Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Hivi ukihisi unafuatiliwa kama ulivyosema wewe, kwanini usiendeshe gari moja kwa moja hadi kituo cha polisi? Au nawaza ujinga?
Nilikuwa katika highway, na vituo au kituo cha polisi kipo ndani ya area (kwa ndani ndani) kama KM kadhaa kutoka barabarani kubwa.
 
Tunakoelekea,

Wote tutarudi home Tanzania.

Nchi yetu ndo makimbilio ya mataifa.

Nenda church ukatoe sadaka ya shukrani.

Amen
Yah ni kweli mkuu.
Kukiwa mazingira mazuri ya kufanya biashara au kujiendeleza kimaisha basi wengi tutaweza kufikiria kurudi.

Kuhusu sadaka, hilo nimelifanya toka jana mkuu. I mean nilituma hela bongo nikaagiza kinunuliwe chakula na kupelekwa katika shule yoyote ya watoto yatima kule Dar.
 
Yah.. watu wakikujua ni rahisi sana kukuchorea ramani. Mfano mtu anajua huyu jamaa anafanya biashara ambayo kwa siku anaingiza kiasi kikubwa cha fedha. Hivyo kama anahitaji hizo fedha na anakufahamu vizuri, basi itakuwa rahisi yeye kukuchorea ramani ya kukuibia.

1. Kwanza huenda anakuwa ashajua wewe haumiliki silaha au unayo lkn huwa unakuwa nayo muda gani.

2. Anakuwa ashajua kwamba wewe ukitoka katika biashara zako, au nyumbani kwako hupitia njia gani na wapi akienda kutinga au akituma watu wakutinge utapatikana kiurahisi.

3. Pia anajua au wanajua kwamba wewe ukitoka huwa peke yako, au unaongozana na nani kwenda kazini au kurudi nyumbani.

Kifupi ukijulikana sana nchi kama hizi huwa ni shida, kwa sababu ni rahisi sana watu kuchora mfumo mzima wa maisha yako, na hivyo kuyaweka hatarini maisha yako.
"The most dangerous enemy in your life is your closer friends, be careful of whom you chose to be your friend."
 
Pole sana. Kama wewe muislam basi zidisha swala na omba dua na toa swadaka. Kama sio muislam basi haraka uingie ktk uislam ili ukifa ufe ukiwa muislam ili ukaishi maisha mazuri
Maralia yaani tuache unyamwezi na usukuma wetu tuufuate uarabuu......na adithi zake kufikirika za mabikira 72..
Ebu kua seriously na sisi wabantu
 
Hata huko mbona watu wanauwana tena kwa bunduki mkuu, au wewe huwa haufatilii taarifa za mauaji ya USA.

Sehemu salama kuishi ni Nordic countries kama Norway, Sweden na Denmark japo kifo kikikuhitaji kutakufuata mpaka huko kukumaliza.
Sweden waarabu na wasomali na waafrika na raia wa nchi za ulaya,wasio wazungu wameshaharibu mambo...
Mfano mzuri malmo island
 
Pole sana
Maisha ni kupambana , Sina uhakika sana kama hayo majambazi walikua wanawajua au ni wale wa pata potea ( guess) TU huyu ana hela tumvamie tuchukue gari au una maisha mazuri kuwazidi.

Lakini pia ushauri wangu Jenga kujiwekea ulinzi ambao hauna gharama mf weka CCTV kamera nyumbani , kwenye gari uweke kitu cha ku-monitor usalama na ikiwekeza anza process za kutafuta bastola hata kama utaipata kwa muda mrefu maadam bado una maisha yako huko itakusaidia kwa siku zijazo.
Lkn pia acha kuamini Kila mtu Kuna Watz pia Wana roho mby anataka aje nyumban labda kakosa nauli anakuomba ukimkatalia anakutafutia majambazi wakuue so kuwa makini sana.

Usisahau kuwekeaza nyumbani Ili Watz wenzako nao wapate ajira na wewe uingize pesa na Serikali ikusanye Kodi kwa ajili ya maendeleo.

La mwisho kama una amini Mungu Katoe sadaka ya shukrani kwa kukuepusha na kifo na sisi ndugu zako tunaokuombea Kila siku ufanikiwe huko fanya mpango hata wa buku mbili kaka maisha magumu sana.
 
Haha highway za SA ukikosea outlet tu mpaka upate nyingine ni KM za kutosha..mbali na yote lakini 🙌🏻mkaburu alijenga bwana
Yani SA ni copy ya USA kwa kila kitu, kuanzia style ya maisha, utawala wa kimajimbo na kila jimbo lina fursa zake na linajitegemea, miundombinu bora, uvaaji wa askari na kila askari ana silaha kiunoni na pia wana magari ya kisasa kwa ajili ya kupakia wahalifu, maendelea makubwa, na mambo mengine mengi yanayoendana na nchi za dunia ya kwanza.

Ndio maana wazungu haswa wanaotoka Ulaya mashariki wakifika hapa lazima wajione wamefika USA kumbe wako Afrika 😂😂😂
 
Back
Top Bottom