Jinsi TFF ilivyoamua kumuonea hadharani Feitoto na kuwatumikia Yanga Ni dhahiri zile ni hisia za bahasha kwenye ligi yetu

Jinsi TFF ilivyoamua kumuonea hadharani Feitoto na kuwatumikia Yanga Ni dhahiri zile ni hisia za bahasha kwenye ligi yetu

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
1. Walianza na barua ya kingereza iliyomtoa uarabuni kwenye program zake wakitaka aje bila kubainisha makosa aliyoshitakiwa nayo ili awe tayari kuandaa utetezi wake. Barua ilikuwa fupi sana. Na kikubwa swala Hilo Feitoto angeweza kulijibu kwa maandishi tu bila kuwepo Sababu Ni la kimkataba. Lkn wanalazimisha arudi.

2. Wakaja na maamuzi yaliyo upande wa Yanga bila kushirikisha wapi Feitoto alikosea. Wakasema ufafanuzi Jana. Lkn maamuzi walishirikisha kwenye vyombo vya habari.

3. Jana hawakutoa ufafanuzi Bali Tuzo zilizoegemea Simba ili kuwazima washabiki wa Simba wanaofatilia swala la Feitoto.

Tff wanajua muda wa dirisha dogo Ni mfupi. Wanajua umuhimu wa uamuzi wa haraka kwa Feitoto kuliko Yanga. Dogo anatakiwa apate timu Kama akishinda. Kutotoa ufafanuzi tu baada ya masaa 72 baada ya hukumu kutolewa kunamyima fursa Feitoto kutafuta haki akiona ameonewa.

Hii Ni roho mbaya Kama sio ushetani. Toka hukumu ya Feitoto itolewe hakuna ata mwanasheria moja wa soka aliyeweza kuja kufafanua Ni vipengere vipi ambavyo vilimbana fei asivunje mkataba wake bila sababu wakati mkataba wake ulikuwa na vipengere hivyo.

Zaidi utasikia oh "mkataba hauvunjwi kihuni".

Fei aliweka kipengere Cha kuvunja mkataba bila Sababu kwa kulipa tsh m 100. (Nakumbusha bila Sababu) na mishahara mitatu.

Tulitegemea Tff ije iseme hakuna kipengere hicho kwenye mkataba wa Feitoto au itoe tafsiri ya hicho kipengere.

Kuvunja kwa Sababu zilizoanishwa na FIFA fei asingelipa chochote.. ikiwa Ni pamoja na kutolipwa mshahara au kukaa benchi 90% ya muda kwa mechi kumi bila sababu

Msitumie tuzo kwa Mgunda na Chama kuzima kimya kimya Swala la Feitoto.

Mliwapa muda kijanja Yanga wa kumrudisha bongo Feitoto ili wapate na gepu waongee nae. Nazani imeshindikana.

Ni muda Sasa wa swala lake kuwa wazi tu.
 
Fei ni mpumbavu , hata kama kuna upenyo huo wa kuvunja mkataba , ni kuwakosea Yanga , tujiulize Yanga wamemkosea nn Fesal? Kulikuwa na malumbano yoyote?

Kama kulikuwa hamna shida kulikuwa na haja gani ya kuwatoroka....ikumbukwe mpira ni biashara , mchezaji anapopanda thaman , na ikatokea timu ikamhitaji tunatarajia mchezaji kulipwa vizur timu atakayokwenda ( hii ni faida Kwa mchezaji) , na pia timu anayotoka ambayo kimsingi ndo imempandisha thamani na wenyewe wapate.

Sasa yeye anatoroka kupitia mlango wa nyuma , timu ibaki haina kitu , ni Ujinga mkubwa Sana huo , dogo hafai hata kidogo , na hili ni tatizo la elimu duni Kwa hawa vijana ,

Yalianzia kwenye mziki akina harmonize, Ray-vanny (yaan wanataka wachukue chote) na sasa yameanza kwenye mpira
 
Tff wanajua muda wa dirisha dogo Ni mfupi. Wanajua umuhimu wa uamuzi wa haraka kwa Feitoto kuliko Yanga. Dogo anatakiwa apate timu Kama akishinda. Kutotoa ufafanuzi tu baada ya masaa 72 baada ya hukumu kutolewa kunamyima fursa Feitoto kutafuta haki akiona ameonewa.
 
