PostGE2025 Jinsi Vyombo vya Usalama vilivyogeuza Ulinzi kuwa chanzo cha hofu

PostGE2025 Jinsi Vyombo vya Usalama vilivyogeuza Ulinzi kuwa chanzo cha hofu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

raiamwematz24

Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
8
Reaction score
21
Tangu yalipofanyika maandamano na baadaye vurugu wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 na baada ya hapo, kumekuwa na hofu kubwa kwa wananchi kutokana na kuongezwa kwa ulinzi wa polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Maandamano yaliyokabiliwa kwa nguvu na polisi na JWTZ yalisababisha mauaji, majeruhi na uharibifu wa mali.

Miezi miwili baadaye bado mpaka sasa askari wameonekana kuzagaa na kuimarisha ulinzi maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam jambo ambalo kwa wananchi imekuwa chanzo cha hofu na kudhani kuwa muda wowote wanaweza kuwa hatarini.
Screenshot 2026-02-04 183206.jpg

Picha ya AI​
Kwa wengi wao, kumuona askari barabarani hakukuashiria usalama wala udhibiti wa sheria, bali hatari inayoweza kubadilisha siku yao ghafla na kuwa mbaya.

Mmoja wa madereva wa pikipiki eneo la Kimara Baruti Dar es Salaam, alipoulizwa kuhusu hofu hiyo, amesema, “Hatukamatwi kama wavunjifu wa sheria za barabarani. Tunakamatwa kama wahalifu wakubwa.”

Waendesha bodaboda wengi walilalamika kuwa wanapokamatwa, hawapewi maelezo ya wazi ya kosa, badala yake, wanahisi kutishwa, kunyanyaswa, au kubebwa kwa nguvu kana kwamba wanahusika na uhalifu mkubwa.

Hali hii imejenga hofu ya kudumu na kwa baadhi yao, hata askari wa kawaida wa barabarani anaonekana kama mwanzo wa matatizo makubwa zaidi huku kukamatwa, kupoteza chombo cha kazi, au kuingia kwenye mlolongo mrefu wa kudaiwa kulipa malipo makubwa yasiyoeleweka.
Mbali na madereva hao, hata wananchi mitaani wameingiwa na hofu kila wanapokutana na maofisa usalama.

Mmoja wa Wananchi katika eneo la Mabibo Sokoni, Juma K. Juma amesema, “Hujui nani ni salama siku hizi, yani bora ukae tu kimya usije kuchukuliwa na watu wasiojulikana.”

Wananchi wengine waligoma kuzungumza chochote, huku wakiniambia kuwa hawajui nani anaweza kuwa mpelelezi, nani anaweza kuripoti maneno yao, au nani anaweza kuwasababishia matatizo.

Mwanamke mmoja wa Manzese maaarufu kwa jina la Mama Abdul amesema wananchi wengi wamekuwa waoga hata kuzungumza na majirani kwa hofu ya kufuatiliwa.
“Siku hizi unanyamaza hata nyumbani yani unaogopa hata ukimwambia jirani wako, kesho unapotezwa,” amesemna.

Wananchi wengi waliohojiwa hawakulalamikia ukosefu wa taarifa tu, bali kutokuwepo kwa taarifa zinazoaminika na zinazoendana na walichokiona kwa macho yao.

Baadhi ya wananchi walirejea kauli ya Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa wanaouliza au kukosoa mwenendo wa Dola, pamoja na kauli yake kwamba nguvu iliyotumika Oktoba 29 ilistahili.

Kauli hiyo aliyoisema katika mkutano wa wazee wa Dar es Salaam Desemba 2, 2025, ambapo alitoa kauli zenye tata ambazo zilizidi kuvunja imani ya wananchi kwa mamlakana husika.

Kauli hizo ni kama “Mnalia watoto wenu wameuawa kwa nini hamkuwazuia wasitoke? akaongeza kwa kusema, Serikali hii sio ya kuamrishwa wala kupewa maelekezo.”

Mpaka sasa Serikali haijatoa idadi kamili ya watu waliokufa wala kujeruhiwa wakati wa vurugu za uchaguzi, badala yake viongozi wametoa orodha ya mali zilizoharibiwa, zikiwamo ofisi, magari, vituo vya mafuta na vituo vya mabasi ya mwendo wa haraka.

Hatua hiyo imezua maswali kwamba Serikali inathamini vitu kuliko uhai wa watu?
Aidha, kauli kwamba nguvu iliyotumika Oktoba 29 ilikuwa sahihi na vifo kuwa sio halisi , iliwafanya wengi waamini kuwa hata wakikumbwa na ukatili au unyanyasaji, mfumo uko upande wa askari, si wao.

Mwanasheria mmoja wa haki za binadamu ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa Serikali inapojaribu kunyamazisha sauti za wananchi kwa kutumia mabavu inakiuka misingi ya kikatiba na kuvunja misingi ya demokrasia.

“Mamlaka inapokataa kusikiliza matakwa ya wananchi na kuondoa uwazi, inaua imani. Na imani ikifa, hata polisi mzuri ataonekana adui.

“Watu hawatoi taarifa za uhalifu kwa sababu hawajui nani ni salama kumuambia. Wanaogopa kuhusishwa na matatizo, wanaona askari si wasikilizaji bali wahukumu ambapo hali hii inaathiri moja kwa moja usalama wa jamii. Pale ambapo bodaboda, wafanyabiashara na wakazi wanaishi kwa hofu ya askari na hofu ya wenzao, usalama wa kweli hauwezi kujengwa,” amesema.

