political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,827
- 5,994
Pole sana mimi nimeshawai kuwachukulia simu zao zaidi ya mara3 uku wananiona na chakufanya awana..nina visa kama vitatu vya uwo utapeli nitavileta apa jukwaani nikitulia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilikutana nao mitaa ya Arusha Meru,Nikiwa darasa la sita arusha nikakutana nao mitaa ya sabena. Ananiuliza hospitali ya macho nikamjibu sipajui akatokea anaepajua et tumpeleke atatupa hela tugawane. Me kuskia hela nshapiga hesabu za matumiz safari ikaanza. Tukashuka posta meru tukakatiza arusha meru sec hao uwanja wa nmc sahiv ndo samunge tukavuka kimfereji njian wananipigisha story kwamba niwachezesha jackpot bingo mara anafanya utabiri wa hapa na pale me nasema huyu mchezesha jackpot mbona kavaa viatu vimeisha upande. Na ilikuwa jpl nkuwa naenda kanisan st teresa ile tumefika karibu nakumaliza uwanja wa arusha sec kuna jomba mmoja alikuwa anachunga ng'ombe afu anavuta bangi alikuja speed kali huku anatukana wale jamaa matus mazito kuwa mnampeleka wap dogo mnataka mkamuibie wale jamaa walifungua turbo sijawahi kuona. Nilibaki nimeduwaa magoti yamelegea mfukon nkuwa na jero sijui yasadaka nkamshukuru tu yule jomba akanambia ukaniombe nanilimuombea kweli kwanzia hapo Nkawa nkikutanaga nao naanza kuchekaa mpaka tukazoeana nao maana walikuwa na hapo hapo town
Wewee acha majivuno, wanapigwa sana Daslam wazawa typical, downtown. Script ikiwa nzuri na inaangukia shida na tamaa zako tayari.lkn pia wanaangaliaga hasa ukishangaa shangaa!! au km umevaaa Laizoni, usoni umepaukaaa kidogo hata upake mafuta....sura ya mjini na ya pori tofautiiii... wanajua enheeee! huyu wakuja!
Weweee!! ukweli ndo ujivuni???.......yaani nyie wanakijiji ndo zenu, tunawajua tu kwa miandiko yenu! mnatuona wana Diaspora/ Dai salama tunariiiingaaa, tunajisiiikiiiaaaa,Wewee acha majivuno, wanapigwa sana Daslam wazawa typical, downtown. Script ikiwa nzuri na inaangukia shida na tamaa zako tayari.
Haujawahi kupigwa hata katika mapenzi, mtu akaiba feelings. Sasa ndio kama hivyo. I love you...unaitikia i love you too.
Majivuno again!! 😆😆. I don' wanna hurt you diaspora😆. Vipi huyo katika picha ni wewe?🤗Weweee!! ukweli ndo ujivuni???.......yaani nyie wanakijiji ndo zenu, tunawajua tu kwa miandiko yenu! mnatuona wana Diaspora/ Dai salama tunariiiingaaa, tunajisiiikiiiaaaa,
sababu tu eti tuna kaa Maghorofani, ni wazuri wa maumbo ajli ya joto, warefu watanashati, tunakula nyama choma/mbuzi. roast za kumwaga/viti myoto, ndizi mnunurisho kila siku, Basi mnakuwa na vinyongooo!
Mpiga Debe wa Bongo/Dalali, sijui dereva wa bodaboda mbongo, ukimuona anavo pendeza utadhania ofisaaa! anakula vizuri na kulala pazuri! sasaaa ulinganishe na mpiga debe wa ntwara maweee!
eti sisi wadaisalama ni wajivuni! nyie wa kijiji mna shida sana, na bado mtakoma tu!...huko Mikoani hatuji ng'ooo!... sikia sie Down town hapigwi kijinga ivo!
sababu anajua kila kona ya jiji, zaidi atawatumia vibaka hao hao! kukujua ulipo, watakuliza utakosa mtetezi, kibaka utajificha wapi?? saaana utajipalia Mkaaa! usifanye yako kwa uhuru, mnaopigwa ni nyie wa kuja!
Wanajua nikipigwa kwenye Mapenzi najua pa kuwa kamatia tena kirahisi sana na wale!! wale! kwani hujawahi ona mdada au mkaka anaazima nguo kwa watu ajisetiri! au mwingine anaomaba Nauri??
Basi ndo km hao wakibugi wanaingiaga cha kike! kwa watoto wa mjini!...hatuendi polisi bali tunamalizana kimjini mjini!......muacheni turinge sisi wabongo level nyangine kabisa hatuna vikwapa!
