Jinsi ya kuandika Tangazo lako la biashara mtandaoni

Jinsi ya kuandika Tangazo lako la biashara mtandaoni

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
1,468
Reaction score
2,767
ZINGATIA:

Hakuna mafanikio yanayokuja kiurahisi, utahitaji juhudi, muda, uvumilivu na kujifunza Zaidi mpaka kupata matokea hivyo usitegemee kupata matokeo ya haraka unapoanza kufanya ishu yoyote mtandaoni.

Haya tuangalie njia hizi.....

1. Uhandishi wa maudhui mtandaoni (Online Content writing).

Uandishi wa Makala katika Blog na Tovuti (Websites).

Kuandaa post kwaajili ya kuweka katika mitandao ya kijamii.

Ujuzi unaohitaji

• Ujuzi wa kuandika.

• Kutambua na kutumia maneno muhimu (keywords).

• Uwezo wa kuchambua taarifa.

• Kufahamu seo (Search Engine Optimization).

2. Kuuza ujuzi wako mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii na freelancing platforms kama Upwork na Fiverr.

Juzi unazoweza kuuza mtandaoni

• Kutafsiri lugha mbalimbali.

• Uandishi wa Makala

• Kusimamia mitandao ya kijamii ya watu au kampuni.

• Graphic design

• Wataalamu wa masuala ya seo

• Web design na App developers

3. Udalali /Uuzaji wa ushirika (Affliate marketing).

Unapata gawio kwa kuuza bidhaa za watu wengine.

Unaweza tumia mitandao yako ya kijamii au kuwa na blog ama Tovuti (Website) maalumu kwaajili ya kuuzia bidhaa hizo.

4. Uza bidhaa zako binafsi mtandaoni.

Jifunze kuuza mtandaoni kisha anza kuuza bidhaa au huduma yako mtandaoni.

Inaweza kuwa huduma pia kuuza mtandaoni inawezekana na wateja wengi kwasasa wapo mitandaoni hivyo ni rahisi kuwafikia ikiwa utakuwa na mbinu sahihi za kuwatafuta.

Unaweza kuongezea njia nyingine zaidi katika comment
png_20211213_210423_0000.jpg
 
Habari!
Binafsi nashauku kubwa sana ya kufanya biashara mitandaoni lkn sijui najiunga kufanya hivo. Ungetoa muongozo jinzi ya kujiunga mpk kuuza ungetusaidia wengi.
Hebu tililika ndugu
 
Habari!
Binafsi nashauku kubwa sana ya kufanya biashara mitandaoni lkn sijui najiunga kufanya hivo. Ungetoa muongozo jinzi ya kujiunga mpk kuuza ungetusaidia wengi.
Hebu tililika ndugu
Asante sana mkuu.

Jambo muhimu na la kwanza ni kuwa na mpango mkakati wa kile unachoenda kufanya mtandaoni na mpango huo unaweza kuzingatia mambo yafuatayo:-

1. Tambua nini unaenda kuuza mtandaoni.

Je ni huduma/biashara ambayo tayari unayo hivyo unataka kuiamishia tu mtandaoni au ni kitu kipya ambacho unataka kuanza moja kwa moja mtandaoni?

2. Elewa hicho unachoenda kufanya kipo katika kundi gani ili iwe rahisi kujua unaenda kutengeneza maudhui ya aina gani katika kutangaza bidhaa/huduma yako mtandaoni.

Hii wengi huitambua kama "niche".

Kwa mfano:

kama unauza accessories za simu na computer, niche yako itakuwa katika kundi la mambo ya Teknolojia.

Kama una uza dawa/vyakula vya kupunguza uzito, "niche" yako itakuwa masuala ya Afya upande wa Kupunguza uzito.

Unaweza kukaa na kuangalia wewe biashara yako inaangukia kundi gani.

(Unaweza kuweka hapa pia aina ya biashara yako ili kukusaidia kutambua lipo kundi gani)

3. Jifunze na kuwasoma washindani wako. Fanya tafiti ya kufuatilia wale wanaofanya biashara kama yako mtandaoni.

Hapa angalia ni njia gani wanatumia hasa katika kujitangaza mtandaoni.

