Kingubwe
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 210
- 165
K
Kaka hebu fafanua vizuri hapo kwenye official/custom ststus nipate mwanga kidogoSikuhizi simu hasa hizi zilizo nje ya maboks, hata kama ni dukani usiingie kichwa kichwa...
1. Ukinunua simu nenda kwenye Phone status hakikisha ni Official sio Custom, hizo ni za mbio wanazibadilisha imei, ndio Kwa kupitia imei UNAWEZA usikamatwe ila siku uka restore tuu, kwisha habari yako., haitashika network, ukilazimisha kuirudisha upo nyavuni..
2. Hakikisha pamoja na kupewa Risiti ya ki electronic (hizi mimi hua sizikubali kabisa, hua hazioneshi model, imei n.k) omba risiti ya mkono, model ya simu iandikwe,
Imei number iandikwe, hii imei ifanane na ya kwenye boksi, ndani ya simu/software na oia i match na ya kwenye hardware yasimu, namaanisha nyuma ya simu(kama ipo)
3. Piga picha pale pale dukani,
4. Haikisha unapata mhuri na risiti ni ya duka lao,
5. Hakikisha unauziwa ndani ya duka lao(kuna mawinga wanajisogeza na fremu ya mtu anajifanya ni yake, kumbe umesetiwa, mkimaliza biashara anasepa, siku umepata la kupata, unaenda unakuta mawingu.
Simu ya Mkononi..
1. Hakikisha namba Mnayotumia kuwasiliana na muuzaji ni yake, imesajiliwa kwa ID yake..
2. Omba kitambulisho, kipige picha kikiwa na simu, na pesa unayompa.
3. Piga naye Selfie/record video akiwa ameshika ID yake na makubaliano ya mauziamo..
4. Fanya biashara hio nyumbani/ofisini au basi uchukue namba ya mtu wake wa karibu, huyo mtu umtafte wewe..
Shtuka ukiona haya.
1. Muuzaji wa simu anasema ni yake lakini haitumii inasoma imergence.
2. Phone status inasoma Custom.
3. Muuzaji anakuambia exchange allowed lakini haweki conditions zozote na ukiangalia simu ni ya gharama.
4. Muuzaji ana namba za simu nyingi kupitiliza,
Nimepiga sana u winga, Nina scenario nyingi sana ambazo ziliniokoa.
YOTE HAYA YANAWEZA KUA MATESO,
NENDA SHOP YA KUELEWEKA ZAMA MFUKONI VIZURI, NUNUA KITU SEALED.
NOTE : SEALED na FULLBOX ni vitu viwili tofauti.