Kuna kipindi nilichalala sana, nilikua natumia simu niliyopewa na ofisi tu kama simu yangu binafsi. Mi simu yangu imefia kwa fundi wakati huo. Nikaona tangazo la simu used inauzwa nikatamani kuinunua.
Dogo anayeuza ananiambia yuko Magomeni. Nikachoma wese mpaka Magomeni, dogo akaja, ni pale Morocco karibu kabisa na Kanisa Katoliki. Nikaikagua simu iko vizuri, na sio ya mkopo, nikaridhika nayo. Dogo anasema simu ni ya dada yake. Tukapatana tena bei pale mambo yakawa mukide.
Kipengele kikaja, dogo hana ID. Na mahali tulipo sio sehemu official ni pembezoni tu mwa barabara. Nikamwambia dogo asiponipa ID sinunui simu. Dogo akasema ID hana ana namba ya NIDA ambayo hata hivyo, haikumbuki. Nikaingia NIDA web nikafanya mchakato nikapata NIDA namba yake. Nikaangalia namba ya simu tuliyowasiliana ina jina lake.
Dogo akaanza kupata wasi wasi huenda mimi ni pot. Akaghairi hauzi anaogopa isje kuwa mimi askari. Nikamtoa hofu, nikamwambia hii ni kwa usalama wangu. Just imagine dogo kazaliwa 2001, tukio la kwaka 2023.
Nikamlipa. Nikabeba simu. Sikupata usumbufu wowote.