Jinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita

Jinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita

Cross examination questions ya upande wa utetezi zinalenga kuu - expose UONGO na HILA na UJINGA wa upande wa waandaa mashitaka haya...!

Hebu jaribu kufanya catch up hapa...

Kwamba, katika maswali yote ambayo ndiyo ya msingi kutetea UKWELI WA MASHITAKA yao, majibu yake yanakuwa kati ya haya;

å Kimya au;

å Ni/tulisahau ila upo/ipo/kipo au tulifanya ila sikuandika, au;

å Sikumbuki/nimesahau, au;

å Bahati mbaya zaidi kwa jinsi hawa jamaa wakivyo WAJINGA eti mpaka mahakamani wanathubutu kusema kauli zile za kijinga za siku zote wanapoonea na kunyanyasa wasio na hatia za;

"....niliagizwa na wakubwa wangu au yalikuwa maagizo toka juu..."

##This is very pathetic and stupid police force administration...!!!!
Ni rahisi sana kuzibomoa kesi za kubumba
 
Maswali yote ya huyu wakili ni ya kijinga kabisa tena yamepitwa na wakati na ni irrelevant kabisa hayana uhusiano wowote na fact in issue na sijajua ni kwa nini jaji alikuwa anaruhusu maswali utopolo baba wa shahidi ana uhusiano gani na ushahidi? Haya ma cross examinations wanajaza tuu fail la mahakama mapumba matupu.
Mbona umeumia sana ndg? Kazi za watu hizo na vile tunda sawa na mti
 
Maswali yote ya huyu wakili ni ya kijinga kabisa tena yamepitwa na wakati na ni irrelevant kabisa hayana uhusiano wowote na fact in issue na sijajua ni kwa nini jaji alikuwa anaruhusu maswali utopolo baba wa shahidi ana uhusiano gani na ushahidi? Haya ma cross examinations wanajaza tuu fail la mahakama mapumba matupu.
Mkuu, kama hujui mambo kaa kimya
 
Ila hukumu ikitolewa tuwe tunashangilia hivi hivi kwa kujikumbusha zaidi naomba mkasome kitabu cha kesi ya uhaini sehemu ya 1&2 jinsi kesi ilivyoendeshwa mpaka hukumu ilivyotolewa
 
Polisi imeamua kutengeneza Sinema ya kudharirisha Makomandoo wa JWTZ. Polisi huwa wanatafuta sana nafasi kuwadharirisha JW, wanafikia kutengeneza maelezo ambayo inafikia mahali mtu anajisemea kama Jeshi lenyewe ni hili basi nchi haipo salama.
Makomando wanakua arrested na Kingai bila ya msaada wa Jeshi!? Yaani Kingai na kikosi chake cha watu watano wanajipanga kwenda kukamata Makomandoo watatu wa Jeshi.
Inafikirisha sana!
 
Inafikurisha sana!
 
Hv sasa ndy vituko vya nchi yenu
Yaani policcm iwakamate makomando wa jwtz kama mateja wa tandale?
Chaajabu zaidi eti hata hawakuwafunga pingu!
 
Wewe ndyo mjinga,njia rahisi ya kugundua kama mtu anatoa ushahidi wa uongo ni kumtoa kwenye topic then unamrudisha tena.Kama ushahidi wake ni wauongo lazima kuna baadhi ya maeneo atasahau!
Haya maswali ya hivyo yalishapigwa chini na mahakama nyingi enzi zile mawakili.wa.zamani.wanauliza umevaa viatu vya rangi gani. Nashangaa vijana wa sasa bado wanauliza maswali hayo ya kijinga na shahidi mwenyewe naye anajibu?
 
Ila hukumu ikitolewa tuwe tunashangilia hivi hivi kwa kujikumbusha zaidi naomba mkasome kitabu cha kesi ya uhaini sehemu ya 1&2 jinsi kesi ilivyoendeshwa mpaka hukumu ilivyotolewa

Watu wanaongelea contents za mwenendo wa kesi. Hukumu itabaki kuwa hukumu, haitazuia contents zilivyotolewa. Ndio maana kwa kesi hiyo hiyo na contents zake watu hukata rufaa na kupata majibu tofauti. Hivyo, hukumu mwachie hakimu/jaji kulingana na level ya mahakama.
 
