Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Rudi nchini, huko hapakufai kabisa. Bora kulala njaa penye amani na usalama kuliko shibe penye shari na uhatarishi
Sidhani kama huo ushauri ni sahihi sana mkuu. Vipi angelikuwa ni mwanajeshi yupo vitani mstari wa mbele, ungemwambia atoroke vita?

Mimi nafikiri, badala ya kumwambia arudi nchini, mshauri namna ya kuendeleza mapambano huko huko au kwingineko hadi apte alichokuwa anakifukuzia huko.
 
Mkuu, unang'ang'ania nini huko Bondeni, rudi Bingo. Maisha ya roho mkononi yana raha gani?

Vv
Mkuu ushauri wako ni mzuri na pia wenye kujali maisha ya mtu, nakushukuru mno kwa hilo.

Tatizo tayari nishakuwa na familia. Hivyo inaniwia vigumu kuchukua uamuzi huo haraka haraka, maana watoto wapo shule now. Sasa nikirudi na hiyo elimu yetu ya huko ni kama vile nakuja kuwaharibia elimu zao na ndoto zao kwa ujumla.

Lakini kwa ushauri uliotoa ni mzuri haswa kwa mtu ambae ni bachela na hajajipanga.
 
Unapoteza nguvu nyingi kumjibu mpuuzi
 
Kwanza poleni watafutaji wote mliopo South

Pili naomba kuuliza hivi wahanga wa mauaji kwa kiasi kikubwa huwa ni wahamiaji weusi wasiowazawa kwa hapo?

Je wazungu na race nyingine hupata madhila hayo hayo?

Yote kwa yote Afrika Kusini ni nchi hatari sana nadhani ipo kwenye tano bora za rank ya juu ya uhalifu duniani
 
Wabongo bhana
 
Ulichoandika yani kimepita mle mle mkuu.
 
Nafikiri haujasoma maelezo ya watu wenye uelewa hapo juu, ndomaana umeandika hiki ulichoandika.

Hata hivyo sikulaumu maana wenye akili na uelewa wameshaelewa nilichoandika. Na wengi wamewahi kuishi au bado wanaishi hapa, hivyo baadhi yao wametoa ushuhuda unaofanana na huu, hivyo hili ni swala linalowakuta au lililowakuta watu wengi haswa wanaotokea uwanja wa ndege usiku.

Wewe endelea kuona kuwa haya ni mambo yasiowezekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…