Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 11,191
- 35,870
Mnamo 1989, house boy wa ki-Thai aliyekuwa akifanya kazi katika jumba la kifalme la Saudi Arabia huko Riyadh aliiba mamia ya pauni za vito, ikiwa ni pamoja na almasi ya bluu ya karati 50. Alisafirisha nyara hizo hadi Thailand ndani ya vacuum cleaner kupitia kampuni ya usafirishaji ya DHL.
Saudi Arabia ilipodai vito hivyo virejeshwe, polisi wa Thailand walidai walikuwa wamevipata. Lakini vitu hivyo viliporudishwa, vipande vingi vya thamani zaidi, ikiwa ni pamoja na almasi maarufu ya bluu, vilikuwa havipo au kubadilishwa na bandia.
Kashfa hiyo iligeuka kuwa mbaya. Wanadiplomasia watatu wa Saudi Arabia waliokuwa wakichunguza huko Bangkok waliuawa katika usiku mmoja. Mfanyabiashara wa Saudi Arabia aliyehusishwa na kesi hiyo pia alitoweka kusiko julikana.
Wakiwa na hasira kwa kile walichokiona kama kufanyiwa utapeli, Saudi Arabia ilikata uhusiano wote wa kidiplomasia na Thailand kwa zaidi ya miaka 30. Walipiga marufuku wafanyakazi wa Thai na kuweka vikwazo vya kiuchumi ambavyo viliigharimu Thailand mabilioni.
Wizi wa mtu mmoja, pamoja na ufisadi wa kiwango cha juu, uliunda moja ya migogoro ya kidiplomasia ya ajabu na yenye uharibifu zaidi katika historia ya kisasa.