Ili kupunguza hofu na kurejesha imani kati ya wananchi na vyombo vya usalama, ameshauri mamlaka kujenga mawasiliano ya wazi na ya mara kwa mara kwa jamii, kutoa taarifa sahihi na zinazoeleweka kuhusu matukio na operesheni za usalama, pamoja na kuhakikisha matumizi ya nguvu yanazingatia sheria na uwajibikaji.

“Vyombo vya usalama vinapaswa kuimarisha mfumo wa polisi jamii, kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa uwazi bila kulipiza kisasi, na kuwachukulia raia hususan makundi kama waendesha bodaboda kama washirika wa usalama badala ya wahalifu,” amesema

20251225_122549.jpg
 
Msianze kutafuta sijui watendaji,wakurugenzi, walimu sijui kina nani, hao wote wanapewa maelekezo na wanatakiwa kutekeleza na wala sio kuhoji au kukataa, na hayo yote Yatolewa na waziri,mkuu wa mkoa na wilaya wakiwa na viongozi wa usalama wenye mitutu na vitisho vya kila aina.

Jiulize tu jepesi kama tundu lisu na umaarufu wake wote ndani na nje ya nchi lakini mwaka sasa yupo gerezani kwa kesi isiyo eleweka, na je? Hamprey polepole ambaye amesha wahi kuwa kiongozi wajuu kabisa wa CCM na bado akawa balozi kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi lakini naye hajulikani alipo hadi sasa

Sasa je? Vipi kwa mtendaji wa kijiji au kata yeye ni nani hadi apate nguvu ya kugomea maelekezo anayo pewa mbele ya mitutu, mwalimu ni nani hata aweze kugomea maelekezo anayo pewa akiwa kashikiwa mitutu?

Kuna mambo huhitaji akili kubwa au CHADEMA wakulishe maneno unatafakari mwenyewe kwa kina un apata majawabu, utumishini huku ukionesha vimelea tu vya kupingana na msimamo wa Chama na serikali basi utakuwa katika hali mbaya sana na unahatarisha kazi na maisha yako kwa ujumla,

Huwa mnauliza Ooh! Kwa nini wasikatae! Maelekezo, hivi kwa mazingira ya nchi hii na mifumo yake ilivyo unaweza ukakataa maagizo unayo pewa na serikali ? Bila kujali ni ya wazi au ya siri? utayakataa kweli na ukabaki salama? Nani asiye penda kuishi ?

Ni bora basi hata hao unao jitoa kwao kuwatetea wawe wanateteeka, matokeo yake mwisho wa siku wanakuacha pekeyako wao wapo busy kuwafutilia kina Diamondi na zuchu na harmonize na kajala mitandaoni na kubishana kuhusu simba na yanga, hawana mda na wewe mtetezi wao pale unapo sulubishwa, kama ilivyo kwa lisu na wengineo kwa sasa.

Kwa lisu hata idadi tu ya wananchi wanao enda kusikiliza hiyo kesi imepungua sana wakati alipo kuwa akiongea maelfu walikuwa nyuma yake, hii inamana gani?

Msiwalaumu watumushi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya serikali hii ya CCM, hasa haya yenye maelekezo kutoka vyombo vya dola kama UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUPIGA KURA, UCHAGUZI na mengineyo yafananayo, mtawaonea bure hawana cha kufanya au kubadilisha hasa kwa mustakabali wa ajira zao na maisha na uhai wao.

Mwaka jana kuna vijana walikuwa wapiga kelele sana mitaani Oooh! Watendaji waizi wa kura, Oooh! Walimu wezi wa kura . Sasa wakapata shavu la kusimamia uchaguzi na wao ,matokeo yake wameyafanya yake yale waliyo kuwa wanatuhumu wenzao na wameona na kujifunza ugumu uliopo hasa yanapo toka maelekezo fanya hiki ,fanya kile, na wakashindwa hata kukataa, wakafanya kwa nguvu kabisa na walipo maliza zoezi wametoka kushuhudia kwamba kumbe tuna walaumu bure watumishi na wao sio wao hakuna namna ya kubisha hasa kama unapenda kuishi'

Hivyo wale waonao laumu watumishi nawashauri zinapo tokea kazi hizi ombeni mkafanye na nyie halafu wengine wajifunze kwenu jinsi ya kugomea maelekezo ya serikali hii ya CCM na ukabaki salama.

Idara pekee yenye uwezo wa kufanya nchi hii itawalike na rasilimali zake ziwe na faida kwa wananchi wake na sio watu wachache kama ilivyo hivi sasa ni
VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA TU.na kwakuwa vyombo hivi vyooote vimeamua kuacha uzalendo kwa taifa na kuamua kuwa wazalendo kwa watu na watawala pekee basi itoshe kusema kwamba kwa sasa watanganyika hawa wamebaki pekeyao na wakidai haki zao ya oktoba 19 2025 yatakuwa yanajirudia mara kwa mara maana hawana tena wakusimama nao wamesalitiwa na kila mwenye jukumu la kuwatetea na kutetea taifa lao kilicho baki kwao kwa sasa nikufurahia tu pale, kiongozi wa serikali anapo kufa ua kupatwa na baya, maana wamesha jikatia tamaa hawana wakuwabeba wala kuwashika na kutembea nao wala kusikiliza mahitaji yao l.
 
Tanzania tunahitaji ukombozi wa kweli!
Screenshot_20251129-214516~2.png
 
Back
Top Bottom