Dada alitamani sana kukujua Dar Es Salaam maana alisikia kuna fursa nyingi sana za kazi za viwandani na ajira.
Na hii ni kweli miaka ya nyuma wakazi wengi wa Dar Es Salaam ,walikuwa ni waajiriwa wa viwandani .Idadi ya viwanda ilikuwa kubwa kuliko hata idadi ya wakazi wa Dar Es Salaam kipindi hicho nchi nzima tulikuwa kama 17Milion tofauti ma sasa tupo tunakimbilia 60Milion.
Mkoa kama Dar Es Salaaam naweza kukadilia inawezekana tulikuwa kama laki 4 au 5 mji ulikuwa mdogo sana Mbagala ilikuwa mwisho pale kiwanda cha nguo kona ya kwenda Chanika mbele huko kote kulikuwa mapori tupu yaliyotawaliwa na simba ,chui ,tembo na wanyama wakali.Kipindi hicho kiwanja kinauzwa Tsh 80 mpaka 20 .
Kinyerezi ,Ubungo zote zilitawaliwa na mapori tupu ya wanyama wakali kama tupo Serengeti Mbugani.Ni kawaida sana kwa kipindi hicho kusikia katika redio Tanzania mtu kaliwa na Simba Mtoni Mtongani,au kusikia Tembo wamevamia Tabata na kuua watu sita
Ananiadithia dada kwamba Mussa ndiye aliyemsaidia kuja Dar Es Salaam,na alipokuja Dar Es Salaam alifikia kwa mjomba wetu ambaye kwa ss anaweza akawa na miaka kama 80 au 90 ndio aliyempokea.
Mjomba yake huyo ajulikanaye kama Alfred alikuja Dar miaka mingi sasa na kufikia sehemu moja inaitwa Kariakoo ipo mtaa unaohitwa Keko Magurumbasi karibu naChuo cha Mafunzo ya ufundi veta Chang'ombe.
Endelea...