Jinsi Nilivyotengeneza Million 5 kwa Mwezi kupitia Biashara ya Chakula Dar es Salaam, Maeneo ya Mwenge

Jinsi Nilivyotengeneza Million 5 kwa Mwezi kupitia Biashara ya Chakula Dar es Salaam, Maeneo ya Mwenge

Hesabu yake ana maana anauzia watu zaidi ya mara 95 kwa siku vyakula vyake kwa hesabu ya 2000 kwa order. Ili apate faida hiyo maana yake anauza order 190 kwa siku.
Kutengeneza 5.7 profit per month.aiseee. inabidi uwe busy sana hapo ofisini kwako.

Sasa kama hiyoni mauzo yake kwa mwezi na si faida.
Ina maana anauza sahani 95 za elfu mbili kwa siku. Aisee jamaa anawateja.
Haya wale waliosifia na kuelewa somo.
Inakubidi uuze mara 95 chakula cha elfu na kuendele kupata mauzo ya jamaa.
Upo tayari? Kazi kwako.
 
Hello waungwana wa jamiiforums Naitwa, Davidmmarista. Mimi ni kijana mjasiriamali, programmer, na mkulima. Hii ni stori yangu ya mafanikio katika biashara ya chakula, na jinsi nilivyoweza kufikia hatua ya kutengeneza milioni tano kwa mwezi.

Kila kitu kilianza kwa maamuzi yangu ya kuwekeza mtaji mdogo wa milioni moja. Nilijua kabisa kwamba ni lazima niwe na malengo na kuwa na mikakati madhubuti. Kwa hiyo, nilianza kwa kununua vyombo muhimu vya biashara, ambavyo vilikamilisha kiasi cha shilingi 400,000. Baada ya hapo, nilijua kuwa ili biashara yangu iweze kufanikiwa, lazima nimpate mwenye eneo ambapo ningeanzisha biashara yangu. Nilitembelea maeneo mbalimbali, na baada ya uchambuzi kidogo, nilikubaliana na mwenye frame moja kwenye maeneo ya Mwenge kwa shilingi 200,000 kwa mwezi wa kuanzia.

Baada ya kuhakikisha kuwa nipo katika eneo sahihi, nilijua sasa nilihitaji kuajiri mfanyakazi ambaye alikuwa na ujuzi katika upishi wa chakula bora. Niligundua kuwa kuwa na mfanyakazi bora upishi kunaweza kuleta faida kubwa kwa biashara yangu. Kwa hiyo, nilimpata mdada mmoja kutoka Tanga ambaye alikuwa na vizuri kwenye kupika. Tulikubaliana kumlipa shilingi 70,000 kwa mwezi, na alikubali. Alianza kazi na haraka sana alionyesha uwezo wa kujituma sana.

Nilijua kuwa ili biashara yangu iweze kuwa na mafanikio, lazima nisimamie kila kitu mwenyewe. Hii ilikuwa ni kazi kubwa, lakini nilikuwa tayari kufanya juhudi zote. Mwaka jana, mwezi wa 6, nilielekea sokoni Mabibo nikaenda kununua vyakula vya kutosha pamoja na viungo mbalimbali ili niweze kuanzisha maandalizi ya chakula. Nilikuwa na mtaji kidogo, lakini kwa akili yangu na mikakati bora, niliweza kununua samaki wazuri na dagaa kutoka kwa dada mmoja anayeitwa Tricy Dagaa yupo Twitter(X). Hali ya kupata pweza pia ilikamilika, na nilikuwa na uhakika wa kupata bidhaa za ubora.
View attachment 3233342

Kila jioni, nilikuwa na supu ya pweza ambayo iliuzwa sana, na pia chips zilikuwa ni bidhaa maarufu. Wateja walikuwa wanarudi tena na tena kwa supu nzuri ya pweza na chips za kufurahisha. Kila asubuhi, tuliandaa uji maridadi na supu iliyovutia wateja wengi. Nilijua kuwa kila sehemu ya biashara inahitaji kuwekwa kwa umakini, hivyo nikawekeza kwa kiasi cha shilingi 300,000 kwa viungo vyote. Nilikuwa na mtungi wa gesi, hivyo nilikuwa na uhakika wa kuwa na gesi ya kutosha. Nilijua kuwa ni muhimu kuwa na jiko la mkaa na vifaa vingine vya kupikia ili biashara yangu iweze kutimiza malengo yangu.
View attachment 3233353

