Jinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita

Jinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita

Mawakili wote wana ripoti nzima ya kesi toka polisi, hivyo maswali mengi yanatokana na hoja za polisi kwenye faili lao.
Hapo polisi kwenye hizo ripoti zao lazima waruke sehemu zinazowagusa ambayo ndo hayo maswali mashahidi wanajichanganya
 
Kama fact moja kuwa pamoja na kuwa hawakujua tarehe za matukio ya ulipuaji vituo vya mafuta na masoko - bado polisi angalau katika mikoa husika hawakutoa tahadhari kwa umma wala vituo vya mafuta!! Toka taarifa ya kwanza mpaka sasa hakuna angalizo kutoka polisi. Jambo zima lilichukuliwa kama wanakifahamu - kwa hakika walichofahamu ni kwamba kusingekuwa na ulipuaji huo!!

Maelekezo ya msingi aliyopewa shahidi namba moko ni kuhakikisha hiyo mipango haifanikiwi lakini wakati huo huo kuona mtuhumiwa ana nia hiyo kweli? Kwa mfano ikitokea hao makomandoo Mbowe alitafutiwa na yule Mwanajeshi aliye toa taarifa na akaombwa kuendelea kutoa ushirikiano utasema nini tena? Kumbuka wako mashahidi 24.
 
Serikali hawatakubali tena kudhali lishwa Kwenye mitandao kiasi hiki najua wiki ijayo watazuia Kwa nguvu zote watu wasiripoti LIVE....
ni aibu kubwa Sana hii ni Bora hii kesi waachane nayo kuliko kujipaka kinyesi namna hii
 
Kama fact moja kuwa pamoja na kuwa hawakujua tarehe za matukio ya ulipuaji vituo vya mafuta na masoko - bado polisi angalau katika mikoa husika hawakutoa tahadhari kwa umma wala vituo vya mafuta!! Toka taarifa ya kwanza mpaka sasa hakuna angalizo kutoka polisi. Jambo zima lilichukuliwa kama wanakifahamu - kwa hakika walichofahamu ni kwamba kusingekuwa na ulipuaji huo!!

Kuna vitu vinne:
1: Kuna maelezo kutoka kwenye andiko la hati ya mashitaka/polisi.
2: Kuna maelezo ya shahidi husika/mahakamani.
3: Maelezo ya shahidi mmoja kwenda mwingine kwenye tukio moja.
4: Kuna maelezo ya mshitakiwa kwa wakili wake kwa anachokifahamu.

Ndo maana utasikia, huku mlisema risasi moja huku tatu au tuliwakamata wanakunywa supu vs wanatembea.


Unatengeneza sausages.
 
Supu, Ndizi , gari moja, kusafiri nao makilomita kibao, labda kama hao makomandoo sio wale wa akina bruce Lee, check noris and Van dame, halafu wakatembea nao bila pingu wala nini, halafu leo tuamini kwamba ni kama vile wao ni Hamza, hapana kwa kweli, kazi bado wanayo hao watu wa serikali...
Polisi imeamua kutengeneza Sinema ya kudharirisha Makomandoo wa JWTZ. Polisi huwa wanatafuta sana nafasi kuwadharirisha JW, wanafikia kutengeneza maelezo ambayo inafikia mahali mtu anajisemea kama Jeshi lenyewe ni hili basi nchi haipo salama.
Makomando wanakua arrested na Kingai bila ya msaada wa Jeshi!? Yaani Kingai na kikosi chake cha watu watano wanajipanga kwenda kukamata Makomandoo watatu wa Jeshi.
 
Jinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita.

MATATA: Nikumbushe Majina yako.

SHAHIDI: Naitwa Inspector Mahita Omary Mahita.

MATATA: nitakuwa Sahihi nikisema wewe ni Mtoto wa IGP mstaafu Omary Mahita.

SHAHIDI: Upo sahihi

MATATA: Wakati Baba yako akiwa IGP wewe Ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa Chuo kikuu

MATATA: Wakati Baba yako akiwa IGP ulikuwa na akili timamu?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Unakumbuka madai ya baba yako kuwakuta CUF na visu akadai wamekusudia kufanya ugaidi.

WAKILI WA JAMHURI: Objection Mheshimiwa Jaji. Naomba swali hilo liondolewe.

MATATA: Wakati mnawakamata watuhumiwa mlikuwa na Kikosi Maalum?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Kikosi chote kilitokea Arusha?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Na kikosi hicho kilikuwa chini ya RPC Kingai ambaye wakati huo alikua RCO Arusha?

SHAHIDI: Sahihi kabisa

MATATA: Unapotoka kwenye kituo unapaswa kuwa na Movement Order?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Ulipotoka Arusha kwenda Moshi hukueleza kuwa na movement order.

SHAHIDI: Nilikua nayo.

MATATA: Ulimweleza nani?

SHAHIDI: Sikueleza lakini nilikua nayo

MATATA: Maelezo yako ya awali hayaelezi hivyo.

SHAHIDI: Kimya.

MATATA: Je unajua kwamba unapofika mkoa mwingine unapaswa uriporti kwanza kwa Mlmamlaka za Mkoa huo?

SHAHIDI: Ni kweli.

MATATA: Katika maelezo yako hakuna popote uliposema umeripoti kwa mamlaka za polisi Moshi.

SHAHIDI: Ni kweli lakini?

MATATA: Hakuna lakini, jibu NDIYO au HAPANA.

SHAHIDI: Niliripoti lakini labda kwenye maelezo nilisahau kuandika.

