Jinsi Wakenya wanavyotajirika na pumba za karanga za Tanzania

Pumba wanatumia kutengeneza chakula cha kuku. Nafikiri watakuwa wana miradi mikubwa ya kuku huko kwao.

Kuna mikate yao fulani hivi mitamuu huwa inaharibika haraka sana. Wakikuletea kama leo, after 3 au 4 days wanakuletea tena mingine kwakuwa ile ya mwanzo inakuwa imefikia expiring date.

Wanakupa mipya then ile iloharibika(kama ulikuwa haujaiuza) wanachukua. Siku moja ikabidi niwaulize, wakanieleza inakwenda kutumika kutengenezea chakula cha kuku.
 
Hii ni kwa wale wanaopenda maisha bora!
Hawa Wakenya jamani mimi kila week nawaona huku..wanakuja na gari wanasomba pumba nyingi kweli kweli...wanapeleka kwao..lakini nimejaribu kuwahoji wanaishia kuniambia endeleeni kulia lia tu[emoji24]...!wanatudharau sn pia ..!

pia wanachukua karanga kwa wingi sana wanaenda nazo Kenya hivi shida yetu ni nini jamani kama nchi?? Moyo unauma ...wapi tunakosea?yaan hapa naandika niko nao hapa wanapakia hii mizigo ...!

Nadhani pumba ni kwaajili ya ceiling board..au kuna mishe nyingine?na hiz karanga ndo wanaongeza thamani au?

Kama vipi tuchangamkie fursa hii jaman..watanzania mliopo kwa "Uhuru" hebu semeni neno basi!..
°Kwenye karanga ndo pamenigusa! That wananunua karanga kwa shilingi 5000 kwa debe ..!ah bwana eh nimechoka mm kwanza!
Hiyo tsh 5000 kwa debe sijaielewa,ni zilizomenywa au ambazo hazijamenywa
 
Jaribu kufikiri kwa upana wako na kuangalia biashara ambayo unaweza kufanya na siyo kuchungulia ambayo unaona mwenzako anafanya na unaona kama vile unapatia sana.Kwa Kenya pumba inatumika sana maana kuna wafugaji wengi sana wa kuku kulinganisha na TZ na kuna hata wamarekani wamewekeza kwenye kuku so Pumba inatumika kutengeneza chakula cha kuku na hawajaanza leo ni tangia miaka ya 1990s.
Kuhusu karanga sina uhakika sana na hiyo bei uliyoitaja maana hata kwa Dar huwezi pata kwa hiyo bei.

Biashara haza hizi za mazao kama karanga na pumba zikipata mnunuzi hasa wa nje ni nzuri maana wanatuletea hela na kupandisha thamani ya mazao yetu.
Wakenya wananunua maparachichi,maharage,maembe na mahindi kwa wingi sana hasa mikoa ya Kilimanjaro Arusha na wilaya ya Tarime
Kweli maparachichi wananunua sana, na wanadai maparachichi ya Kilimanjaro(haswa yale ya kienyeji) ni matamu sana na yana soko kubwa Kenya.
 
wewe binafsi pengine na wenzio ni zao gan haswaa umeadd value kama usemavyo
Mimi sipo upande huu, kuna vitu vingine nafanya mbali na hivyo japo yawezekana nikafanya huko mbeleni. ila kwa hao wenzangu kwa kuwa umeuliza ni hivi " wanafanya research kwenye masoko ambayo yapo profitable, kuanzia supermarket hadi nchi za nje (nchi jirani pamoja na zilizo nje ya Afrika), wanaangalia bidhaa gani za kilimo inahitajika na kwa ubora upi then wanalima wenyewe au kuwashauri na kuwapa wakulima zana ili wawazilishie kwa ubora wanaoutaka. Kinachofuata ni kuifanyia packaging then wanaziuza"....

Nimeongelea short and simple lakini bado kuna changamoto zao.. ukitaka kujua zaidi ingia field watafute wakulima kile commercial halafu fanya mawasiliano nao watakueleza. Siri ya kwanza ndio hiyo kujua soko linataka nini na ndipo wenzetu wametuzidi
 
Sasa kupata koneksheni na hao wakulima inakuwaje mkuu?
 
Mara nyingi hupatikana kwenye maonesho mfano wa wale wenye mabanda labda sabasaba au nanenane, wengine kwenye hafla za kibiashara au njia nyingineyo ni kuingia field, unakutana labda na wazalishaji wadogo wadogo then wao watakupa picha nzima ya soko linavyoendeshwa (hii sio rahisi mara nyingine maana inategemea na huyo mtu utakayekutana nae, wengine hawakupi picha nzima ili wakupige pesa directly ila ukienda nao taratibu watakueleza )..
 