Ndo maana mnakufa mapema wanakijiji!!! sie ndo tulivo! nyie mwaona majivuno shekhe! majivuno again and again! mnaendelea kuumia mijidonda ya tumbo! mnakufa kwa mengi! sasa tunanuua Meli ya wana daisalama!Majivuno again!! 😆😆. I don' wanna hurt you diaspora😆. Vipi huyo katika picha ni wewe?🤗
Hahaha😆😆🤗.Ndo maana mnakufa mapema wanakijiji!!! sie ndo tulivo! nyie mwaona majivuno shekhe! majivuno again and again! mnaendelea kuumia mijidonda ya tumbo! mnakufa kwa mengi! sasa tunanuua Meli ya wana daisalama!
halafu tunapendana sana! tukijua weye no mbongo kindaki ndaki! unakula bure!
Lool! dis is completely nonsense!.....I cannot be 'u, as de villager as you're! never! come what may!.. If en' If' -u let me win, it's just b'se u've nothin' to argue about ma gorgeous drift!Hahaha😆😆🤗.
I let you win, sababu unashindana na ukweli. Nilisema kila mtu anaweza kutapeliwa, hata Dar downtown...nikasema ulichoandika ni majivuno. Kosa au tatizo liko wapi?
Jibu kwa busara, au na mimi nitaandika kama wewe😆😆
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣dawa yao hao ni kuongea,kwa ishihara yani akikuuliza swali wewe mjibu kwa ishara
Hii stori na mimi ilishanitokea na mtiririko wake unafanana na huu 100%.wanakupumbaza akili kwa madawa ya kienyeji ama technique wazijuazo wao na kukufanyia mazingaombwe ya kukutemesha kucha au nywele, huwa wanakua wawili mmoja anajifanya anauliza sehemu mwengine anajifanya mpita njia.
Mkasa wangu niliwahi kumsimulia mtu moja tu wa karibu sana, wengine huwa nadanganya kwamba "ilibaki kidogo nitapeliwe", "niliwatoroka", "nilijiongeza", n.k, hivi ni vichaka ambavyo watanzania wengi tunavikimbilia kukwepa aibu ya kuchekwa na kuonekana washamba ila kiuhalisia sio ushamba, haya mambo hata maprofesa wanaliwa timing wanaingia kingi ila wanapiga kimya, hata hao wanaocheka na kuwaona wenzao ni washamba nao wameshawahi kutapeliwa ila wanaficha ukweli. Huku JamiiForums kuna usiri kwa hio naweka mkasa mzima.
Kilichonikuta mimi ni hiki;
Ilikua mida ya mchana majira ya saa saba katika jiji mojawapo hapa nchini, niliondoka ofisini niende centre kwenye maduka kununua vifaa kwajili yakukamilisha kazi ya mteja, nilipofika centre nilishuka kwenye bajaji nikaanza kutambea kuelekea madukani, mbele hatua kadhaa nilikutana na mzee mmoja wa makamo mwenye umri Kama miaka 48 au zaidi na alikua amevalia tisheti nyeusi na suruali ya jinsi ya blue iliyopauka kwa kuchakaa.
Alinifuata na kuniuliza "Kijana hoteli ya wapemba unaifahamu? Mimi ni mgeni katika hili jiji naomba unielekeze”. Kabla hajamaliza kuna mpita njia kijana alipita amesimama karibu yetu ni kama anataka kuvuka barabara, yule mzee akasema ngoja nimuulize huyu kijana.
Akamuuliza, "Samahani kijana hoteli ya wapemba unaifahamu?" Yule mpita njia akamwamuonesha kwa kidole akiangalia upande wa mashariki akasema “Hoteli ya wapemba iko tu pale”, akamwambia yule mzee “Twende kidogo hapo mbele nimuelekeze huyu (mimi) akupeleke manake mimi nawahi stendi kumpokea mtu".
tukaanza kutembea kuelekea huko na hata sijui niliwezaje, maana nilienda centre kwa mambo mengine ila nikajikuta nafanya vingine. Tukiwa njiani ili yule mzee akaanza kusema, "Mimi nimetoka Morogoro natibu kwa kutumia kitabu, hata nyie nikiwaangalia tu viganja vyenu naweza kujua nyota zenu na matatizo yenu".
Yule mpita njia mwenzangu akamjibu"Hebu tuangalizie", akamwangalia kiganjani alitikisa kichwa kwa masikitiko akasema kwa uchungu "Wewe umehangaika sana hapa mjini lakini hujafanikiwa kwakua umelishwa kucha za maiti" jamaa alishtuka akawa kama amepanik hivi.
