Jinsi wenye mafanikio wanavyotudanganya

Jinsi wenye mafanikio wanavyotudanganya

Huu ndio ukweli..
Huwezi kuwa bilionea kwa kuanza na mtaji au biashara ya kawaida (ndogo) and then eti ndiyo hiyo hiyo ikukuze mpaka uwe bilionea.
Lazima, ukwapue sehemu au ufanye janja fulani ili ukue zaidi.
Ndiyo maana biashara haramu zipo kwa ajili hiyo.
Sasa wewe komaa na laki mbili kama mtaji wako huku ukitegemea kuwa bilionea, haitatokea.
 
changamoto kwa wasomi wengi ni kubadilisha shule/elimu alopata kuwa PESAaaaaaa

walioweza jinasua kwenye matumizi ya nadharia (application of theories) kwenye uhalisia (real life) wamefanikiwa sana
 
Mengi alianza na Ball point pen na mtaji wa kwanza ulikuwa Idea wapili negotiation na wazalishaji pen walivyokubakiana wa import mzigo faida ikisomeka awawsilishie pesa.
Jidanganye tu,ulitaka Mengi akiambie mikopo aliyo default?
 
Mengi alianza na Ball point pen na mtaji wa kwanza ulikuwa Idea wapili negotiation na wazalishaji pen walivyokubakiana wa import mzigo faida ikisomeka awawsilishie pesa.
Unajua hapo wkt Mengi anaanza biashara alikua ni Managing Patner wa Cooper Brothers kwa sasa ikijulikana kama PriceWaterHouseCoopers- PWC?

Usidhani alikua Maskini hata kidogo alikua tajiri tu kwa mazingira ya kibongo bongo,Mengi exposure huko Ulaya ilimsaidia sana,kufanya Auditing kwny Mashirika ya Umma+Ma Co. makubwa ya private kulimfanya akajua sana jinsi yanavyo operate na akatake advantage+Uthubutu wake.

All in all mafanikio ni mchanganyiko wa factors mbalimbali.

Na-declare kuna watu nimewaona wameanzia chini kabisaa na sasa ni matajiri wa kiukweli ukweli,chochote kinawezekana tu.
 
Katika utajiri wa watu wengi,kuna msukumo wa namna flani uliowawezesha kufika hapo walipo,lakini sio mapambano tu ya kawaida,mfano mtu kaiba hela serikalini katajirikia halafu mwisho wa siku anataka kusadikisha watu kuwa alifuata rules flani ndio maana kawa tajiri...
Ki-ukweli kabisa sijawahi kuona mtu yoyote yule aliyefanya kazi serikalini nikimaanisha halmshauri/jiji/mashirika ya umma then akawa tajiri bila kuiba hela ya serikali hayupo hata mmoja.

Wote wezi wezi walidokoa sehemu wakaanzisha vimiradi vyao wakatoboa lkn story za walidunduliza sijui nini hakuna kitu kama hicho.
 
Ki-ukweli kabisa sijawahi kuona mtu yoyote yule aliyefanya kazi serikalini nikimaanisha halmshauri/jiji/mashirika ya umma then akawa tajiri bila kuiba hela ya serikali hayupo hata mmoja.

Wote wezi wezi walidokoa sehemu wakaanzisha vimiradi vyao wakatoboa lkn story za walidunduliza sijui nini hakuna kitu kama hicho.
Trueeeee
 
Uzuri dangote hajawahi kuficha story za utajiri wa babu zake.

Hata mtaji wake hua anasema waziwazi alipewa na hao hao ndugu zake miaka hio,na anasemaga wmtaji aliopewa kipindi ni pesa ambayo mtu angeweza kununua mercedes benz mpya 10 kwa miaka hio.

So hapo utajiongeza na kujua alipewa mtaji heavy wa kuanza biashara ya Cement za jumla jumla.
 
Ndio kona kona na ujanja ujanja! Sio kwa Africa tu. Ni duniani kote kwa ujumla..lazima ucheze na system ili ufike juu. Hakuna bilionare yoyote duniani ambae hajacheza na system.
Hata bill gates/warren buffet wana makando kando ya kufa mtu.

Trump ndo hata usimseme amegoma kutoa tax returns zake za miaka 10 iliyopita mpk Judge amelazimisha azitoe zifanyiwe uchunguzi.
 
Naamini ipo siku biashara yangu ya uuzaji asikirimu nitakua Kama bakhera...[emoji12]
Maisha ni hatua mkuu.
 

Attachments

  • tapatalk_1570449182994.jpeg
    tapatalk_1570449182994.jpeg
    32.1 KB · Views: 3
Konde boy alianzia chini, sa ivi anagawa hela jukwaani.

Pia Makonda kuna picha za zamani alikua choka mbaya sa ivi yuko hapo alipo.
The Masanja na wenzake walikua choka mbaya, sa ivi wana magari ya kubadilisha kuanzia jumapili mpaka jumaosi.

Tatizo hapo katikati huwa hatuambiwi ukweli walifanyaje, labda mfano kujipendekeza kwa wakubwa, kuuza unga, walisoma elimu ya juu zaidi, walienda kanisani na kuombewa etc. huwa hawatamki kabisa, ili na sisi tuwe matajiri.
Na hapo huwezi kukuta panatankwa mahali popote kwa kuwa ndio maisha ya mtu yalipo, hiyo ndio siri. (Ya mtu mmoja)
 
Back
Top Bottom