Ila hukumu ikitolewa tuwe tunashangilia hivi hivi kwa kujikumbusha zaidi naomba mkasome kitabu cha kesi ya uhaini sehemu ya 1&2 jinsi kesi ilivyoendeshwa mpaka hukumu ilivyotolewa
Hivi kwa aina hii ya mashahidi wa design ya Mahita you can predict judgement.... na bahati mbaya mahakamani kila shahidi ana anaweza kuwa na athari kwenye hukumu.... hivi kweli huyu mahita alijua kabisa akuja kufanyiwa cross -examination?

hivi kweli shahidi uliyemuandaa aseme alisahau, sikumbuki, nitakuwa niliandika..... kweli kulikuwa na haja ya kuwa na shahidi kama huyu? yani polisi mzima una sahau kuandika kama uliwafunga pingu watu unao waita magaidi? polisi mzima hujui taratibu za kusachi mtuhumiwa?
Kwanii Dpp asiondoe hii case ya kujidhalilisha? hii ni aibu...kwa aina hii ya mashahidi...
Hii ni case ya kufuta serikali haiwezi shinda kamwe.... ujinga mtupu
 
Watu wanaongelea contents za mwenendo wa kesi. Hukumu itabaki kuwa hukumu, haitazuia contents zilivyotolewa. Ndio maana kwa kesi hiyo hiyo na contents zake watu hukata rufaa na kupata majibu tofauti. Hivyo, hukumu mwachie hakimu.
Ni Jaji, siyo hakimu
 
Jinsi wakili msomi Dickson Matata alivyompeleka puta mtoto wa IGP Mahita.

MATATA: Nikumbushe Majina yako.

SHAHIDI: Naitwa Inspector Mahita Omary Mahita.

MATATA: nitakuwa Sahihi nikisema wewe ni Mtoto wa IGP mstaafu Omary Mahita.

SHAHIDI: Upo sahihi

MATATA: Wakati Baba yako akiwa IGP wewe Ulikuwa wapi?

SHAHIDI: Nilikuwa Chuo kikuu

MATATA: Wakati Baba yako akiwa IGP ulikuwa na akili timamu?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Unakumbuka madai ya baba yako kuwakuta CUF na visu akadai wamekusudia kufanya ugaidi.

WAKILI WA JAMHURI: Objection Mheshimiwa Jaji. Naomba swali hilo liondolewe.

MATATA: Wakati mnawakamata watuhumiwa mlikuwa na Kikosi Maalum?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Kikosi chote kilitokea Arusha?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Na kikosi hicho kilikuwa chini ya RPC Kingai ambaye wakati huo alikua RCO Arusha?

SHAHIDI: Sahihi kabisa

MATATA: Unapotoka kwenye kituo unapaswa kuwa na Movement Order?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Ulipotoka Arusha kwenda Moshi hukueleza kuwa na movement order.

SHAHIDI: Nilikua nayo.

MATATA: Ulimweleza nani?

SHAHIDI: Sikueleza lakini nilikua nayo

MATATA: Maelezo yako ya awali hayaelezi hivyo.

SHAHIDI: Kimya.

MATATA: Je unajua kwamba unapofika mkoa mwingine unapaswa uriporti kwanza kwa Mlmamlaka za Mkoa huo?

SHAHIDI: Ni kweli.

MATATA: Katika maelezo yako hakuna popote uliposema umeripoti kwa mamlaka za polisi Moshi.

SHAHIDI: Ni kweli lakini?

MATATA: Hakuna lakini, jibu NDIYO au HAPANA.

SHAHIDI: Niliripoti lakini labda kwenye maelezo nilisahau kuandika.

MATATA: sasa kama hukuandika ulitegemea mahakama iote?

SHAHIDI: Kimya

MATATA: Una ushahidi wowote unaoonesha mliripoti mamlaka za polisi Moshi kabla ya operesheni yenu?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Uko wapi?

SHAHIDI: sijaja nao

MATATA: mlipowakamata watuhumiwa mliwasafirisha kuja Dar?

SHAHIDI: Ndio

MATATA: walipofika Dar mliwatoa central na kuwapeleka Mbweni?

SHAHIDI: Ni kweli.

MATATA: Kwanini mliwapeleka Mbweni?

SHAHIDI: Kwa sababu ya usalama.

MATATA: Kati ya Cetral na Mbweni wapi kuna usalama zaidi?

SHAHIDI: Lakini..

MATATA: Jibu, acha lakini.

