SoC01 Jinsi vijana wanavyoweza kujifunza TEHAMA

SoC01 Jinsi vijana wanavyoweza kujifunza TEHAMA

Stories of Change - 2021 Competition

Emmanuel E Shirima

New Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
3
Reaction score
3
Habarini wana Jamii Forum ni matumaini yangu yote ni wazima.

Andiko langu linahusu jinsi TEHAMA inavyoweza kusaidia vijana katika kupanua uwelewa wao na kuweza kutumia ili wajipatie kipato.

Utangulizi:
Idara ya Teknolojgia na Mawasiliano imekuwa sehemu muhimu sana katika karne hii ya kisasa mambo mengi yameweza rahisishwa kwa kutumia TEHAMA katika nyanja mbali mbali kama vile kiuchumi, elimu, afya na sekta nyinginezo.

Kufikia 2035, inasemekana Afrika itakuwa kati ya bara lenye nguvu kazi kubwa Duniani. Hivyo kuwekeza katika kuwaelimisha vijana ni njia moja bora ya kuhakikisha nguvu kazi hiyo itatumika kwa manufaa ya kimaendeleo kwa taifa na bara la Afrika kiujumla. Mabadiliko ya kidigitali yanachangia ukuzi wa haraka sana katika nyanja za kiuchumi, ukuzi wa miundombinu ya kidigitali na pato la mtu moja moja. Vijana wanapaswa kuandaliwa ili waweze kukabiliana na mabadiliko hayo ya baadaye.

Changamoto:
Zifuatazo ni changamoto katika ukuzi huu wa TEHAMA hasa kwa vijana
  • Kukosa vifaa kama vile kompyuta, simu janja n.k
  • Kukosa elimu ya kutosha kuhusu mabadiliko ya kidigitali
  • Ukosekanaji wa wakufunzi wa kutosha katika sekta ya TEHAMA nchini

Kutokana na changamoto hizo mimi kama Mkufunzi niliyeajiriwa na Tasisi isiyo ya kiserikali itwayo “Camara Education Tanzania” nilianzisha Klabu za TEHAMA mashuleni lengo hasa likiwa ni kuwafikia vijana (wanafunzi) ambao ndo nguvu kazi ya taifa letu kwa kipindi kijacho. Dhumuni la kuunda klabu hizi mashuleni ni kuanda vijana kwa ajili ya mabadiliko ya kidigitali katika nyanja ya kibiashara na kisosholojia.

Kuanzia 2021, tumefanikiwa kuanzisha klabu Shule za sekondari 8 kama kufanya utafiti wa majaribio wa klabu hizo za TEHAMA kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Shule hizo 3 ziko jijini Dar es salaam na 5 ziko nje ya mkoa.
IMGL3607-2.jpg
IMG_1936.jpg
IMG_2705.jpg


Klabu huundwa kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi jinsi ya kuanzisha klabu, pia wanafunzi hupatiwa maudhui yote kwa ajili ya kujifunza kutia ndani kompyuta, nakala mbali mbali za kujifunzia, video na vitabu vya kujisomea. Mfumo ambao nimeunda unaweza tumika bila kutumia interneti na hii ili kuwezesha hata vijana ambao wako maeneo ya vijijini waweze kupata maudhui hayo na kueleimika katika maswala ya TEHAMA ili waendane na mabadiliko ya kidigitali.
Pia mfumo ambao nimetengeneza una video za kufundisha picha na mazoezi mbalimbali ambayo yanaweza mfanya kijana kutumia yale anayojifunza si kwa kusoma tu bali pia kwa vitendo kupitia mfumo huo wakujifunzia. Mfumo ambao nimeunda ni bure hauhitaji kulipia unachopaswa kufanya ni kujisajili na kuanza kujifunza mambo yaliyopo.
Mimi hutoa mafunzo kwa vitendo katika shule hizo za sekondari nikishirikiana na Camara Education Tanzania, ili vijana wenzangu waweze jifunza kwa vitendo. Nimeunda mijadala mbalimbali inayohusu TEHAMA kama jukwaa la vijana kulumbana kwa hoja katika njia ya kujifunza.
IMG_2211.jpg
IMG_2928.jpg


Hitimisho:
Kwanza ningependa kutoa shukurani kwa Camara Education Tanzania kwa kutambua uwezo wangu na kunipa fursa ya kuongoza Klabu hizi nchini Tanzania, pia nipende kutoa shukurani kwa shule, walimu na serikali ambao wamekuwa wadau wakubwa katika kuendesha na kuhakikisha klabu hizi zinaendelea kufanikiwa. Kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 lengo ni kufikia zaidi ya shule 500 nchi nzima, ningependa kutoa wito kwa vijana wenzangu ambao bado wako shuleni kutumia fursa hii kujifunza ili waweze kabiliana na mabadiliko ya kidigitali pia kujitengenezea kipato kupitia TEHAMA ambayo ni sekta inayokuw kwa kasi sana.

Nimefikia mwisho wa andiko langu. Natumaini mtakuwa mmenielewa japo nimejaribu kueleza kila kitu kwa uchache kutokana na kile nachofanya.

USIACHE KUNIPIGIA KURA ANDIKO HILI. ASANTE SANA
 
Upvote 2
Back
Top Bottom