Jinsi nilivyougua miaka mingi na kunusurika kifo baada ya kurogewa uchawi wa bundi

Jinsi nilivyougua miaka mingi na kunusurika kifo baada ya kurogewa uchawi wa bundi

Endelea...
Dada Mwenda (Mwali) ananisimulia sasa:
Baada ya kupita miaka miwili tangu dada atoke mwali alibahatika kukutana na kijana aitwaye Mussa ambaye kwa sasa ni marehemu alifariki tangu 2010.

Kijana huyu alikuwa ni mzaliwa wa Kusini mkoani Lindi sehemu moja inaitwa Nambalapala ,lakini aliondoka kusini miaka mingi na kuweka makazi yake Jijini Dar Es Salaam.

Kijana Mussa alikuwa mfanyabiashara wa nguo .Shughuri yake kubwa ilikuwa kuchukua nguo toka Dar Es Salaam soko la Kariakoo na kupeleka mkoani Morogoro kuuza katika minada na masoko mbalimbali ya vijiji vya Morogoro na vitongoji vyake.

Pia Mussa alikuwa anachukua maharage baada ya kumaliza kuuza nguo anasafirisha kuja kuuza Dar Es Salaam ,maana Morogoror nao ni walimaji wa maharage na mbogamboga.

Endelea...
 
Dada alitamani sana kukujua Dar Es Salaam maana alisikia kuna fursa nyingi sana za kazi za viwandani na ajira.

Na hii ni kweli miaka ya nyuma wakazi wengi wa Dar Es Salaam ,walikuwa ni waajiriwa wa viwandani .Idadi ya viwanda ilikuwa kubwa kuliko hata idadi ya wakazi wa Dar Es Salaam kipindi hicho nchi nzima tulikuwa kama 17Milion tofauti ma sasa tupo tunakimbilia 60Milion.

Mkoa kama Dar Es Salaaam naweza kukadilia inawezekana tulikuwa kama laki 4 au 5 mji ulikuwa mdogo sana Mbagala ilikuwa mwisho pale kiwanda cha nguo kona ya kwenda Chanika mbele huko kote kulikuwa mapori tupu yaliyotawaliwa na simba ,chui ,tembo na wanyama wakali.Kipindi hicho kiwanja kinauzwa Tsh 80 mpaka 20 .

Kinyerezi ,Ubungo zote zilitawaliwa na mapori tupu ya wanyama wakali kama tupo Serengeti Mbugani.Ni kawaida sana kwa kipindi hicho kusikia katika redio Tanzania mtu kaliwa na Simba Mtoni Mtongani,au kusikia Tembo wamevamia Tabata na kuua watu sita

Ananiadithia dada kwamba Mussa ndiye aliyemsaidia kuja Dar Es Salaam,na alipokuja Dar Es Salaam alifikia kwa mjomba wetu ambaye kwa ss anaweza akawa na miaka kama 80 au 90 ndio aliyempokea.

Mjomba yake huyo ajulikanaye kama Alfred alikuja Dar miaka mingi sasa na kufikia sehemu moja inaitwa Kariakoo ipo mtaa unaohitwa Keko Magurumbasi karibu naChuo cha Mafunzo ya ufundi veta Chang'ombe.

Endelea...
 
Dada mwenda anaendelea kunisimulia kwamba alivyofika Dar alipata kazi kwenye kiwanda cha biskuti ambacho kipo Chang'ombe Keko maeneo ya viwanda ,hapo ndipo maisha yake yalipoanzia.

Mahusiano ya kirafiki kati ya Dada Mwenda na Mussa yaliendelea.Mussa alikuwa anamletea taarifa au barua za salamu kutoka kijijini kila akirudi Dar .Maana kipindi hicho hakikuwa na mitandao ya simu wala mitandao ya kijamii tulitumia barua tu za kuandika kwa mkono.

Baadaye Mussa na dada Mwenda walijikuta wakiwa katika mahusiano ya kimapenzi atimaye wakafunga ndoa .

Endelea...
 
Endelea.....

Baada ya Mussa na dada Mwenda kufunga ndoa atimaye mgogoro wa mashamba wa ndugu unatatuliwa (1978).
Baada ya Mussa kufunga ndoa na dada Mwenda na kujikusanya wanaamua kuja kijijini kutatua mgogoro wa mashamba kati ya familia yetu na ndugu wa upande wa babu wakitarajia labda inaweza ikaleta nafuu wale walioniroga upande wa babu wakalegeza mateso tukasamehana na mm nikapona.

