Jinsi watu wa mikoani tunavyofanyiwa tunapoagiza bidhaa toka kwa watu wa Dar es Salaam

Habari za asubuh ndugu wana jf.
Leo nimekuja kutoa mikasa miwili mitatu jinsi watu wa mikoani tunavyofanyiwa pale tunapoagiza bidhaa toka huko dar es laam.

KISA CHA KWANZA niliwah ona page 1 ya facebook & instagram ambayo inapost nguo nzuri sana za dukani hasa mashati, kwakua nilipenda basi nikachukua namba yao nikaagiza shati 4 kutokana na picha ya shati nilizozipenda basi nikawatumia whatsap waone zile shati 4 alafu wanitumie mzigo had mkoa nilipo.

NIkawatumia pesa kamili ya mzigo ila pesa ya usafiri nililipa nilipochukua mzgo. Kuja kutahamaki katika zile shat 4 nilizotuma picha anitumie ni shat 1 tu ndio niliyochagua na nyingine 3 ni shati tofauti kabisa yani mara nyingne oversize,nyngne ipo vile, nilivyompigia hakuweza kupokea tena simu.
KISA CHA PILI, nilipata mtu anayeuza simu dar , nikaagiza simu samsung a24 , ram 6 ,rom 128, nilimtumia pesa kamili ya simu na pesa ya transport, ila nilipopokea simu nilikuta ni RAM 4 rom 128, japo ni simu mpya na ni nzuri ila alileta ulaghai kwenye Ram kadr ya tulipokubaliana, nilipompigia nae hakuwa na jibu.

Hivyo basi, wafanyabiashara wa daslama, tunaomba muwe mnaenda ndani ya makubaliano, sio kila mtu anaweza kufika dar au ana ndugu dar.
Wewe ni mtu wa hovyo, kumuamini kiumbe wa kiswahili ambaye humjui na humuoni, sio Dar tu, kokote unapigwa, kuna wale wa Pemba au Tanga, watakufrahisha ukiendelea na tabia yako hiyo ya kijinga.
 
Habari za asubuh ndugu wana jf.
Leo nimekuja kutoa mikasa miwili mitatu jinsi watu wa mikoani tunavyofanyiwa pale tunapoagiza bidhaa toka huko dar es laam.

KISA CHA KWANZA niliwah ona page 1 ya facebook & instagram ambayo inapost nguo nzuri sana za dukani hasa mashati, kwakua nilipenda basi nikachukua namba yao nikaagiza shati 4 kutokana na picha ya shati nilizozipenda basi nikawatumia whatsap waone zile shati 4 alafu wanitumie mzigo had mkoa nilipo.

NIkawatumia pesa kamili ya mzigo ila pesa ya usafiri nililipa nilipochukua mzgo. Kuja kutahamaki katika zile shat 4 nilizotuma picha anitumie ni shat 1 tu ndio niliyochagua na nyingine 3 ni shati tofauti kabisa yani mara nyingne oversize,nyngne ipo vile, nilivyompigia hakuweza kupokea tena simu.
KISA CHA PILI, nilipata mtu anayeuza simu dar , nikaagiza simu samsung a24 , ram 6 ,rom 128, nilimtumia pesa kamili ya simu na pesa ya transport, ila nilipopokea simu nilikuta ni RAM 4 rom 128, japo ni simu mpya na ni nzuri ila alileta ulaghai kwenye Ram kadr ya tulipokubaliana, nilipompigia nae hakuwa na jibu.

Hivyo basi, wafanyabiashara wa daslama, tunaomba muwe mnaenda ndani ya makubaliano, sio kila mtu anaweza kufika dar au ana ndugu dar.
Kama wanaoenda physically wanapigwa iweje wewe ambaye upo mbali...!!

Hawezi kukuogopa wewe uliyopo mbali maana huwezi kumharibia hata kidogo akikupiga.

Kupigwa kunauma, bora upigwe ukiwa physically ambapo lazima atumie akili kukupiga kuliko na ukiwa mbali ambapo haumizi kichwa kukupiga. Ukiwa physically hauwezi kujilaumu sana kwani utajua udhaifu wako ulipo.
 
Usije ukarogwa ukaagiza kitu Zanzibar..utalia sana.tena unakuja kuta kitu cha milion mbili wanakwambia 1.2milion ukijaaa..imeishia

Bongo bado hakuna online platform..mtalia sana
Yule jamaa wa wete Zanzibar ni tapeli yupo Dar ana accounts Instagram kama 10 hivi ,watu wanapigwa daily.
 
Mimi nimeagiza mara nyingi sana kwa wauzaji wa online tofauti tofauti toka dar nikiagiza leo kesho mzigo nimepata na ukiwa tofauti huwa nawajulisha nawarudishia kwa gharama zao wanabadilisha kama hamna huwa wananipa option ya kurudishiwa hela au kuchagua bidhaa nyingine.
 
Hii nzr
 
Bac ao ni waminifu.
 
Biashara ya kuaminiana bila kujuana kwa kina au uwepo wa dhamana ya uhakika achana nayo kabisa, hata ndugu sio watu wa kuamini.
Sio watu wa Dar tu, hata watu wa mikoani, wahuni na matapeli wametapakaa nchi nzima.

Hatari za tuma pesa nikutumie bidhaa ni hizi.
1. Kutapeliwa pesa.
2. Kuchelewa kupata bidhaa zako.
3. Kuletewa bidhaa duni (kuna bidhaa feki na bidhaa halisi lakini zenye mapungufu)
4. Bidhaa kupotea njiani au kuharibika njiani. (Wauzaji ni wengine na wasifirishaji ni wengine, na hawana uhusiano)
 
Tatzo mkuu huku mikoan simu ya laki 5 ,uko dar n lak 4 na 20 labda, na sio rahisi kumfaham/ kujuana na mwenye duka la simu uko dar, kwahyo unajikuta unaagiza kwa mtu wa jf tu.
We sema km unahitaji biashara,kuna watu wako golini hapo kkoo bongo.
Utaletewa chochote,pesa unatoa unataftiwa kitu unachotaka kinaletwa.
Haina utapeli wowote ni biashara tu.
Ogopa sana mitandao
 
Mbna ni yaleyale tu mkuu
 
Biashara ya kuaminiana bila kujuana kwa kina au uwepo wa dhamana ya uhakika achana nayo kabisa, hata ndugu sio watu wa kuamini.
Sio watu wa Dar tu, hata watu wa mikoani, wahuni na matapeli wametapakaa nchi nzima.

Hatari za tuma pesa nikutumie bidhaa ni hizi.
1. Kutapeliwa pesa.
2. Kuchelewa kupata bidhaa zako.
3. Kuletewa bidhaa duni (kuna bidhaa feki na bidhaa halisi lakini zenye mapungufu)
4. Bidhaa kupotea njiani au kuharibika njiani. (Wauzaji ni wengine na wasifirishaji ni wengine, na hawana uhusiano)
Mkuu upo sahh sana, asante kwa ushauri wako mzuri.
 
Back
Top Bottom