Jinsi Wakenya wanavyotajirika na pumba za karanga za Tanzania

Jinsi Wakenya wanavyotajirika na pumba za karanga za Tanzania

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
34,962
Reaction score
70,576
Hii ni kwa wale wanaopenda maisha bora!

Hawa Wakenya jamani mimi kila week nawaona huku; wanakuja na gari wanasomba pumba nyingi kweli kweli wanapeleka kwao, lakini nimejaribu kuwahoji wanaishia kuniambia endeleeni kulialia tu😭...! Wanatudharau sana pia!

Pia, wanachukua karanga kwa wingi sana wanaenda nazo Kenya. Hivi shida yetu ni nini jamani kama nchi? Moyo unauma, wapi tunakosea? Yaani hapa naandika nipo nao hapa wanapakia hii mizigo!

Nadhani pumba ni kwaajili ya ceiling board, au kuna mishe nyingine? Na hizi karanga ndiyo wanaongeza thamani au?

Kama vipi tuchangamkie fursa hii jamani. Watanzania mliopo kwa "Uhuru" hebu semeni neno basi!

Kwenye karanga ndiyo pamenigusa. That wananunua karanga kwa shilingi 5000 kwa debe. Eh bwana eh! Nimechoka mimi kwanza.
 
Jaribu kufikiri kwa upana wako na kuangalia biashara ambayo unaweza kufanya na siyo kuchungulia ambayo unaona mwenzako anafanya na unaona kama vile unapatia sana.

Kwa Kenya pumba inatumika sana maana kuna wafugaji wengi sana wa kuku kulinganisha na TZ na kuna hata Wamarekani wamewekeza kwenye kuku, so pumba inatumika kutengeneza chakula cha kuku na hawajaanza leo ni tangia miaka ya 1990s.

Kuhusu karanga, sina uhakika sana na hiyo bei uliyoitaja maana hata kwa Dar huwezi pata kwa hiyo bei.

Biashara hasa hizi za mazao kama karanga na pumba zikipata mnunuzi hasa wa nje ni nzuri maana wanatuletea hela na kupandisha thamani ya mazao yetu.

Wakenya wananunua maparachichi, maharage, maembe na mahindi kwa wingi sana hasa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na wilaya ya Tarime.
 
Yote ina faida, auze Mtanzania au anunue Mkenya. Labda ungeniambia tuwe na semi-processed manufacturing ili kuongeza value. Hapo inakua na faida mara mbili manake pia unakuwa umetengeneza ajira kwa watu wetu.

Lakini we mzalendo nimekukubali; ni lazima rasilimali zetu zitunufaishe, inabidi nikutafute sasa tufanye biashara ya karanga au siyo?
Unamis point yangu bwana[emoji1787]...ww hebu fikiria kwann isingekuwa mtzed anasafirisha haya mazao??lols..huenda kun ukweli
 
Jaribu kufikiri kwa upana wako na kuangalia biashara ambayo unaweza kufanya na siyo kuchungulia ambayo unaona mwenzako anafanya na unaona kama vile unapatia sana.Kwa Kenya pumba inatumika sana maana kuna wafugaji wengi sana wa kuku kulinganisha na TZ na kuna hata wamarekani wamewekeza kwenye kuku so Pumba inatumika kutengeneza chakula cha kuku na hawajaanza leo ni tangia miaka ya 1990s.
Kuhusu karanga sina uhakika sana na hiyo bei uliyoitaja maana hata kwa Dar huwezi pata kwa hiyo bei.


Biashara haza hizi za mazao kama karanga na pumba zikipata mnunuzi hasa wa nje ni nzuri maana wanatuletea hela na kupandisha thamani ya mazao yetu.
Wakenya wananunua maparachichi,maharage,maembe na mahindi kwa wingi sana hasa mikoa ya Kilimanjaro Arusha na wilaya ya Tarime



Karanga niliyosemea hapa ni ya maganda. Ohh! Asante kunifumbua macho, mkuu.
 
Yote ina faida auze mtanzania au anunue mkenya.labda ungeniambia tuwe na semi processed manufacturing. Ili kuongeza value hapo inakua na faida mara mbili manake pia unakuwa umetengeneza ajira kwa watu wetu.lakini we mzalendo nimekukubali ni lazima rasilimali zetu zitunufaishe.inabidi nikutafute sasa tufanye biashara ya karanga au siyo.



Tumeshindwa kuwa na kiwanda cha kuprocess tomato zaidi ya kile cha iringa sembuse cha karanga mkuu?bdw mm sio mzalendo hata!
 
Hawa watu wana kiwanda cha uwongo, leo mnazusha hili kesho hili.

Karanga debe elfu tano ilikuwa mwaka 2001.

Wacha porojo.
 
Back
Top Bottom