MATATA: sasa kama hukuandika ulitegemea mahakama iote?

SHAHIDI: Kimya

MATATA: Una ushahidi wowote unaoonesha mliripoti mamlaka za polisi Moshi kabla ya operesheni yenu?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Uko wapi?

SHAHIDI: sijaja nao

MATATA: mlipowakamata watuhumiwa mliwasafirisha kuja Dar?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: walipofika Dar mliwatoa central na kuwapeleka Mbweni?

SHAHIDI: Ni kweli.

MATATA: Kwanini mliwapeleka Mbweni?

SHAHIDI: Kwa sababu ya usalama.

MATATA: Kati ya Cetral na Mbweni wapi kuna usalama zaidi?

SHAHIDI: Lakini..

MATATA: Jibu, acha lakini.

SHAHIDI: Mbweni.

MATATA: Kati ya Central na Mbweni wapi kuna askari wengi?

SHAHIDI: Central.

MATATA: Kati ya central na Mbweni wapi kuna silaha nyingi zaidi?

SHAHIDI: Central.

MATATA: Kati ya central na Mbweni wapi panaweza kupatikana msaada wa haraka ikitokea dharura?

SHAHIDI: Central.

MATATA: Sasa unasemaje Mbweni kuna usalama kuliko central?

SHAHIDI: ili watuhumiwa wasiweze kutoroka.

MATATA: Umewahi kusikia pale central kuna watuhumiwa wametoroka?

SHAHIDI: kimya

MATATA: Jibu swali, umewahi kusikia watuhumiwa kutoroka central?

SHAHIDI: wangeweza kutoroka.

JAJI: Mbona swali rahisi, jibu kama umeshawahi kusikia wametoroka?

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji mimi sijui.

MATATA: Kwanini mliwapeleka watuhumiwa Mbweni?

SHAHIDI: Ni kwa maelekezo ya viongozi wangu.

MATATA: Nakuuliza wewe, sio viongozi wako.

SHAHIDI: Kama nilivyosema ni sababu za kiusalama.

MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba mlipowaleta watuhumiwa Dar hujasema mliripoti kwa nani?

SHAHIDI: Tuliripoti kwa mamlaka za polisi kanda maalumu na mkoa wa kipolisi Kinondoni.

MATATA: Kwenye taarifa yako kuna mahali umeeleza hayo?

SHAHIDI: Hapana.

MATATA: Unaelewa kabla ya kuwasachi watuhumiwa, ilibidi nyie mlisachiwe kwanza?
shahidi ni kweli sijazungumza hilo.

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Lakini kwenye maelezo yako hujaeleza ka mlisachiwa kwanza kabla ya kuwasachi watuhumiwa.

SHAHIDI: Tulisachiwa japo sijaeleza.

MATATA: Kwa kuwa hujaeleza nitakosea nikisema hamkusachiwa.

SHAHIDI: Kimya.

MATATA: Umeeeleza kuwa watuhumiwa ni Makomandoo wa JWTZ?

SHAHIDI: Ni kweli.

MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba Makomandoo ni watu ambao wanahitaji ulinzi zaidi?

SHAHIDI: Sahihi.

MATATA: Lakini katika maelezo yako hakuna popote umesema mliwasifirisha kwa pingu? Je utakubaliana na mimi nikisema mliwasafirisha makomandoo wa jeshi kizembe bila kuwafunga pingu?

SHAHIDI: Tuliwafunga

MATATA: Lakini maelezo yako uliyoandika hayaelezi hivyo.

SHAHIDI: Itakua nilisahau tu.

MATATA: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.!

Malisa GJ

View attachment 1942312
Wakili mjinga Sana hayo ya babake yatamsaidia nini mbowe kutolewa jera

USSR
 
Supu, Ndizi , gari moja, kusafiri nao makilomita kibao, labda kama hao makomandoo sio wale wa akina bruce Lee, check noris and Van dame, halafu wakatembea nao bila pingu wala nini, halafu leo tuamini kwamba ni kama vile wao ni Hamza, hapana kwa kweli, kazi bado wanayo hao watu wa serikali...
Duu mkuu umenikumbusha Check Noris mtu mbaayaaaaa
 
[/QUOTE]
Wakili mjinga Sana hayo ya babake yatamsaidia nini mbowe kutolewa jera

USSR

Yanakuvuruga na kukupoteza mazima kama ni mwepesi ku-panic.
Wanasheria wanajua implication yake.
 
Hat
Unamnunulia supu na Mo energy [emoji23][emoji23][emoji23]
Hata wewe Idawa ni Gaidi Tena mbaya sana.. huwezi kuleta Riwaya Tangu April 2015 Jpm hajawaza Kuwa Rais mpaka Leo katangulia Tena Muhula Wa Pili hujaimalizia... Sasa tukikutia Mikononi hakuna Cha Supu Wala Mo Energy... Ni pingu mikono na Miguu virungu vya Kutosha na Miti ya fagio.... We subiri utaona
 
Hat
Hata wewe Idawa ni Gaidi Tena mbaya sana.. huwezi kuleta Riwaya Tangu April 2015 Jpm hajawaza Kuwa Rais mpaka Leo katangulia Tena Muhula Wa Pili hujaimalizia... Sasa tukikutia Mikononi hakuna Cha Supu Wala Mo Energy... Ni pingu mikono na Miguu virungu vya Kutosha na Miti ya fagio.... We subiri utaona
Duh! Mzee Ngoja niingie maktaba.[emoji120]
 
Back
Top Bottom