1. Walianza na barua ya kingereza iliyomtoa uarabuni kwenye program zake wakitaka aje bila kubainisha makosa aliyoshitakiwa nayo ili awe tayari kuandaa utetezi wake. Barua ilikuwa fupi sana. Na kikubwa swala Hilo Feitoto angeweza kulijibu kwa maandishi tu bila kuwepo Sababu Ni la kimkataba. Lkn wanalazimisha arudi.

2. Wakaja na maamuzi yaliyo upande wa Yanga bila kushirikisha wapi Feitoto alikosea. Wakasema ufafanuzi Jana. Lkn maamuzi walishirikisha kwenye vyombo vya habari.

3. Jana hawakutoa ufafanuzi Bali Tuzo zilizoegemea Simba ili kuwazima washabiki wa Simba wanaofatilia swala la Feitoto.

Tff wanajua muda wa dirisha dogo Ni mfupi. Wanajua umuhimu wa uamuzi wa haraka kwa Feitoto kuliko Yanga. Dogo anatakiwa apate timu Kama akishinda. Kutotoa ufafanuzi tu baada ya masaa 72 baada ya hukumu kutolewa kunamyima fursa Feitoto kutafuta haki akiona ameonewa.

Hii Ni roho mbaya Kama sio ushetani. Toka hukumu ya Feitoto itolewe hakuna ata mwanasheria moja wa soka aliyeweza kuja kufafanua Ni vipengere vipi ambavyo vilimbana fei asivunje mkataba wake bila sababu wakati mkataba wake ulikuwa na vipengere hivyo.

Zaidi utasikia oh "mkataba hauvunjwi kihuni".

Fei aliweka kipengere Cha kuvunja mkataba bila Sababu kwa kulipa tsh m 100. (Nakumbusha bila Sababu) na mishahara mitatu.

Tulitegemea Tff ije iseme hakuna kipengere hicho kwenye mkataba wa Feitoto au itoe tafsiri ya hicho kipengere.

Kuvunja kwa Sababu zilizoanishwa na FIFA fei asingelipa chochote.. ikiwa Ni pamoja na kutolipwa mshahara au kukaa benchi 90% ya muda kwa mechi kumi bila sababu

Msitumie tuzo kwa Mgunda na Chama kuzima kimya kimya Swala la Feitoto.

Mliwapa muda kijanja Yanga wa kumrudisha bongo Feitoto ili wapate na gepu waongee nae. Nazani imeshindikana.

Ni muda Sasa wa swala lake kuwa wazi tu.
Naanza kuamini zile zama za msemo kuwa wahaya ni shomile zimepita!!
 
1. Walianza na barua ya kingereza iliyomtoa uarabuni kwenye program zake wakitaka aje bila kubainisha makosa aliyoshitakiwa nayo...
Ndugu mwandishi tulia kwanza! Hivi nanni anaweza kukubali kuweka kipengere cha kuvunja mkataba bila sababu? Mbona mnafanya mambo kihisia nani hiyo?

Hakuna mkataba wa mchezaji yeyote Dunian ambao unakosa kipengere cha kiterminate mkataba kwa kila upande, ila lazima kuwe na sababu zitazopelekea kuvunjwa kwa mkataba uo! Msije mkadhan hiko kipengere kitatumika eti kwasababu kuna ofa nzuri umepata basi uamke ukavunje mkataba, usije ukadhan hicho kipengere kiko uchi namna hiyo!

Onyango kipindi Mgunda hajaingia Simba alikuwa anakosa namba, unakumbuka iliibuka tetesi hapa kutaka kuondoka? Unajua angeondokaje? Basi nakuambia moja ya kipengere hichohicho ndicho akitaka kukitumia kwasababu alikuwa hapangwi, ila Onyango alikaa na waajiri wake wakayamaliza ila sio utoto kama wa Feisal kuwa umelala umeamka asubh bas unaenda kuterminate mkataba! Hakuna uo mwanya aisee.

Mwisho Feisal ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba sio kwa mujibu wa hisia, Feisal atulize kitako atafute wanajua sheria aachane na washauri wabovu kama nyinyi mtampotosha na atapotea.
 