Kila mtanzania anawaza kuuza duka la nguo au vipodozi, au afungue restaurant au anunue bajaji wakati mkenya na mnyarwanda wanaingia tabora kuchukua asali wanaenda kwao wanaisafisha then wanapack na kwenda kupiga pesa uarabuni hasa saudia na dubai
Watz hamuwezi kutoa ushauri mpaka mtunange? sisi tumeona Nguo haya wewe Umeona nini au na wewe unapeleka pumba na karanga Kenya?
 
Jaribu kufikiri kwa upana wako na kuangalia biashara ambayo unaweza kufanya na siyo kuchungulia ambayo unaona mwenzako anafanya na unaona kama vile unapatia sana.Kwa Kenya pumba inatumika sana maana kuna wafugaji wengi sana wa kuku kulinganisha na TZ na kuna hata wamarekani wamewekeza kwenye kuku so Pumba inatumika kutengeneza chakula cha kuku na hawajaanza leo ni tangia miaka ya 1990s.
Kuhusu karanga sina uhakika sana na hiyo bei uliyoitaja maana hata kwa Dar huwezi pata kwa hiyo bei.

Biashara haza hizi za mazao kama karanga na pumba zikipata mnunuzi hasa wa nje ni nzuri maana wanatuletea hela na kupandisha thamani ya mazao yetu.
Wakenya wananunua maparachichi,maharage,maembe na mahindi kwa wingi sana hasa mikoa ya Kilimanjaro Arusha na wilaya ya Tarime
kwetu mbeya pumba laini yampunga gunia elf kumi waambie hao wakenya
 
Hii ni kwa wale wanaopenda maisha bora!

Hawa Wakenya jamani mimi kila week nawaona huku; wanakuja na gari wanasomba pumba nyingi kweli kweli wanapeleka kwao, lakini nimejaribu kuwahoji wanaishia kuniambia endeleeni kulialia tu[emoji24]...! Wanatudharau sana pia!

Pia, wanachukua karanga kwa wingi sana wanaenda nazo Kenya. Hivi shida yetu ni nini jamani kama nchi? Moyo unauma, wapi tunakosea? Yaani hapa naandika nipo nao hapa wanapakia hii mizigo!

Nadhani pumba ni kwaajili ya ceiling board, au kuna mishe nyingine? Na hizi karanga ndiyo wanaongeza thamani au?

Kama vipi tuchangamkie fursa hii jamani. Watanzania mliopo kwa "Uhuru" hebu semeni neno basi!

Kwenye karanga ndiyo pamenigusa. That wananunua karanga kwa shilingi 5000 kwa debe. Eh bwana eh! Nimechoka mimi kwanza.
Nlidhan unaleta facts kumbe speculation...kila kitu unadhani tu
 
Kweli maparachichi wananunua sana, na wanadai maparachichi ya Kilimanjaro(haswa yale ya kienyeji) ni matamu sana na yana soko kubwa Kenya.
Ni kweli mkuu kuna siku nilikua kilimanjaro kule KYUU machame nikakuta fuso inapakia viroba vya parachichi balaaa
 
Unamis point yangu bwana🤣...ww hebu fikiria kwann isingekuwa mtzed anasafirisha haya mazao??lols..huenda kun ukweli
Jamaa alivyokujibu ndiyo jinsi watanzania wengi tulivyo. Hajui wale jamaa wakinunua wana add value kisha wanauza kwa bei kubwa huku mkulima Tanzania akiendelea kulia umasikini. Mimi najiuliza kwa nini wizara ya mambo ya nje wakishirikiana na kilimo na hii ya biashara wasizunguke kuangalia masoko yakoje na yanahitaji nini huko nje. Balozi zetu sehemu mbalimbali zinakuwa na kazi gani zenye tija kwa nchi. Nakumbuka kipindi marehemu Samwel Sitta akiwa hai alihojiwa akasema Sudani ya Kusini kuna soko kubwa watanzania changamkieni fursa,nikajiuliza mkulima wa Namtumbo hiyo taarifa inamtosha kupeleka zao lake Juba.
 
Ww umeuelezea huu uzi nilivyotaka watu wanielewe nnamaanish nn..asante sn mkuu...!mi lengo kuu ilikua watz wenye mitaji wachngmkie fursa wapeleleze hii ishu inakuwaje mapema iwezekanavyo..iweje mkenya aje achukue pumba jmn..!
 
Kila mtanzania anawaza kuuza duka la nguo au vipodozi, au afungue restaurant au anunue bajaji wakati mkenya na mnyarwanda wanaingia tabora kuchukua asali wanaenda kwao wanaisafisha then wanapack na kwenda kupiga pesa uarabuni hasa saudia na dubai
Hiii idea ninayo mtaji ninao sema starting point sijapata... system
 
Back
Top Bottom