SHAHIDI: Mbweni.

MATATA: Kati ya Central na Mbweni wapi kuna askari wengi?

SHAHIDI: Central.

MATATA: Kati ya central na Mbweni wapi kuna silaha nyingi zaidi?

SHAHIDI: Central.

MATATA: Kati ya central na Mbweni wapi panaweza kupatikana msaada wa haraka ikitokea dharura?

SHAHIDI: Central.

MATATA: Sasa unasemaje Mbweni kuna usalama kuliko central?

SHAHIDI: ili watuhumiwa wasiweze kutoroka.

MATATA: Umewahi kusikia pale central kuna watuhumiwa wametoroka?

SHAHIDI: kimya

MATATA: Jibu swali, umewahi kusikia watuhumiwa kutoroka central?

SHAHIDI: wangeweza kutoroka.

JAJI: Mbona swali rahisi, jibu kama umeshawahi kusikia wametoroka?

SHAHIDI: Mheshimiwa Jaji mimi sijui.

MATATA: Kwanini mliwapeleka watuhumiwa Mbweni?

SHAHIDI: Ni kwa maelekezo ya viongozi wangu.

MATATA: Nakuuliza wewe, sio viongozi wako.

SHAHIDI: Kama nilivyosema ni sababu za kiusalama.

MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba mlipowaleta watuhumiwa Dar hujasema mliripoti kwa nani?

SHAHIDI: Tuliripoti kwa mamlaka za polisi kanda maalumu na mkoa wa kipolisi Kinondoni.

MATATA: Kwenye taarifa yako kuna mahali umeeleza hayo?

SHAHIDI: Hapana.

MATATA: Unaelewa kabla ya kuwasachi watuhumiwa, ilibidi nyie mlisachiwe kwanza?
shahidi ni kweli sijazungumza hilo.

SHAHIDI: Ndio

MATATA: Lakini kwenye maelezo yako hujaeleza ka mlisachiwa kwanza kabla ya kuwasachi watuhumiwa.

SHAHIDI: Tulisachiwa japo sijaeleza.

MATATA: Kwa kuwa hujaeleza nitakosea nikisema hamkusachiwa.

SHAHIDI: Kimya.

MATATA: Umeeeleza kuwa watuhumiwa ni Makomandoo wa JWTZ?

SHAHIDI: Ni kweli.

MATATA: Utakubaliana na mimi kwamba Makomandoo ni watu ambao wanahitaji ulinzi zaidi?

SHAHIDI: Sahihi.

MATATA: Lakini katika maelezo yako hakuna popote umesema mliwasifirisha kwa pingu? Je utakubaliana na mimi nikisema mliwasafirisha makomandoo wa jeshi kizembe bila kuwafunga pingu?

SHAHIDI: Tuliwafunga

MATATA: Lakini maelezo yako uliyoandika hayaelezi hivyo.

SHAHIDI: Itakua nilisahau tu.

MATATA: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.!

Malisa GJ

View attachment 1942312
My classmate,nafurahi kuona akifanya vizuri.
 
Maelekezo ya msingi aliyopewa shahidi namba moko ni kuhakikisha hiyo mipango haifanikiwi lakini wakati huo huo kuona mtuhumiwa ana nia hiyo kweli? Kwa mfano ikitokea hao makomandoo Mbowe alitafutiwa na yule Mwanajeshi aliye toa taarifa na akaombwa kuendelea kutoa ushirikiano utasema nini tena? Kumbuka wako mashahidi 24.
Samahani mkuu, mimi sio mtaalam wa sheria, naomba unielimishe.

Hivi mtu anahukumiwa kwa kutenda kosa, au anahukumiwa kwa kua na nia ya kutenda kosa?

Hebu tuassume kweli Mbowe alikua na nia ya kulipua vituo vya mafuta. Je anaweza kutiwa hatiani ingawa hakulipua kituo chochote?
 
Mimi nimezungumzia makomandoo kuwepo kwenye hiyo kesi ya Mbowe na jinsi shutuma hizi zilivyo ripotiwa polisi mpaka kuonekana
ni muhimu kutolewa maagizo ya kufaywa investigation yake. Nilisoma mahali Mbowe alimuomba msaada huyo mwanajeshi aliye ripoti tuhuma hizi polisi. Ni msaada gani kesi inavyoendelea na amini tutaelewa
 
Ok sawa.
 
Back
Top Bottom