Tff wanajua muda wa dirisha dogo Ni mfupi. Wanajua umuhimu wa uamuzi wa haraka kwa Feitoto kuliko Yanga. Dogo anatakiwa apate timu Kama akishinda. Kutotoa ufafanuzi tu baada ya masaa 72 baada ya hukumu kutolewa kunamyima fursa Feitoto kutafuta haki akiona ameonewa.
Just imagine jana wangetoa ufafanuzi, embu niambie wakienda huko CAS wanaanza kusikilizwa mara moja? Au utaratibu ukoje?
 
Ndugu mwandishi tulia kwanza! Hivi nanni anaweza kukubali kuweka kipengere cha kuvunja mkataba bila sababu? Mbona mnafanya mambo kihisia nani hiyo...
Yeye fei aliweka. Uwenda Alijua thamani yake itakuwa na atataka kuondoka bila bugudha. Na Yanga wakasaini wakiwa na Akili timamu. Wachezaji wengi hawana kipengere hicho.

Kama taasisi Kama ilijua masharti hayo ilitakiwa kujiandaa kwa lolote. Na uwenda walitumia kipengere hicho kumshawishi asaini kwa dau dogo. Nazani wewe ndio unaweka hisia mi nachotaka Tff watoe ufafanuzi tuache hizi porojo
 
1. Walianza na barua ya kingereza iliyomtoa uarabuni kwenye program zake wakitaka aje bila kubainisha makosa aliyoshitakiwa nayo ili awe tayari kuandaa utetezi wake...
Ni uelewa wako mdogo wa mambo ya mikataba ni ufahamu wa majukumu ya kamati ndio unaokusumbua
 
Just imagine jana wangetoa ufafanuzi, embu niambie wakienda huko CAS wanaanza kusikilizwa mara moja? Au utaratibu ukoje?
Cas wakiwa wanasubiri kutoa hukumu kulingana na kesi huweza kumpa mchezaji Uhuru Hadi hukumu ili asiaribu kipawa chake. Na hili swala Ni jepesi Sana Ni la mkataba. Tff haioni pa kumbana fei
 
Yeye fei aliweka. Uwenda Alijua thamani yake itakuwa na atataka kuondoka bila bugudha. Na Yanga wakasaini wakiwa na Akili timamu. Wachezaji wengi hawana kipengere hicho...
Bado unahitaji kujifunza brother! Hicho kipengere kipo sio kwa mujibu wa Feisal, ila kipo kwa mujibu wa muongozo wa Fifa, Feisal labda angekuwa na akili kipindi anasaini uo mkataba 2020 angeweza kusema mshahara uongezeke kama atakuwa na perfomance nzuri na akatwe akiwa na perfomance mbovu!

Nakusisitiza tena kuwa kila mkataba unavunjika, ila kuwe na sababu maalumu ambazo zitapelekea mkataba uvunjike, sio uamke tu useme naenda kununua mkataba niondoke uo ni ujuha.

Na ukae ukijua kila upande una haki ya kuvunja mkataba, ata Yanga nao wanakipengere chao cha kuvunja mkataba katika ya msimu ila lazima kuwe na sababu ila nje ya hapo lazima biashara ifanyike mezani.
 
Cas wakiwa wanasubiri kutoa hukumu kulingana na kesi huweza kumpa mchezaji Uhuru Hadi hukumu ili asiaribu kipawa chake. Na hili swala Ni jepesi Sana Ni la mkataba. Tff haioni pa kumbana fei
Umelielewa swali langu? Nimeuliza japa wangetoa maelezo ya ziada it means wangeenda CAS sio? Huko CAS tuchukulie kesi ingepokelewa leo au kesho, Je! Wangeanza kusikilizwa leo au kesho hiyohiyo au unapewa Date?
 
Mimi sio shabiki wa Utopolo ila Feisal na hao wanaotaka kumsajiri wamezingua sana.! Hawa wachezaji wetu kutokua na elimu ya kutosha ni tatizo kubwa huwezi kuamka asubuhi tu huna tatizo lolote na timu yako kisa umepewa hela mlango wa nyuma ukavuje mkataba kihuni tu.!
 
Back
Top Bottom