Ikafika zamu yangu nikampa kiganja akasema "Wewe una nyota nzuri lakini umelishwa nywele za mtoto mchanga, kuna mtu hapendi ufanikiwe zaidi ya hapa ulipo na pia nywele hizo zinakufanya usiwe na nguvu, huwezi kuja kuzalisha mwanamke". Niliingiwa na woga.
yule mpita njia akamwamba yule mzee “tusaidie kuondoa matatizo hayo mkuu" yule mzee akasema "mna kioo hapo?" tukajibu hapana akauliza mna karatasi nyeupe, yule mwenzangu akaitikia " ndio" akatoa karatasi mfukoni akampa akaishika kisha akasema " tafuneni hiyo karatasi” aliigawa vipande viwili, tukapokea na kuitafuna, akasema "haya kohoeni kwa nguvu", naam!
Sikuamini nachokiona, nikakohoa nywele kidogo na mwenzangu akakohoa kucha, baada ya hapo mzee yule alionesha kukasirika akaongea kwa ukali, "Nimesema mkohoe kwa nguvu mmekohoa taratibu, nywele zimebaki tumboni na kucha sasa mtakufa sijui niwasaidiaje”. Nilitetemeka kwa woga.
Yule mzee alikuwa kama anatafuta mbinu ya kutusaida huku kashika kichwa, mimi hapo najuta hata kukutana naye, yule mwengine anamuomba kila mara “Mzee tusaide”. Baada ya dakika 2 hivi akatuambia "Sasa sikilizeni fuatani maelekezo nitakayowapa la sivyo mtakufa hapahapa” aliongea kwa msisitizo akaanza kutoa maelekezo.
"Hizo nywele na kucha mlizotema inabidi muwahi kwenda kwenu mkazichome kwa manuizi ili mziyeyushe zilizobaki tumboni, mnavyozichoma wewe ulietema kucha nuia kucha zote zilimo tumboni ondoka na wewe wa nywele nuia nywele zote zilimo tumboni ondoka. “
Tulitafuta karatasi pembezoni, yule mpita njia alifungasha kucha zake na mimi nikafungasha nywele nilizotema. Baada ya hapo yule mzee akatuambia tuweke kwenye mifuko ya suruali lakini kama hairusiwi mifuko mingine iwe imebeba chochote, iwe ni ya suruali/jeans, shati au koti kwahiyo tuvitoe vyote tulivyovibeba tuvifungie ndani ya rambo.
Kulikuwa na kijiduka kwa karibu yule mpita njia alienda kununua vimifuko viwili ni vile vikaki, yule mpita njia aliweka saa, pesa kama elf 70 hivi na simu mbili, mimi nikaweka pesa 138,000 na simu. Tuliambiwa tuchukue pesa ya nauli tu, yule mpita njia alisema kwao siyo mbali atatembea, mimi nilichukua buku ambayo ilikuwa ndogo katika hela nilizoweka.
Zile kaki mzee akatupa zikiwa zimekazwa na akatuambia "Hii mifuko msithubutu kufungua mpaka mfike kwenu, mkifika kwenu muiweke pembeni, mchome kwanza hizo nywele na kucha huku mnanuia nilivyowaelekeza, baada ya hapo ndiyo mnaweza kuchukua vitu vyenu vya kwenye hio mifuko".
Yule mpita njia alisema anarudi kwao ambako ni karibu na ile hoteli aliyoulizia yule mzee kwahiyo wacha amsindikize kwanza mzee. Mimi nikamuaga yule mzee na kumshukuru, mzee alinikumbusha kwamba nichome kwanza zile nywele ndiyo nifungue mfuko.
Nilifika stendi ya mabasi nikapanda usafiri nikarudi kwangu, nilipofika kitu cha kwanza nilichukua kiberiti nikaenda kuchoma kile kikaratasi nilichofungashia zile nywele. Baada ya hapo sasa nikaenda kufungua kaki ili nitoe simu nicheki kama kuna missed call au message, daah!
Yaani ndani ya bahasha nilikuta vipande vya maboksi vyenye ukubwa wa zile noti na nikaona kuna kimbao fulani ukubwa kam wa simu, pamoja na uanaume huu nusu nipige ukunga aisee! Nilikagua ile bahasha kama dakika 5 hivi siamini nachokiona, nilipaniki na kuchanganyikiwa nisijue cha kufanya kwa yaliyonikuta.
Nilirudi centre ile sehemu niliyowakuta nikazunguka sana mpaka kule eneo la tukio, nilikuwa nauliza watu wenye shughuli zao maeneo hayo kama wamewaona nikijaribu kuwaeleza walivyovaa na walivyo ila hakuna aliewaona, wengine nikiwauliza hata kabla sijamaliza wanajibu kwa mkato, umeshapigwa!
Basi hayo ndiyo yaliyonikuta, nikisimulia wenzangu huwa nawadanganya kwamba nilijiongeza kiakili nilikataa kutoa pesa na simu nikaondoka nikaamua liwalo na liwe lakini ukweli bado naujua mimi mtendwa kwamba niliingizwa chaka.