Jinsi Panyabuku walivyofanya bure kazi ambayo serikali ilitenga dola millioni 1.2 ( Tsh Billioni 3.24 ) kwaajili ya kuifanya

Jinsi Panyabuku walivyofanya bure kazi ambayo serikali ilitenga dola millioni 1.2 ( Tsh Billioni 3.24 ) kwaajili ya kuifanya

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
785
Reaction score
1,413
images - 2025-02-20T033342.991.jpeg

Huyu ni Panyabuku maji, anaishi kwenye maji na nchi kavu.


Wakati mradi wa kujenga dimbwi la maji huko jamuhuri ya Czech ulikua umekwama kwa ajili ya vibali vya ujenzi kwa miaka 7, licha ya kupata ufadhili wa dola millioni 1.2 kukamilisha ujenzi huo

siku moja watu wa maeneo hayo waliamka asubui na kukuta bwawa limeshajengwa bure kabisa na Panyabuku nane tu.

Panyabuku maji ni wanyama wa majini na nchi kavu ambao hutumia mawe, matope, na mbao kuzuia mito. Hili huunda maeneo ya maji yanayojulikana kama “madimbwi ya Panyabuku maji,” ambayo wanayatumia kama chanzo cha chakula na kinga dhidi ya wanyama wakali.

Lakini haya mabwawa pia huleta makazi kwa viumbe wengine wengi kama wadudu wa majini, samaki, vyura, ndege wakubwa kama korongo na bundi, pamoja na wanyama wakubwa kama nyati n.k, Mabwawa yao pia huzuia moto wa misitu, kunasa hewa ya kaboni, na kusaidia kudhibiti mafuriko.

Gerhard Schwab, mtaalamu wa Panyabuku kusini mwa Bavaria, hakushangazwa na kazi nzuri ya beva, lakini alishangazwa na madai kuwa walifanya kazi hiyo “usiku mmoja.”

"Naweza pia kuamini kwamba piramidi zilijengwa kwa wiki moja," alisema Schwab.

Ingawa Panyabuku wanaweza kuathiri mtiririko wa maji haraka, ujenzi wa bwawa halisi huchukua wiki kadhaa. Inawezekana hakuna mtu aliyegundua kazi yao hadi walipomaliza.

Kwa kutumia meno yao makubwa, Panyabuku hukata miti na mimea mingine, si tu kwa ajili ya kujenga mabwawa, bali pia kwa kuunda mabadiliko katika misitu.

Mabwawa yao yanaweza kuwa makubwa sana. Bwawa kubwa zaidi lililorekodiwa liko katika Hifadhi ya Taifa ya Wood Buffalo, Kanada, likiwa na urefu wa viwanja saba vya mpira wa miguu na linaweza kuonekana kutoka angani.

hawafaidishi tu wanyamapori wengine, bali pia wanawasaidia binadamu.

Kwa mfano, huko Oregon, Panyabuku walijenga mabwawa kwenye eneo la kituo kikubwa cha water treatment.

Wanasayansi walipofanya uchunguzi, waligundua kuwa mabwawa ya Panyabuku yaliweza kuchuja metali nzito na uchafu mwingine mara mbili kwa ufanisi zaidi kuliko miundo ya kibinadamu.

baadhi ya maeneo pia sasa binadamu wanaiga nama ya ujengaji wao wa mabwawa

source: Natgeo
 
Back
Top Bottom