakutana na vile viembe vitamu tena vimeoza[emoji35][emoji35][emoji35]. Namshkr Mungu nilikuwa na miatatu mfukoni iliyonifikisha kwa shangazi yangu. Tokea hapo tapeli yoyote akijichanganya anakula ngeta ya maana
 
wanakupumbaza akili kwa madawa ya kienyeji ama technique wazijuazo wao na kukufanyia mazingaombwe ya kukutemesha kucha au nywele, huwa wanakua wawili mmoja anajifanya anauliza sehemu mwengine anajifanya mpita njia.

Mkasa wangu niliwahi kumsimulia mtu moja tu wa karibu sana, wengine huwa nadanganya kwamba "ilibaki kidogo nitapeliwe", "niliwatoroka", "nilijiongeza", n.k, hivi ni vichaka ambavyo watanzania wengi tunavikimbilia kukwepa aibu ya kuchekwa na kuonekana washamba ila kiuhalisia sio ushamba, haya mambo hata maprofesa wanaliwa timing wanaingia kingi ila wanapiga kimya, hata hao wanaocheka na kuwaona wenzao ni washamba nao wameshawahi kutapeliwa ila wanaficha ukweli. Huku JamiiForums kuna usiri kwa hio naweka mkasa mzima.

Kilichonikuta mimi ni hiki;

Ilikua mida ya mchana majira ya saa saba katika jiji mojawapo hapa nchini, niliondoka ofisini niende centre kwenye maduka kununua vifaa kwajili yakukamilisha kazi ya mteja, nilipofika centre nilishuka kwenye bajaji nikaanza kutambea kuelekea madukani, mbele hatua kadhaa nilikutana na mzee mmoja wa makamo mwenye umri Kama miaka 48 au zaidi na alikua amevalia tisheti nyeusi na suruali ya jinsi ya blue iliyopauka kwa kuchakaa.

Alinifuata na kuniuliza "Kijana hoteli ya wapemba unaifahamu? Mimi ni mgeni katika hili jiji naomba unielekeze”. Kabla hajamaliza kuna mpita njia kijana alipita amesimama karibu yetu ni kama anataka kuvuka barabara, yule mzee akasema ngoja nimuulize huyu kijana.

Akamuuliza, "Samahani kijana hoteli ya wapemba unaifahamu?" Yule mpita njia akamwamuonesha kwa kidole akiangalia upande wa mashariki akasema “Hoteli ya wapemba iko tu pale”, akamwambia yule mzee “Twende kidogo hapo mbele nimuelekeze huyu (mimi) akupeleke manake mimi nawahi stendi kumpokea mtu".

tukaanza kutembea kuelekea huko na hata sijui niliwezaje, maana nilienda centre kwa mambo mengine ila nikajikuta nafanya vingine. Tukiwa njiani ili yule mzee akaanza kusema, "Mimi nimetoka Morogoro natibu kwa kutumia kitabu, hata nyie nikiwaangalia tu viganja vyenu naweza kujua nyota zenu na matatizo yenu".

Yule mpita njia mwenzangu akamjibu"Hebu tuangalizie", akamwangalia kiganjani alitikisa kichwa kwa masikitiko akasema kwa uchungu "Wewe umehangaika sana hapa mjini lakini hujafanikiwa kwakua umelishwa kucha za maiti" jamaa alishtuka akawa kama amepanik hivi.

Ikafika zamu yangu nikampa kiganja akasema "Wewe una nyota nzuri lakini umelishwa nywele za mtoto mchanga, kuna mtu hapendi ufanikiwe zaidi ya hapa ulipo na pia nywele hizo zinakufanya usiwe na nguvu, huwezi kuja kuzalisha mwanamke". Niliingiwa na woga.

yule mpita njia akamwamba yule mzee “tusaidie kuondoa matatizo hayo mkuu" yule mzee akasema "mna kioo hapo?" tukajibu hapana akauliza mna karatasi nyeupe, yule mwenzangu akaitikia " ndio" akatoa karatasi mfukoni akampa akaishika kisha akasema " tafuneni hiyo karatasi” aliigawa vipande viwili, tukapokea na kuitafuna, akasema "haya kohoeni kwa nguvu", naam!

Sikuamini nachokiona, nikakohoa nywele kidogo na mwenzangu akakohoa kucha, baada ya hapo mzee yule alionesha kukasirika akaongea kwa ukali, "Nimesema mkohoe kwa nguvu mmekohoa taratibu, nywele zimebaki tumboni na kucha sasa mtakufa sijui niwasaidiaje”. Nilitetemeka kwa woga.

