Jinsi ninavyopata Faida ya 45,000/= kwa siku, huku nikiendelea na kazi zangu kila siku

Jinsi ninavyopata Faida ya 45,000/= kwa siku, huku nikiendelea na kazi zangu kila siku

Asante kwa maelezo mazuri..... Subiri niutafuteee huo uzi
Soma huu uzi upo vzuri umeelezea biashara ya bajaji

 
Wenye akili ndogo wanakuaga na mitazamo ya ajabu sana. Yote yaloandikwa umeona ni marketing tu ya pikipiki. Na hapo utakuta we ni graduate unasaka ajira
Utakuta ni hivi, utakuta ni vile.

We Jiambie lolote tu unaloona ni sawa kujiambia.
 
Kama kawaida, utamtenga vipi mswahili maskini na matusi...

Matusi ni faraja ya mtu ambaye ubongo wake umefika mwisho kufikiri, hana tumaini lolote, hivyo huishia kutukana ili ajifariji...
Wacha kukashifu shughuli za watu ikiwa wewe unaishi kwa mume wa dada yako kula kulala bure

Tuletee pdf lako hapa haraka sana
 
Wacha kukashifu shughuli za watu ikiwa wewe unaishi kwa mume wa dada yako kula kulala bure

Tuletee pdf lako hapa haraka sana

Wewe Geoffrey Christopher usitukane watu usiowajua, umesikia wewe kijana wa Mbeya?

Kati ya matamshi yangu na ya kwako, yapi yenye kuonesha kashfa?
 
Wewe Geoffrey Christopher usitukane watu usiowajua, umesikia wewe kijana wa Mbeya?
Aisee naona unatapatapa tu

Wacha kuparamia na kutajataja majina ya wanaume...utapelekewa 🔥
 
Mkuu nimetaja pikipiki zote hapo juu kuna Fekon, Huoniao, Huaojue, Boxer etc hizi zote zipo hapo juu ila kwa maeneo nilipo hizi ndio pikipiki ngumu zaidi.

Dar bila kuwa na Boxer haufanyi kazi vzuri ila huku vijijini kwetu tunatumia hizi nyingine
Kweli kabisa. Binafsi ninazo na zinaenda sawa tu.
Kwa anayehitaji soft copy ya mkataba nimeuwekaje aje PM nitampa tu..!! Baada ya hapo anaweza akarekebisha anavyoona yeye unafaa kwa mujibu wa mazingira aliyonayo
 
Changamoto madereva, ukiwekeza kwenye pikipiki faida yako iko kwa dereva. .

Ukiwa na dereva sio umeingia changa na pesa yako imewaka na moto., Hence changamoto 😊
Ukiogopa changamoto hakuna kitu utafanya.
Samaki wanaoza, nyama buchani kuna kuoza, bajaj na gari kuna kupinduka au kugongwa hadi ikawa haifai kwa matumizi ya binadamu, kuna vya kuwaka moto.. etc AND ALL IN ALL KUNA WEWE KUFA UKAVIACHA. So ni full risk
 
Jaribu kubadili mitazamo katika maisha....mitazamo mingine ni ya kimaskini sana na ndio inayowarudisha watu nyuma halafu wanatafuta mchawi
Boss, ule ulikuwa mtazamo. Nilimpa hongera kisha nikatoa mtazamo wangu. Kusema anafanya marketing ya hizo pikipiki haibadili fursa aloyoitoa kwa atakayeiona.
 
Kwa hesabu hizo bado ni biashara ambayo hailipi halafu risk nyingi
Sawa kiongozi, pikipiki moja inakupa faida ya 108,000/= kwa mwezi kwa pikipiki ya mkataba wa miezi 12 so kwa mwaka utaoata faida ya 1,300,000/= per motorcycle.

Pikipiki ya miezi 11 mkataba itakupa faida ya 109,000/= kila mwezi so kwa miezi 11 utapata jumla ya faida ya 1,200,000/= per motorcycle.

Narudia tena risk yyote ile ya barabarani ni juu ya dereva na service yoyote ile ni juu ya dereva mwenyewe.

Biashara zipo nyingi ambazo hazina RISK, so ni kipaumbele chako kuchagua chaguo sahihi uwekeze ktk biashara uipendayo na ambayo haina RISK.
 
Nitakutumia ipo kwenye pc, nitaedit baadhi ya documents then nitakutumia uione yaani ni kuweka kumbukumbu tu ya kila dereva. Kiasi alicholeta na deni lake.

Mfano mimi nawekaga kumbukumbu ya marejesho ya kila dereva kwa siku kumi za kazi yaani kama ameleta 80,000 ndani ya siku kumi basi naandika paid ni 80K na deni ni 20K so formula inajicalculate yenyewe.
Ooh ok, shukrani sana mkuu
 
Yes, ipo mikoa ambayo wakazibwake wanaheshimu sana na kuogopa mali za watu !

Biashara nzuri. Japo faida ni ndogo kama mtaji wako ni pikipiki chini ya 5
 
Back
Top Bottom