Je ni platform zipi wanazitumia sana katika kujitangaza.

Je wanatumia sana mitandao ya kijamii au tovuti (Websites) ?

4. Baada ya kujifunza kutoka kwa washindani wako sasa kaa angalia njia gani nyepesi ya kuanza. Chagua njia moja au mbili wakati wa kuanza, kama ni (tovuti) website au mitandao ya kijamii kisha taratibu utaanza kujitanua katika majukwaa mengine mtandaoni.

5. Muhimu sana kuweka biashara yako Google My business.

Hii ni platform ya bure inayosaidia biashara yako kuonekana Google na kwenye Google map.

Baada ya kupitia hivyo vipengele vitano naomba kama una swali lolote uliza nitakujibu hapahapa mkuu.
 
ZINGATIA:

Hakuna mafanikio yanayokuja kiurahisi, utahitaji juhudi, muda, uvumilivu na kujifunza Zaidi mpaka kupata matokea hivyo usitegemee kupata matokeo ya haraka unapoanza kufanya ishu yoyote mtandaoni.

Haya tuangalie njia hizi.....

1. Uhandishi wa maudhui mtandaoni (Online Content writing).

Uandishi wa Makala katika Blog na Tovuti (Websites).

Kuandaa post kwaajili ya kuweka katika mitandao ya kijamii.

Ujuzi unaohitaji

• Ujuzi wa kuandika.

• Kutambua na kutumia maneno muhimu (keywords).

• Uwezo wa kuchambua taarifa.

• Kufahamu seo (Search Engine Optimization).

2. Kuuza ujuzi wako mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii na freelancing platforms kama Upwork na Fiverr.

Juzi unazoweza kuuza mtandaoni

• Kutafsiri lugha mbalimbali.

• Uandishi wa Makala

• Kusimamia mitandao ya kijamii ya watu au kampuni.

• Graphic design

• Wataalamu wa masuala ya seo

• Web design na App developers

3. Udalali /Uuzaji wa ushirika (Affliate marketing).

Unapata gawio kwa kuuza bidhaa za watu wengine.

Unaweza tumia mitandao yako ya kijamii au kuwa na blog ama Tovuti (Website) maalumu kwaajili ya kuuzia bidhaa hizo.

4. Uza bidhaa zako binafsi mtandaoni.

Jifunze kuuza mtandaoni kisha anza kuuza bidhaa au huduma yako mtandaoni.

Inaweza kuwa huduma pia kuuza mtandaoni inawezekana na wateja wengi kwasasa wapo mitandaoni hivyo ni rahisi kuwafikia ikiwa utakuwa na mbinu sahihi za kuwatafuta.

Unaweza kuongezea njia nyingine zaidi katika comment View attachment 2043683
Long plan ahead 6months up to 2 yrs ya mwanzoni atleast kuanza kupata effectively kile unachotaka bila kusahau low expectaction,nimeona lots of startups zikifa coz ya high expectation
 
Moja kati ya kosa ambalo Wafanyabiashara wengi wanalifanya, ni kudhani kuwa ukishafungua Fremu yako ya biashara hapo mtaani kwako au sokoni basi umemaliza.

Aisee, ulimwengu kwasasa umebadilika sana na staili hiyo ya kufanya biashara ilikuwa ni ya zamani sana. Kwasasa ili utoboe kwenye biashara unahitaji kujiongeza haswa katika eneo la masoko.

Ushindani umekuwa mkubwa sana, ebu jaribu kupanua wigo wa biashara yako kufikia watu wengi zaidi hasa hasa mtandaoni. Usiishie hapo ulipo.

Tupe uzoefu wako tujifunze, wapi ulipo kwasasa? Kwenye Fremu au Fremu na mtandaoni pia?
Biashara%20mtandaoni%20Jinsi%20ya%20kuuza%20mtandaoni.jpg
 
Ulishawahi kukutana na tangazo likakukatisha tamaa ya kununua?

Wafanyabiashara wakati mwingine wanadhani tunawaza jinsi wanavyowaza wao wakati wanaandika tangazo la biashara.

Fanya haya wakati wa kuandaa tangazo la bidhaa yako Facebook, Instagram au mtandao wowote wa kijamii.

