Jinsi Sheria Hutungwa Kenya: Mwananchi Ana Nafasi Gani?

Jinsi Sheria Hutungwa Kenya: Mwananchi Ana Nafasi Gani?

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
images-10.jpg

Sheria nyingi tunazofuata nchini Kenya hazitokei tu kama uamuzi wa viongozi. Katiba ya Kenya inaweka utaratibu maalum wa kutunga sheria, huku Bunge na wananchi wakiwa na nafasi muhimu katika mchakato huo.

Mchakato huanza wakati Mswada (Bill) unapowasilishwa Bungeni. Mswada unaweza kuanzishwa na mbunge au kamati ya Bunge husika. Mswada usiohusu serikali za kaunti kwa kawaida hushughulikiwa katika National Assembly, huku miswada inayohusu serikali za kaunti ikihitaji mchakato unaohusisha National Assembly na Senate kulingana na aina yake.
images-11.jpg


Baada ya kuwasilishwa, Mswada hupitia hatua mbalimbali za mjadala Bungeni. Wabunge hujadili mapendekezo yaliyomo, na unaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kupigiwa kura.
Lakini mwananchi anaingia wapi?
images-12.jpg

Katiba, kupitia Article 118, inaitaka Bunge kufanya shughuli zake kwa uwazi na kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli za Bunge na kamati zake. Hii ndiyo sababu wananchi wanaweza kuitwa kutoa maoni kuhusu Mswada kabla haujakamilisha safari yake ya kuwa sheria.

Zaidi ya kutoa maoni, kila mtu ana haki ya kuwasilisha ombi (petition) Bungeni kuhusu jambo lililo ndani ya mamlaka ya Bunge, ikiwemo kutungwa, kurekebishwa au kufutwa kwa sheria.

Baada ya Bunge kupitisha Mswada, huwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kuidhinishwa (assent). Rais anaweza kuuidhinisha au kuurudisha Bungeni pamoja na maelezo kuhusu masuala anayopendekeza yazingatiwe. Katiba pia inaweka utaratibu wa Bunge kushughulikia Mswada uliorejeshwa.

Baada ya kukamilika kwa hatua zinazotakiwa kikatiba, sheria huanza kutumika kulingana na masharti yake ya kuanza kutekelezwa.
Kwa hivyo, kutunga sheria Kenya si jambo la Bunge pekee. Katiba imeweka mlango wa wananchi kushiriki, kutoa maoni na hata kuwasilisha petition kuhusu sheria wanazotaka zitungwe, zibadilishwe au zifutwe.
Swali kuu ni: Unapopewa nafasi ya kutoa maoni kuhusu Mswada, unajua wapi pa kuyawasilisha na maoni yako yanaweza kuathiri vipi mchakato wa kutunga sheria.
 

Attachments

  • a-guide-to-the-legislative-process-in-kenya-cover.jpg
    a-guide-to-the-legislative-process-in-kenya-cover.jpg
    7.6 KB · Views: 20
Back
Top Bottom