Jinsi Putin alivyoibadilisha Urusi kuwa na nguvu ya kibabe ulimwenguni

Jinsi Putin alivyoibadilisha Urusi kuwa na nguvu ya kibabe ulimwenguni

Russia ya sasa imerithi nguvu za kijeshi na silaha kwa kiasi kikubwa kutoka iliyokuwa Umoja wa Kisovieti (USSR). Ambayo ilikuwa na muunganiko wa mataifa mengine mengi kama Ukraine, Lithuania, Estonia, Belarus n.k.

USSR ilikuwa ni taifa lenye nguvu sana kijeshi na hata kiuchumi. Ilikuwa ni nchi ya pili kiuchumi duniani baada ya Marekani kabla ya mgogoro wa ndani na hatimaye kuvunjika kwa umoja huo miaka ya 80 mwishoni na miaka ya 90 mwanzoni.

Hapo kabla, USSR iliweza kufanya vumbuzi nyingi kwenye masuala ya teknolojia, hususani masuala ya anga za mbali, na katika masuala ya kivita.

Miongoni mwa vumbuzi zao wakati wa uwepo wa USSR:

1) Mfumo wa uongozaji (navigation) wa GLONASS

2) Satellites na roketi (Sputnik 1, Soyuz)

3) Bunduki maarufu sana duniani ya Kalashnikov (AK-47)

4) Ndege za kivita za MIG (Mikoyan na Gurevich)

Na kadhalika!

Urusi ya sasa yaweza kuwa tishio kijeshi lakini si katika masuala ya uchumi tofauti na ilivyokuwa USSR. Uchumi wa Urusi sasa hivi hauna utofauti sana na jimbo moja tu la nchi kama Marekani. Mfano, Texas.
Lkn sijawahi sikia kuwa wanakopa Sana WB
 
Hiyo ni moja ya dalili kwamba huyo uliemjibu hajui hata makala inazungumzia Nini,pia haijui siasa za kimataifa lakini kubwa zaidi amechangia kwa kuiga michango ya baadhi ya wachangiani humu.
Kwa kifupi sana hajui lolote.
[emoji23][emoji23]
 
Nchi inaheshimika kwa kuwa na uchumi imara na wala sio una Nuclear Warheads ngapi.

Leo hii China, Japan na South Korea zinaheshimika zaidi duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa na wala sio kwa kujilimbikizia silaha nyingi na itakumbukwa kwamba miaka 40 iliyopita Urusi ilikuwa mbele ya hayo mataifa kiuchumi lakini leo yameiacha Russia mbali kwa sababu Russia haijui vipa umbele vyake ni nini.

Wao wangejishughulisha na maendeleo ya watu wao wakaachana na ndoto za kutafuta umaarufu wa kuuza silaha kwa sababu hiyo ndiyo imewafanya leo hii wawe maskini pamoja na akili nyingi walizonazo.
Leo hii nchi kama china ana nguvu kwa sababu ana influence kubwa sana kiuchumi nchi nyingi zinamtegemea azalishe bidhaaa wakanunue kwake

Marekani technologia ndo inayombeba, Sasa Putin anataka influence kupitia mtutu wa bunduki he has nothing to offer in economy point of view, ndo maana nchi kama Ukraine wanaona wawe upande wa ulaya kuliko urussi
 
Hujajibu swali ulilo ulizwa
Sijajibuje ananunua kwa local manufactures ambapo serekali Ina share na anawekeza kwenye research and development kote huku ni ela inatumika au unadhani zile silaha zinashushwa kutoka mbinu hakunaga cha bure ndugu

Haya ndo baadhi ya makampuni ya urussi
Almaz-Antey – air defense systems
United Aircraft Corporation – fixed-wing airplanes

Tactical Missiles Corporation – air- and naval-based missiles

Russian Helicopters – helicopters
Uralvagonzavod – main battle tanks

United Shipbuilding Corporation- submarines, corvettes, frigates, aircraft carriers.
 
Ni hivi Russia na USA wanajua kuchezea nchi nyingi Ili zinunue silaha zao mfano nakupa tu hapo Ukraine hakuna vita itatokea ila kutokana na pressure ya Russia tayari USA ameshasaini na mkataba na Poland kuwapa zana vita za USD 6B+ na bado nchi zingine, Kwa ufupi USA anafaidika na migogoro ya RUSSIA kuliko RUSSIA anvyofaidika kumbuka hao wanotengeneza migogoro ni Waisrael waliopo pande zote Mbili
Kuna mbibi fulani wa Ukraine alihojiwa na BBC wakati wanapewa silaha akasema yeye anachukua silaha ila haamini kama kuna mtu anaweza vamia ndugu zake 😝😝
 
Putin awekeze kuinua wananchi wake kiuchumi aachane na mambo ya Kununua silaha za kivita, huwezi amini Canada yenye watu million 30+ imewapita Russia kwa GDP yenye watu million 130+
Warusi wananunua silaha kutoka....
 
Amna mkuu.. Russia ili dicline after collapse of USSR .....

TOFAUTISHA. KATI YA USSR na RUSSIA
Najua tafauti baina ya USSR na Russia lakini usijidanganye kwamba Russia imepungua nguvu zake.

Bado anao mkono wa chuma kwa yale mataifa yote yaliyokuwa chini ya himaya ya USSR na hawafurukuti kwa lo lote lile.
 
Back
Top Bottom