Maana ugomvi mkubwa ulikuwa ni mashamba yaliyoachwa na babu ambayo sisi hatukupaswa kuyalima ,kama tulitaka kuyalima basi ilibidi tuyanunue kwa ndugu zake babu.

Lakini sisi tulitumia utemi kuyalima maana hatukukuwa na hela ya kununua na kama tusingekomaa kuyalima kinguvu basi tungekufa njaa maana maisha ya kijijini yanategemea kilimo ili mtu kuishi .

Itaendelea......
 
Tuendelee mkuu..
Dada mwenda anaendelea kunisimulia kwamba alivyofika Dar alipata kazi kwenye kiwanda cha biskuti ambacho kipo Chang'ombe maeneo ya viwanda ,hapo ndipo maisha yake yalipoanzia.

Mahusiano ya kirafiki kati ya Dada Mwenda na Mussa yaliendelea.Mussa alikuwa anamletea taarifa au barua za salamu kutoka kijijini kila akirudi Dar .Maana kipindi hicho hakikuwa na mitandao tulitumia barua tu za kuandika kwa mkono.

Baada ya muda Mussa na dada Mwenda walijikuta wakiwa katika mahusiano ya kimapenzi atimaye wakafunga ndoa .

Endelea...
 
Ni kama ulikufa ukafufuka sema mganga alikuchelewesha
 
Endelea...
Dada Mwenda (Mwali) ananisimulia sasa:
Baada ya kupita miaka miwili tangu dada atoke mwali alibahatika kukutana na kijana aitwaye Mussa ambaye kwa sasa ni marehemu alifariki tangu 2010.

Kijana huyu alikuwa ni mzaliwa wa Kusini mkoani Lindi sehemu moja inaitwa Nambalapala ,lakini aliondoka kusini miaka mingi na kuweka makazi yake Jijini Dar Es Salaam.

Kijana Mussa alikuwa mfanyabiashara wa mitumba.Shughuri yake kubwa ilikuwa kuchukua mitumba Dar Es Salaam soko la Kariakoo na kupeleka mkoani Morogoro kuuza katika minada....
Endelea...

Rekebisha kidogo, miaka ya Sabini enzi ya Nyerere hakukuwa na biashara ya mitumba.

Mitumba ilianza enzi ya Mwinyi kwenye 1986...
 
Rekebisha kidogo, miaka ya Sabini enzi ya Nyerere hakukuwa na biashara ya mitumba.

Mitumba ilianza enzi ya Mwinyi kwenye 1986...
Upo sahihi asilimia 100 ni kweli hakukuwa na mitumba mpaka ilipofika hawamu ya mzee ruksa ila kulikuwa na maduka ya nguo,kaniki n.k na kulikuwa na wafanyabiashara wa nguo wakichukua toka Dar kwenda mikoani.

Nitaondoa neno mtumba nitaweka nguo .
Asante kwa masahihisho nashukuru kuona mnafuatilia kwa makini.
 
Safari ya kupelekwa Dar Es Salaam kwa matibabu (1979).
Baada ya mgogoro wa mashamba kuisha shemeji Mussa yaani mume wa dada yangu Mwenda anaona bora anichukue niende Dar Es Salaam kwa ajiri ya matibabu ya kihospital maana anaona kijijini sipati huduma stahiki.

Kwa kifupi tu shemeji yangu huyu Mussa ambaye kwa ss ni marehemu hakuwa mtu wa kuamini uchawi na waganga na hiyo ni kawaida kwa watu waliosoma shule za mishieni chini ya kanisa katoriki kwa kipindi hicho cha nyuma.

Hivyo alisiistiza kwamba huu ugonjwa ni wa hospital hivyo ndugu walinichelewesha sana kunipeleka hospital hata hivyo hakuna ubaya yeye ataubeba msalaba na kunipeleka Dar ambako kuna hospital nzuri na za kisasa na anaamini nitatibiwa na kupona.

Kiukweli ndugu walimshukuru sana maana waliona wamepata mkombozi katika familia.Mume aliweza kupatanisha ndugu wenye ugomvi wa muda mrafu na kuwaungaisha kuwa kitu kimoja pia aligharamikia safari na matibabu yangu yote .

Endelea......
 
Back
Top Bottom