Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Rudi nchini, huko hapakufai kabisa. Bora kulala njaa penye amani na usalama kuliko shibe penye shari na uhatarishi
Sidhani kama huo ushauri ni sahihi sana mkuu. Vipi angelikuwa ni mwanajeshi yupo vitani mstari wa mbele, ungemwambia atoroke vita?

Mimi nafikiri, badala ya kumwambia arudi nchini, mshauri namna ya kuendeleza mapambano huko huko au kwingineko hadi apte alichokuwa anakifukuzia huko.
 
Mkuu, unang'ang'ania nini huko Bondeni, rudi Bingo. Maisha ya roho mkononi yana raha gani?

Vv
Mkuu ushauri wako ni mzuri na pia wenye kujali maisha ya mtu, nakushukuru mno kwa hilo.

Tatizo tayari nishakuwa na familia. Hivyo inaniwia vigumu kuchukua uamuzi huo haraka haraka, maana watoto wapo shule now. Sasa nikirudi na hiyo elimu yetu ya huko ni kama vile nakuja kuwaharibia elimu zao na ndoto zao kwa ujumla.

Lakini kwa ushauri uliotoa ni mzuri haswa kwa mtu ambae ni bachela na hajajipanga.
 
1. I think umekuja hapa kubisha tu, na sio kusoma kilichoandikwa.

2. South sio peponi wala mbinguni, ni duniani ambapo kila mtu, hata wewe ambae unaonesha hujawahi kufika Dar unaweza kufika. Kuna wamalawi kibao ambao hata Town yao Lilongwe hawaifahamu lkn wako hapa, so usitishike au kushangazwa na mimi au mtu yoyote kuwepo hapa maana kunafikika wakati wowote.

Hapo kwenye namba 2 yako unasema nipo bongo alafu unasema tena barabara nilizozitaja ni sahihi! Mtu ambae yupo bongo kama unavyodai anawezaje kutaja kwa usahihi barabara hiyo.

3. Mimi nimeandika kwa kujiamini kwa sababu nina watu kibao humu wanaonifahamu na wanajua nipo wapi. Pia huu sio uzi wa kwanza mimi kuandika habari za huku South labda wewe ndo mgeni hapa jukwaani, hivyo unaona maajabu mno.
Unapoteza nguvu nyingi kumjibu mpuuzi
 
Kwanza poleni watafutaji wote mliopo South

Pili naomba kuuliza hivi wahanga wa mauaji kwa kiasi kikubwa huwa ni wahamiaji weusi wasiowazawa kwa hapo?

Je wazungu na race nyingine hupata madhila hayo hayo?

Yote kwa yote Afrika Kusini ni nchi hatari sana nadhani ipo kwenye tano bora za rank ya juu ya uhalifu duniani
 
It's a very normal day life in Jozi, .. kufuatiliwa, kukurupushwa, kukoswakoswa, kuporwa gari, simu na wallet , kukabwa mchana kweupe huku watu wakiendelea na shughuli zao km vile hamna kinachoendelea.....nk

Yaani gari kukufuata nyuma tu unakimbilia conclusion ya kwamba walitaka kukuuwa.... umejuaje walichokitaka?

Inawezekana
1. Wewe ni mgeni sana Jozi
2. Upo bongo, ila hii story umesimuliwa, kwani hizo road ulizotaja ni sahihi.
3.Muongo.

Unapata wapi utulivu wa kusimulia story ndefu namna hii" (with details) kwenye maisha yasiyokuwa na utulivu where every second count?
Wabongo bhana
 
1. Capitalism.


2. Historical background of the Country.

Sheria za umiliki wa silaha ziko dhaifu sana.

Watu wengi ktk nchi kuwa na Mafunzo ya kijeshi, wengine ni makomandoo kabisa wa "Umkhonto We Sizwe " (MK) lakini hawana kazi au hawajaajiriwa popote pale

3.International Migration.
Kuwepo Wahamiaji wengi kwenye nchi hiyo, illegal migrants ambao wengine ni wahalifu (crooks and criminals).
Ulichoandika yani kimepita mle mle mkuu.
 
Wewe tunakujua ni sensationalist na attention seeker plus unajua kutunga riwaya out of nothing. Huna lolote. Unatafuta sympathy tu. Labda unadaiwa mahela au unafanya drug deals zako. Nani anajua? Watu wakufukuze kwa makilomita, kona kwa kona bila sababu?
Nafikiri haujasoma maelezo ya watu wenye uelewa hapo juu, ndomaana umeandika hiki ulichoandika.

Hata hivyo sikulaumu maana wenye akili na uelewa wameshaelewa nilichoandika. Na wengi wamewahi kuishi au bado wanaishi hapa, hivyo baadhi yao wametoa ushuhuda unaofanana na huu, hivyo hili ni swala linalowakuta au lililowakuta watu wengi haswa wanaotokea uwanja wa ndege usiku.

Wewe endelea kuona kuwa haya ni mambo yasiowezekana.
 
Back
Top Bottom