Yule mzee alikuwa kama anatafuta mbinu ya kutusaida huku kashika kichwa, mimi hapo najuta hata kukutana naye, yule mwengine anamuomba kila mara “Mzee tusaide”. Baada ya dakika 2 hivi akatuambia "Sasa sikilizeni fuatani maelekezo nitakayowapa la sivyo mtakufa hapahapa” aliongea kwa msisitizo akaanza kutoa maelekezo.

"Hizo nywele na kucha mlizotema inabidi muwahi kwenda kwenu mkazichome kwa manuizi ili mziyeyushe zilizobaki tumboni, mnavyozichoma wewe ulietema kucha nuia kucha zote zilimo tumboni ondoka na wewe wa nywele nuia nywele zote zilimo tumboni ondoka. “

Tulitafuta karatasi pembezoni, yule mpita njia alifungasha kucha zake na mimi nikafungasha nywele nilizotema. Baada ya hapo yule mzee akatuambia tuweke kwenye mifuko ya suruali lakini kama hairusiwi mifuko mingine iwe imebeba chochote, iwe ni ya suruali/jeans, shati au koti kwahiyo tuvitoe vyote tulivyovibeba tuvifungie ndani ya rambo.

Kulikuwa na kijiduka kwa karibu yule mpita njia alienda kununua vimifuko viwili ni vile vikaki, yule mpita njia aliweka saa, pesa kama elf 70 hivi na simu mbili, mimi nikaweka pesa 138,000 na simu. Tuliambiwa tuchukue pesa ya nauli tu, yule mpita njia alisema kwao siyo mbali atatembea, mimi nilichukua buku ambayo ilikuwa ndogo katika hela nilizoweka.

Zile kaki mzee akatupa zikiwa zimekazwa na akatuambia "Hii mifuko msithubutu kufungua mpaka mfike kwenu, mkifika kwenu muiweke pembeni, mchome kwanza hizo nywele na kucha huku mnanuia nilivyowaelekeza, baada ya hapo ndiyo mnaweza kuchukua vitu vyenu vya kwenye hio mifuko".

Yule mpita njia alisema anarudi kwao ambako ni karibu na ile hoteli aliyoulizia yule mzee kwahiyo wacha amsindikize kwanza mzee. Mimi nikamuaga yule mzee na kumshukuru, mzee alinikumbusha kwamba nichome kwanza zile nywele ndiyo nifungue mfuko.

Nilifika stendi ya mabasi nikapanda usafiri nikarudi kwangu, nilipofika kitu cha kwanza nilichukua kiberiti nikaenda kuchoma kile kikaratasi nilichofungashia zile nywele. Baada ya hapo sasa nikaenda kufungua kaki ili nitoe simu nicheki kama kuna missed call au message, daah!

Yaani ndani ya bahasha nilikuta vipande vya maboksi vyenye ukubwa wa zile noti na nikaona kuna kimbao fulani ukubwa kam wa simu, pamoja na uanaume huu nusu nipige ukunga aisee! Nilikagua ile bahasha kama dakika 5 hivi siamini nachokiona, nilipaniki na kuchanganyikiwa nisijue cha kufanya kwa yaliyonikuta.

Nilirudi centre ile sehemu niliyowakuta nikazunguka sana mpaka kule eneo la tukio, nilikuwa nauliza watu wenye shughuli zao maeneo hayo kama wamewaona nikijaribu kuwaeleza walivyovaa na walivyo ila hakuna aliewaona, wengine nikiwauliza hata kabla sijamaliza wanajibu kwa mkato, umeshapigwa!

Basi hayo ndiyo yaliyonikuta, nikisimulia wenzangu huwa nawadanganya kwamba nilijiongeza kiakili nilikataa kutoa pesa na simu nikaondoka nikaamua liwalo na liwe lakini ukweli bado naujua mimi mtendwa kwamba niliingizwa chaka.
Hii stori na mimi ilishanitokea na mtiririko wake unafanana na huu 100%.
Kwangu walipita njia zote kama walizopita kwako. Tumetofautiana tu hapo kwenye aina ya matatizo waliyoyaona baada ya kuwaonesha kiganja.
Moja ya kitu kilichonifanya niwaamini ni pale nilipowapa kiganja na kuniambia "dooh pole sana kijana, wewe una tatizo kila ukipata hela matatizo yanaingia" na kwakweli hilo ni tatizo ambalo ninalo na linanitesa hadi leo.
Yani kila nipatapo senti lazima nipate matatizo eitha mtoto aumwe, ndani vitu vimeisha ghafla tu na hata hela yenyewe ninavyoitumia mpaka kuisha kwake nakuwa sielewi elewi.

Hili jambo lilinifanya niwaamini na nilijikuta nawaachia Simu bila kujijua
 
Back
Top Bottom