Endelea...
Dada anaadithia...
Tulipokea wito wa kuitwa serikali ya mtaa ,bila kusita tulifanya hivyo .
Mazungumzo yaliyojiri pale Serikali ya mtaa yalikuwa yanataka tulipe pesa tulizokuwa tumekopa kwa mzee Issa Shaibu ambazo tuliweka dhamana ya nyumba na endapo tutashindwa kufanya hivyo itabidi nyumba yetu uchukuliwe.
Siku zilienda ikafika siku tuliyo ahidi kulipa deni lakini hatukuweza kulipa hivyo ikaamuliwe kwamba mzee Issa Shaibu achukue nyumba yetu.
Dada anaeleza walipinga uamuzi huo ambao ulifanywa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kipindi hicho ,baadaye walienda kufungua kesi mahakamani kupinga kuchukuliwa kwa nyumba yao.
Mzee Issa Shaibu alikuwa mfanyabiashara na mtu anaye jiweza kipesa kwa mtaani mtu ukikwama vipesa vidogo au hata kubwa ulikuwa unamuona huyu mzee kama una shamba ,kiwanja au nyumba unaweka kama dhamana anakukopesha ukishindwa kulipa ndio mali yako imekwenda .
Hakunaga mtu ambaye aliwahi kukopa harafu akafanikiwa kurejesha rejesho ,huyu mzee inasemekana alikuwa mchawi yaani anakukopesha pesa kidogo unaweka nyumba au kiwanja harafu anakuroga ushindwe kurudisha achukue mali yako.
Tuliporudi kutoka Tanga baada ya mganga kufariki ,mambo mengi ya shemeji yalivurugika sana biashara zilikufa maana Tangu waliponipokea walikuwa wanapoteza hela na muda mwingi sana kunihudumia hali hii ilipelekea wao kuteteleka kiuchumi .
Hivyo ilibidi wakope kiasi cha pesa ambacho kingeweza kusaidia katika matibabu ,kujikimu na kumuwezesha shemeji kufungua biashara nyingine.
Lakini kwa kipindi hicho kama ilikuwa mkosi kwa shemeji ,licha ya kukopa pesa nyingi kutoka kwa mzee Issa Shaibu za kufungua biashara kubwa kila mara msingi ulikuwa unakata yaani kama alikuwa na mkosi baada ya kurudi Tanga.
Tulikaa zaidi ya mwaka tukifuatilia kesi ya kupokonywa nyumba mahakamani.Huku shemeji akifuatilia mambo yake binafsi.
Hapa sasa familia ilikuwa kwenye wimbi la matatizo makubwa maana teyari tuna kesi mahakamani,shemeji mambo yake hayaendi na mimi ni mgonjwa kitandani.
Dada anaadithia kiukweli hakukuwa na kipindi kigumu kama hiki katika maisha yake.Ilibidi ss waanze kuangaika tena kwa waganga ili kusawazisha mambo maana kuna sehemu inaonyesha kama kuna mtu alitutupia mkosi kule kijijini baada ya kutushuku tumehusika na kifo cha mganga,na uenda ikawa mkosi huo ulikuwa mkubwa wenye lengo la kulipiza kisasi kwa kutuua hivyo nasi hatukuwa na budi kupambana kuondoa mkosi huo.
Endelea..