Nikiwa na viti vizuri, sehemu ya kupumzika kwa wateja, na bango kubwa lililobeba jina langu, biashara yangu ilianza kuwa maarufu. Kila asubuhi, wateja walijaa, na chakula kilikamilika kwa haraka. Supu ya pweza ilikuwa ni maarufu sana, na wateja walikuwa wanapenda bei nafuu. Supu ilikuwa shilingi 1500, donati ilikuwa 500, na maandazi yalikuwa shilingi 200. Kila asubuhi, tulikuwa na chai ya kupendeza na kahawa nzuri. Vyakula vyetu vilikuwa ni vya bei nafuu na vilikuwa bora kwa afya ya watu. Kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa 4, biashara ilikuwa inaenda vizuri, na namshukuru Mungu kwa juhudi zote.
View attachment 3233345

View attachment 3233349

Mwisho wa mwezi, nilikagua hesabu yangu. Nilijua kuwa ningeweza kupata faida kubwa, lakini nilikuwa na shaka kidogo kwa kuwa siyo kila biashara inaweza kuwa na mafanikio makubwa. Lakini, nilikuwa na furaha kubwa nilipoona kuwa nilikuwa na kiasi cha shilingi milioni 5 na laki 7. Hii ilikuwa ni zaidi ya nilivyokuwa na matarajio. Nilijivunia sana na kutambua kuwa mimi ni mjasiriamali aliyejenga biashara kutoka chini na kufanikiwa.

Pamoja na mafanikio yangu, nilianza kuhamasika zaidi na kuongeza watu wawili wa kusaidia katika biashara yangu. Hii iliwezesha kazi kufanyika kwa haraka na vyakula vyetu kuwa bora zaidi. Tulianza kupata oda nyingi kutoka Kariakoo na maofisini mbalimbali. Ili kuendelea kuwa na ubora wa bidhaa, tuliongeza chakula zaidi kama pilau, wali, ndizi, ugali wa samaki, dagaa, nyama, na mboga za majani. Pia, tuliendelea na chips, na tukaanza kutoa full diet ya matunda.

Kwa kweli, nilijifunza jambo muhimu sana katika biashara hii: "A better service, a better income (and vice versa)." Hii ni kanuni niliyoiweka katika biashara yangu. Kutokana na ubora wa huduma, wateja walirudi na kurudia tena. Hata sasa, biashara yangu inashika kasi, na inatambuliwa kwa ubora wake. Siku moja, naamini nitaweza kuwa na biashara kubwa
kama Macdonalds.
Mpishi analipwa buku 70 kwa mwezi! Duh hatari kweli kweli hii
 
"Nikiwa na viti vizuri, sehemu ya kupumzika kwa wateja, na bango kubwa lililobeba jina langu, biashara yangu ilianza kuwa maarufu".

Ndugu unasema ulikuwa na 1m ambapo 200k ilikuwa kodi, 400k ulinunua vyombo, 300k ulinunua viungo na pia umetajaa dagaa za Tricy dagaa wa Twitter. Sasa hela za bango kubwa na viti vizuri zilitoka wapi? Pia kama sehemu yako ni maarufu kwanini usiitaje ili upate wateja wengine wa JF?

Lengo la uzi wako ni kumtangaza Tricy Dagaa, kutangaza biashara yako au kujimwambafy?
 
Sio resta mkuu ni wale wanawekaga kwa pembeni ya frame alafu 5m ni sawa na kuuza msosi wa 170k kila siku
Kweli mkuu kuna watu wana upepo wa biashara ni hatari. Kuna dogo mmoja Lusaka mwaka 2019 aliruhusiwa na mwenye duka mmoja kuwapiga watu picha za passport na za kawaida nje ya duka lake kilichotokea ni kuwa yule dogo alikuwa anajaza wateja nje ya duka la jamaa kiasi kwamba inataka kuwa kama mkusanyiko haramu.. na wateja wenyewe ni vijana na mabinti wadogo wa umri wake. Mwenye duka akamfukuza. Kwa sasa dogo naye ni miongoni mwa vijana wadogo wenye hela nyingi sana.
 
Point kubwa kwenye stori iwe kweli ama ya kufikirika ni kupata somo la kukupa ujasiri wa kukomaa na kupambania ndoto zako
 
Back
Top Bottom