Siyo kweli unapotumia maneno kuwa "walikuwa wanaitegemea Russia kurusha rocket zake." Baada ya NASA kustaafisha space shuttle zake na kuamua kubinafsisha usafiri wa anga za juu, walikuwa wanatumia Soyuz Capsule za urusi kwenda kwenye International space station kutokea Kazakhstan. Baada ya Elon Musk kukamilisha CrewDragon ya SpaceX, NASA wakaanza kuitumia mwaka jana, na vile vile Wanaanga wa urusi pia wameanza kutumia hiyo CrewDragon kwenda huko anga za juu. Ushrikiano baina ya Urusi na marekani kuhusu mambo ya anga za juu siyo kutegemeana. In fact inapokuwa urushaji wa roket, Marekani wana station nyingi sana za kurushia rocket kuliko Urusi. Kwa wakati huu zinazofanya kazi ni 14, wakati urusi wanazo 2 pamoja na hiyo ya Kazakhstan anbayo ndiyo kubwa zaidi ya zote.