1. Tumia Lugha nyepesi ya kueleweka
Epuka kutuonyesha kuwa wewe unajua sana Kiswahili au Kiingereza na kuanza kutuandikia maneno magumu kwenye tangazo lako.

Andika tangazo kama unaongea na mtu kawaida na kwa lugha ya mtaani.

2. Punguza Maelezo mengi
Ni kweli unaielewa bidhaa yako vizuri ila sasa ebu tupunguzie maelezo ndugu.

Andika tu kwa ufupi na ueleze vitu vya msingi tu kuhusu bidhaa yako na sisi tutakuelewa.

3. Weka namba ya Simu
Mimi sijui unapokaa, nimekutana na tangazo lako mtandaoni halafu unataka kunipa adhabu ya kuanza kubashiri nitawasiliana vipi na wewe nipate bidhaa yako.

Aisee tuwekee namba ya simu kwenye tangazo lako tafadhali.

4. Toa Maelezo ya kueleweka kwa njia gani na wapi mteja anaweza kupata huduma
Boss tangazo tumeliona, ila sasa unapatikana wapi na bidhaa hii naipataje. Tuwekee Maelezo hayo wazi kuturahisishia kazi ya kupata huduma au bidhaa yako.

5. Weka bei na punguza masuala ya "Njoo WhatsApp"
Hii inaeleweka ila ni vile tu unataka kutusumbua [emoji23], ebu tuwekee bei ya bidhaa kwenye tangazo la biashara yako tafadhali.

6. Hakikisha tangazo lako linasomeka
Ukimaliza kuandika, tafadhali rudia kusoma ulichoandika. Usiwe na haraka ya kumaliza kazi bali kutoa kazi nzuri hatakama itachukua muda.

Usitupe adhabu ya kuanza kubashiri sijui hapa alimaanisha "Mavazi" au "Makazi".

Vipi umeona utofauti?

Bila shaka utatuandikia vizuri matangazo mengine.

Usisahau kurekebisha post na matangazo yako ambayo tayari ulishaweka huko nyuma na yana makosa.

Jinsi%20ya%20kuandika%20Tangazo%20la%20biashara%20mtandaoni.jpg
 
Kweli kabisa wakati unaandika tangazo lazima ujue linamlenga nani. Je, ni watumiaji wa kawaida au ni wale wenye ujuzi mfano kama watu wa IT.

Kama ni watu wa kawaida wambie watafaidikaje badala ya kuwaambia sifa (features) za bidhaa yako.
Mfano: Unauza flash ya 1GB, kama walengwa ni watu wa kawaida badala ya kuwaambia hii flash in 1GB, wambie hii flash inaweza kubeba movie 50, au inaweza kubeba nyimbo 500.

Baadala ya kuwaambia hili koti limetengenezwa sijui kwa linen, we sema hili koti hata unyeshewe mvua kuanzia asubuhi mpaka jioni haliwezi kulowana au maji hayapenyi kukulowanisha.

Nadhani hii inapply hata kwa wanasiasa wa upinzani. Baadala ya kusema viongozi wameiba bilioni 200, wambie wananchi viongozi wameiba pesa ya kujenga zahanati 800 zikiwa na vitanda na magodoro na mashine za kupima magonjwa. Hapo watakuelewa zaidi maana mtu hajawahi kushika hata milioni 10, bilioni 200 hawezi kujua ni kubwa kiasi gani.

Kama tangazo limelenga wataalam, basi hao wape features za bidhaa yako.

Copywriting....
 
Nimeongeza kitu kikubwa sana mkuu.

Asante sana kwa Maelezo haya boss.

Mifano mepesi na ya kueleweka.
 
Nauza gesi huwa nafanya free delivery Kuna wateja wengi hawaijui ofisi yangu ,
Napiga pesa safi
 
Nauza gesi huwa nafanya free delivery Kuna wateja wengi hawaijui ofisi yangu ,
Napiga pesa safi
Kuna la kujifunza hapa. Shukrani sana mkuu.

Umeweka mtangazo mtaani au wanatokea mtandaoni?
 
Back
Top Bottom