JInsi ya Kuagiza Bidhaa China Kupitia Alibaba

JInsi ya Kuagiza Bidhaa China Kupitia Alibaba

Heritage123

Member
Joined
Jul 24, 2023
Posts
51
Reaction score
100
Unataka kuanza kuagiza bidhaa kutoka China lakini hujui wapi pa kuanzia?
Alibaba.com ni moja ya mitandao mikubwa duniani ya wauzaji wa jumla ambapo unaweza kuagiza bidhaa kwa bei nafuu, kutengeneza brand yako mwenyewe (OEM), au hata kuanzisha biashara ya kuuza kwa mtandao (Dropshipping, Reselling n.k.).
Katika blogpost hii, nitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kuagiza bidhaa kutoka China hadi Tanzania kupitia Alibaba, ukiwa na simu yako tu.

🔹 1. Fungua Account Alibaba​

Tembelea www.alibaba.com kisha:
✔️ Bofya “Sign Up”
✔️ Jaza taarifa zako: jina, email, password
✔️ Chagua “Buyer Account”
👉 Ni bure kabisa.

🔹 2. Tafuta Bidhaa Unayotaka​

Katika search bar, andika bidhaa unayotaka, mfano:
  • “Wireless Earbuds”
  • “Kids Shoes”
  • “Kitchen Set”
Tips:
✅ Tumia filter: Trade Assurance, Verified Supplier, Ready to Ship
✅ Chagua wauzaji walio na reviews nzuri na miaka mingi ya uzoefu

🔹 3. Wasiliana na Supplier (Muuzaji)​

Bofya “Contact Supplier” au “Chat Now”
Muulize:
  • MOQ (Minimum Order Quantity)
  • Bei ya kila item (unit price)
  • Gharama ya usafirishaji (Shipping cost)
  • Aina ya usafirishaji (Air, Sea, DHL, FedEx n.k.)
  • Muda wa kutengeneza mzigo (Production Time)
  • Njia ya malipo (Payment method)
✅ Andika kwa Kiingereza rahisi na heshima

🔹 4. Omba Sampuli Kama Unaweza​

👉 Kama ni order ya bei kubwa, omba sample (mfano) uione kabla ya kulipia mzigo mzima
Unaweza kulipia kupitia:
✔️ Trade Assurance (Salama zaidi)
✔️ Western Union
✔️ T/T (Bank Transfer)
✔️ Paypal (kama wanakubali)

🔹 5. Lipia na Fuatilia Order Yako​

Ukisharidhika na supplier:
➡️ Malizia maelewano
➡️ Lipia kupitia Trade Assurance (inalinda pesa yako)
➡️ Omba tracking number au invoice
⏳ Muda wa kutengeneza mzigo huwa siku 5–20 kulingana na aina ya bidhaa

🔹 6. Usafirishaji: Njia 2 Kuu​

A) Air Freight (Haraka lakini gharama juu)​

  • Inafika ndani ya siku 7–15
  • Inapendekezwa kwa mzigo mdogo au wa haraka
  • Unaweza kutumia DHL, FedEx, UPS n.k.

B) Sea Freight (Polepole lakini bei rahisi)​

  • Inachukua wiki 4–6
  • Inafaa kama mzigo ni mkubwa
  • Unahitaji clearing agent Tanzania
📌 Kuna agents Bongo wanaweza kukuletea mzigo wako hadi Dar es Salaam (door-to-door delivery)

🔹 7. Pokea Bidhaa na Uanze Kuuza​

Ukipokea mzigo:
  • Hakikisha bidhaa hazina kasoro
  • Piga picha nzuri
  • Tumia Instagram, TikTok, WhatsApp au duka la mtandaoni kuuza
💡 Ukiwa na consistency na marudio mazuri ya order — unakuwa mtaalamu wa import business

⚠️ Tahadhari Unazopaswa Kuchukua​

✅ Usilipe kwa njia zisizo salama
✅ Usikubali kupokea mzigo usio na tracking
✅ Fuatilia reviews za supplier
✅ Usikubali offer ambazo ni “too good to be true”

💡 BONUS: Unahitaji Mwongozo wa Kuanza?​

Nimeandaa eBook ya A to Z ya Kuagiza Bidhaa China kwa Kiswahili
Ndani utapata:
  • Template za kuwasiliana na supplier
  • List ya bidhaa 100 zenye demand Tanzania
  • Agencies bora wa clearing & delivery
  • Gharama halisi + faida unayoweza kupata
📘 Bei: 9500 TZS tu (Softcopy PDF)
📲 Pata kupitia WhatsApp: 0623 684 510
 
Hivi tv ya 250,000 hapa bongo china nitauziwa Kwa bei gani
 
Nawezapata gym supplements bora ie zilizothibitiswa China ?
 
Back
Top Bottom